Maswali juu ya kesi ya uhujumu uchumi CWT Maswa: Takukuru yakaa kimya miezi mitano baada ya mahojiano

Maswali juu ya kesi ya uhujumu uchumi CWT Maswa: Takukuru yakaa kimya miezi mitano baada ya mahojiano

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155

Maswa, Simiyu – Zikiwa zimepita takriban miezi mitano tangu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Maswa kuwahoji viongozi wa zamani na wa sasa wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilaya hiyo kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za chama, hakuna hatua yoyote ya kisheria iliyochukuliwa hadi sasa, hali inayozua maswali miongoni mwa wanachama na umma kwa ujumla.​

Viongozi waliotajwa katika uchunguzi huo ni:
  • Floring Rwela, aliyekuwa Katibu wa CWT Maswa, sasa Katibu wa CWT wilaya ya Kwimba, Mwanza;
  • Nazama Tarimo, aliyekuwa Katibu wa CWT Maswa, sasa Katibu wa CWT wilaya ya Rombo, Kilimanjaro;
  • Chesta Maiga, Mweka Hazina wa CWT Maswa.
Tuhuma dhidi yao ni pamoja na:
  • Matumizi mabaya ya fedha za chama, kinyume na taratibu za fedha;
  • Ununuzi wa gari aina ya Coaster kwa zaidi ya Sh milioni 81, kiasi kinachodaiwa kuzidi thamani halisi ya gari hilo;
  • Mchakato wa manunuzi usio wazi wala kufuata taratibu.
Kesi hii, inayojulikana kwa namba Na. 50148/2025, ilianza kuchunguzwa rasmi tarehe 28 Februari 2025 baada ya TAKUKURU kuwaita viongozi hao kwa mahojiano. Tangu kipindi hicho, hakuna taarifa rasmi kutoka TAKUKURU wala hatua zozote za kuwafikisha watuhumiwa mahakamani zimechukuliwa, licha ya uzito wa tuhuma hizo zinazohusiana na uhujumu uchumi.
Wachambuzi wa masuala ya utawala bora wanahoji:
  • Je, TAKUKURU Maswa inasubiri nini kuwafikisha watuhumiwa hao mahakamani?
  • Je, kuna ushawishi au mkono wa kisiasa nyuma ya kusuasua kwa shauri hili?
  • Wanachama wa CWT Maswa watajua lini ukweli kuhusu fedha zao?
Mwandishi wetu alijaribu kufuatilia kwa uongozi wa TAKUKURU wilaya ya Maswa lakini hakupata majibu ya moja kwa moja kuhusu hatua inayofuata kwenye shauri hili.
 
Back
Top Bottom