Masuala ya wananchi ni ya CCM

Masuala ya wananchi ni ya CCM

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
1,505
Reaction score
4,427
Tunaweza kushangazwa na uhusika wa CCM kila janga linapotokea, pengine inaweza kufikiriwa kwamba kwa sababu ndio ina serikali hivyo haina budi kuonesha uhusika wake au wengine wanaweza kusema ni CCM imetengeneza tukio na ili ionekane ina wajali wananchi wake walitatue.

Yote kwa yote, mawazo ya mwanadamu huwa yanafika mbali ya ukubwa wa tatizo. Sijawahi kusikia mwanadamu katengeneza tetemeko lakini CCM ilikuwa pamoja na wananchi wa Bukoba mwanzo mpka mwisho, sijawahi kusikia mwanadamu katengeneza mafuriko lakini CCM ipo pamoja na wahanga wa mafuriko.

Kwenye majanga ambayo chanzo chake kinaweza kuwa ni mwanadamu moja kwa moja, CCM haijawahi kumwacha nyuma mtanzania. Viongozi wa chama wamekuwa wakishirikiana na jamii kwa misaada, michango na mawazo.

CCM kinaamini watu wote ni sawa hivyo tofauti na vyama vingine CCM inajidhatiti kuweka usawa katika kila hali kwa kuhimiza kufanya kazi kwa bidii kwa sababu utu wa mtu ni kazi.

Miaka 45 ya CCM ni fumbo tunalotakiwa kuliishi na kulienzi. Kuenzi fikra na falsafa waasisi wetu juu ya usawa na kujali masuala ya wananchi. Ni miaka mingi CCM imekaa madarakani lakini kulingana na jukumu lililonalo kwa wananchi katika kujenga jamii yenye usawa na kujali masuala ya wananchi CCM ndio chama chenye kubeba imani hiyo ya Watanznania
 
Tunaweza kushangazwa na uhusika wa CCM kila janga linapotokea, pengine inaweza kufikiriwa kwamba kwa sababu ndio ina serikali hivyo haina budi kuonesha uhusika wake au wengine wanaweza kusema ni CCM imetengeneza tukio na ili ionekane ina wajali wananchi wake walitatue...
Hayo ni mawazo yako.Hayafanani na ya kwetu.Imani ya Watanzania haibebwi na chama chochote cha siasa.Zungumza mengine ya kuwasaidia Wtzd.
 
Back
Top Bottom