Maswali 3 ya kujiuliza kama wazo lako la biashara linafaa

Maswali 3 ya kujiuliza kama wazo lako la biashara linafaa

Tycoon_Master

Member
Joined
Oct 18, 2017
Posts
6
Reaction score
12
Wakati business plan nyingi huandikwa kuzishawishi benki au wawekezaji ili kukopesha pesa, business plan nyingine nyingi huandaliwa ili kuangalia kama business idea iliyopendekezwa inaweza kuwa halisia au hapana.

Kama hiyo ndio sababu ya wewe kutaka kuandika business plan basi mbinu za haraka zifuatazo zitakusaidia kama ndio unaanza biashara au unafikiria kununua biashara ambayo tayari ipo.
Jibu haya maswali matatu kwa upeo wako na utatambua kama hilo wazo lako la biashara linafaa kutekelezeka.

1. Je, kuna soko lake?
Watu wengi wanataka kuanza biashara kwa kuuza bidhaa au kutoa huduma kwa sababu wangependa kufanya hivyo. Lakini kanuni ya kwanza ya kuanza biashara ni kwamba inabidi watu wengine wawe na uhitaj wa kununua hiyo bidhaa au huduma husika. Vinginevyo utakua unajaribu kuuza makoti kwenye msimu wa kiangazi – hakuna haja ya kuendelea na huu mpango wa biashara kama hii.

2. Faida stahiki ya biashara hii ni ipi?
Kwa maneno mengine, kuna pesa yoyote itakayopatikana kwenye hii biashara au angalau pesa ya kujitosheleza kuifanya ifae? Unaweza kuwa na malengo mazuri ya kuuza nguo za kiasili lakini, kama hakuna mtu yoyote wa kuzinunua, hapatakua na faida.

Kwa maana nyingine, kama utakua unachukua muda mrefu kuzalisha bidhaa moja kwa mwezi, hautaona faida ya kutosha hata ya kukufanya biashara hii kuwa part time business yako.
Mipango yako ya biashara juu ya wazo hili la biashara itaishia hapa.

3. Ni changamoto zipi zipo kwenye hii biashara na je, zinakabilika?
Inawezekana una wazo zuri la kibiashara ambalo linafaa. Tayari umeshajua soko lake na umeshajua utatengeneza pesa nyingi kupitia hiyo biashara lakini kuna vizuizi na matatizo ambayo yatakutatiza kuifanya biashara husika.

Kwa mfano inawezekana unataka kuanzisha biashara utakayokua unaifanyia kwenye makazi yako unapoishi lakini ukagundua taratibu na sheria haziruhusu ufanyaji wa aina hiyo ya biashara majumbani.

Chukua muda ufanye utafiti juu ya sheria na kanuni zote za manispaa, halmashauri, majimbo na za nchi ambazo zinaweza kuiathiri business plan yako. Kuna baadhi ya sehemu unaweza kuepukana na vikwazo kama unajuana na watu husika. Lakini unaweza ushindwe kufanya kile unachotaka kwa mahala ulipo. Ukifikia hatua hii huna budi kuiacha business plan yako mpaka pale utakapoona ni mazingira sahihi kuifanya au tafuta sehemu nyingine ya kuifanyia biashara yako.
 
Back
Top Bottom