Masudi Kipanya bado yupo mitaa ya Ufipa

Masudi Kipanya bado yupo mitaa ya Ufipa

Joined
Nov 23, 2018
Posts
94
Reaction score
202
Baada ya katuni ya samaki tuliyoijadili jana, leo manzania mwenye kipaji cha hali ya juu ametuletea tafakuri nyingine. Karibuni tuchangie mawazo.

Nionavyo mimi, mtu ambaye amejifungia ndani, anasema Watanzania ni waoga! Nadhani hii inahusiana na maandamano yaliyokuwa yafanyike tarehe 23/9/2024. Kuna vijana walikuwa wanahamasisha maandamano kwa nguvu sana huku wakidai hawawaogopi polisi na wapo tayari kufa.

Mfano ni kijana mmoja kutoka Mbeya ambaye nadhani atakuwa na tatizo la Afya ya akili, licha ya kuhamasisha na kuahidi kuwa mstari wa mbele, hakutokea kabisa Dar es salaam.

Naamini Watanzania si waoga na si wajinga. Watu wa Ufipa waache blame game badala yake waukabili ukweli mchungu kwamba strategies zao zimeshindwa vibaya wakati wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuliko wakati mwingine wowote. Kama wakishindwa kukabiliana na ukweli huu, muda si mrefu watakuwa kama NCCR na CUF.

Wasalaam!

FB_IMG_1727329783684.jpg
 
Sasa hivi wameachana na ishu za maandamano wamedakia ile ya Lisu na Tigo.

Ndio hapa ccm inapojichukulia ushindi kwa asilimia 100 kwa 100
Maandamano lengo lilishatimia ambalo ni kuujulisha ulimwengu jinsi serikali ya CCM inavyoteka na kuua wapinzani .
 
Maandamano lengo lilishatimia ambalo ni kuujuliaha ulimwengu jinsi serikali ya CCM inavyoteka na kuua wapinzani .
Si kweli. Tuliambiwa katika themes za maandamano kuna eti SAMIA MUST GO, dhamira yenye lengo la kumshinikiza Rais aondoke madarakani kwa nguvu ya Umma. Kuna jambo Watu wa Ufipa wanapaswa kulitambua kuhusu rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, nalo ni kwamba si mtu wa kuyumba. Akiona na kuoneshwa destination sahihi, hakuna wimbi wala dhoruba itakayozuia chombo chake kutua palipokusudiwa. Wanachopaswa kufanya ni kutumia fursa vizuri ya "Reconciliation" wakiimarishe Chama Chao kwani sayansi inathibitisha kuwa Samia Suluhu Hassan bado yupo sana pale kwenye throne.
 
Ukiwa na upeo mdogo huwezi kuwaelewa chadema maana wanatumia akili nyingi kwenye harakati zao

Samia ni Rais kwa mujibu wa katiba ya nchi kwa akili Yako ndogo unahisi anaweza kuondoka kwa matamko?
 
Back
Top Bottom