Maswala ya fundi kunambia leta Gari tuone ndipo nikupe gharama inakwaza

Maswala ya fundi kunambia leta Gari tuone ndipo nikupe gharama inakwaza

Ghost MVP

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2022
Posts
439
Reaction score
736
Biashara za Mtandaoni bhana zina Changamoto sana, tunajitahidi mno kuendana na Wakati lakini wafanya biashara wengi hawajui kwanini wanafanya biashara na ipi ni namna nzuri ya kufanya biashara na kuvuta wateja.

Unakuta unashida ya Kubadilisha taa ya Nyuma, au unataka Plug za Ignition, unamuuliza Bei anakwambia Leta Gari tuone ndo nikupe bei, ili iweje? Inamaana hawajui bei za Bidhaa zao? Mpaka watafuta namna ya kukadiria

Mwingine anaweka Bidhaa haina Bei, anataka Uulize kwa kumpigia simu au WhatsApp, bila kujua inacost muda mwingi na mfanya biashara mwenzio kaweka bei akimuona hawez kumbuka kukutafuta tena.

Hii Tabia inakwaza Mnooooo..
 
Sasa unataka akwambie gharama ya milioni 15 bila kujua tatizo? Ukimuuliza hizo milioni zote ni makusudio yepi, atajibuje?

Tumia japo thumni ya akili yako basi!

Kuhusu kuweka bei, huo ni uamuzi wa mfanyabiashara mwenyewe. Hujawahi kusikia kwamba biashara ni maelewano?

Kwako anaweza akasema bidhaa fulani ni 100k, kwa mwingine bidhaa hiyohiyo ikawa 150k. Akiweka bei moja anakuwa amejichocha mwenyewe.
 
Mkuu kwenye nchi za Africa kila kitu kimewekwa ni fursa ya upigaji na ndio maana mengi yanayo husishwa pesa hua yana fichwa fichwa ili ujae upigwe.

Sio kwa fundi magari tu au wauza spare bali kila kitu

Bongo Nyoso.
 
Biashara za Mtandaoni bhana zina Changamoto sana, tunajitahidi mno kuendana na Wakati lakini wafanya biashara wengi hawajui kwanini wanafanya biashara na ipi ni namna nzuri ya kufanya biashara na kuvuta wateja.

Unakuta unashida ya Kubadilisha taa ya Nyuma, au unataka Plug za Ignition, unamuuliza Bei anakwambia Leta Gari tuone ndo nikupe bei, ili iweje? Inamaana hawajui bei za Bidhaa zao? Mpaka watafuta namna ya kukadiria

Mwingine anaweka Bidhaa haina Bei, anataka Uulize kwa kumpigia simu au WhatsApp, bila kujua inacost muda mwingi na mfanya biashara mwenzio kaweka bei akimuona hawez kumbuka kukutafuta tena.

Hii Tabia inakwaza Mnooooo..
Wakati mwingine tatizo unaliona wewe limekuwa triggred na kitu kingine, ndio maana wakati mwingine unafikiri kuwa unaona tatizo la bearing kumbe sio hilo pekee kuna shockup, kuna liner, un-balanced tire, pengine hata hub.
Kwa hiyo ukiliona gari unaweza kujua tatizo halisi na sio hilo analosema mwenye gari.
 
yupo sahihi leta gari tuone kwanza apate uhakika wa kazi sasa akuambie bei gari umelificha ili unde sehemu ingine?
 
Back
Top Bottom