Maswala kuhusu process za polisi, msaada tafadhali.

noella

Senior Member
Joined
Mar 21, 2011
Posts
101
Reaction score
50
Nilireport mtu kunitishia maisha kituo kimoja cha polisi hapa dar,nikapewa RB.baada ya siku mbili nikapigiwa simu na polisi ambaye alijitambulisha kama mpelelezi wa kesi yangu, akaniambia niende anisikilize,kesho yake nikaenda. nikamsimulia kisa chote. sasa polisi kutaka hela eti amenifanyia counselling halafu akamuita na yule mshtakiwa nae akamtoa hela na akamfanya wawe marafiki wakaenda bar kunywa.
kesho yake yule polisi akaniita tena kunipa feedback ya alichokisikia kutoka kwa mshtakiwa.badala ya kunipa feedback sasa akaanza kunitongoza alivyoona sielekei akanambia kwa kuwa sitaki mshtakiwa aende mahakamani basi inabidi tufunge kesi na itanibidi nilipie dolar mia nne, nikashangaa sana.nikamwambia mimi sina hela.akasema hata laki mbili mana wako wengi pale mkuu wa kituo kufunga kesi anaona kama ni usumbufu na maelezo meengi.mi nikachoka sasa nimeamua simpokei simu yake tena.lakini anatuma msg kuuliza nitaenda lini kufunga kesi.

nahitaji kujua, je nikifungua jalada nikapewa RB je ni lazima kufunga kesi?kama ndio je inalipiwa kufunga hiyo kesi? what if nahitaji bado kuitumia hiyo RB just incase mshtakiwa akikurupuka kunitishia tena? nahitaji mwongozo wenu please.
 
Kwa kawaida unaporipoti kituo cha polisi na kutoa malalamiko kama hayo ya kwako au mengine yeyote ya jinai, unabaki kuwa mlalamikaji na polisi kwa kwa upande wao wanakuwa na jukumu la kufanya upelelezi na kuona kama malalamiko yako yana msingi wa kisheria au la? Lengo la kufanya upelelezi ni kukusanya ushahidi ili kumshitaki mtuhumiwa mahakamani, na kuthibitisha kuwa mshitakiwa ametenda kosa, na polisi wanatakiwa kuthibitisha pasipo kuacha mashaka.

Sheria imewapa polisi, kulingana na aina ya kosa, mamlaka ya kuchambua ushahidi na pengine kuamua kama kesi ifutwe au ipelekwe mahakamani, hivyo katika mazingira hayo si jukumu lako kusema kesi ifutwe au iendelee bali ni jukumu la polisi, japo katika kufanya hivyo, polisi/kurugenzi ya mashitaka wanatakiwa kuamua kwa nia ya kutenda haki au kwa maslahi ya taifa. Na jukumu lako ni kutoa ushirikiano wa taarifa zote muhimu kuhusiana na tukio ili kuwawezesha polisi kukusanya uhahidi wa kutosha ili waweze kuithibitishia mahakama na hatimaye kumtia hatiani mshitakiwa.

Kwa msingi wa maelezo hayo hapo juu, huyo polisi anayekudai pesa na ngono mchukulie kama muhalifu mwingine yeyote sawa na huyo alietishia kukuua. Anadai rushwa badala ya kufanya kazi yake ya kupeleleza na kushtaki. Dawa yake ni kumkamatisha kwa makachero wa TAKUKURU, lakini kuwa makini usije ingia kwenye mtego mwingine wa rushwa ya ngono maana siku hizi kila mahali kumeharibika.

Huhitaji kulipia chochote polisi maana sisi (raia) ndo waajiri wao na sisi ndo tunaowalipa mishahara, kwahiyo asikubabaishe na tamaa zake za pesa na ngono.
 
Nashukuru sana umenipa mwangaza.sasa nalisubiri lipolisi lipige tena atajuta.
 
Back
Top Bottom