Hapana kaka. Ni mtazamo tu wala sina niliowalenga bali ukifuatalia utatambua kuwa kuna ukweli. Niliowataja nimetolea mfano tu. Wapo wengi mno ambao hawapendi babazao kujulikana.Mr bean, mi ckubaliani na mada yako, mi naona we umeleta hii mada hapa kwa kuwalenga watu fulani tu kwa sababu unazozijua we mwenyewe,
Ivi we unajua bongo ina masupa staa wangapi?
Wadau hii imenishangaza kitambo sasa juu ya hawa masupasta wetu. Mara zote utasikia wanazungumzia wazazi wao wa kike tu na si wazazi wa kiume. Mfano utasikia Mama Lulu kasema hivi. Mara mama Kanumba vile.?Mara mamaRay anoekana kariokoo. Mara Mama kiba aja juu. Nk nk Sijawahi kusia Wazazi wa kiume wa hao mastaa wakiwataja watoto wao au hao mastaa wakiwataja babazao kama wanavyowataja mamazao.Kulikoni?.
..mkuu hapo umenena mkuu....kutajwa sio inshu inshu ni kutajwa kivipKIJANA MWENYE HEKIMA NI SIFA KWA BABA YAKE...lakini kijana mpumbavu ni mzgo kwa mama yake..! JIULIZE, Je hao mama zao wanatajwa kwa yenye HEKIMA, BUSARA au ya kijinga na kpumbav?..
Kimahesabu titasema mama anachukua asilimia 75 katika moyo wa mtoto na baba 25 tuu, very amazing truth!!Siku moja Mtume aliulizwa na Maswahaba zake. Ewe mjumbe wa Allah ni nani ana haki zaidi juu ya mwenzake(kufanyiwa ihsani)?Mtume akajibu MAMA yako,akaulizwa tena kisha nani?akajibu MAMA ako,akaulizwa tena kisha nani akajibu tena MAMA yako,akaulizwa tena kisha nani?akajibu BABA yako!
Kutokana na hadithi hiyo fupi utaona wazi ni kwa jinsi gani Mama ana cheo hata kwa Mungu,hivyo ni automatically kumpa Mama kipaumbele katika majambo mengi kuliko Baba,hii ni sheria ya kimaumbile...na ndo maana mara nyingi Mtu anapoondokewa na Mama ake mzazi(anapofariki)huwa na huzuni saaana kuliko anapoondokewa na Baba ake.Hii ni kutokana na Mahaba ya asili yaliyopandikizwa na Mungu kwa mtoto juu ya MAMA ake!
Yaani MAMA ni sawa na vipaumbele vya lowassa,namely:
1-ELIMU
2-ELIMU
3-ELIMU
Hii kali.... kwa hiyo sisi kazi yetu ni kuwika tuBaba mdogo aliwahi kuniambia "wanaume hatuna watoto, watoto ni wa mama angalia hata vifaranga wa kuku hukuti wakiambatana na jogoo."
BT, na mie wazo langu lilikuwa hilo hilo, pata picha ulimtelekeza mama wa watu, akahangaika na mtoto ghafla mtoto nyota imemuangukia, unaanzaje anzaje kurudisha mahaba?!Baadhi wababa waliingia mitini....hivyo inabidi waisome tu namba kimya kimya
Watake radhi wasanii!!! Nayo ni kazi kama zingine. Huko gesti hao wamama walikuwa wenyewe, it takes two.....km mtoto msanii unategemea mama atakuwaje? mimba yenyewe ilitungwa guest,