Fikra Pevu
Senior Member
- Oct 13, 2010
- 128
- 20
Naomba kuwasilisha kero yangu hii kwa viongozi wa sekta ya elimu Tanzania. Kwa miaka kadhaa kumekuwa na tabia ya watungaji wa mitihani ya Kidato cha Nne hasa kwa masomo ya sanaa, kutumia lugha ngumu ya kiingereza katika maswali yao, hali inayopelekea wanafunzi wengi kufeli masomo hayo kwa sababu ya kujibu tofauti na swali lilivyouliza. Mfano, swali linataka mwanafunzi ajibu sababu zilizopelekea kitu fulani, mwanafunzi anajibu athari za kitu hicho na hivyo kukosa swali zima.
Ushauri wangu;
Kwa kuwa somo la kiingereza lipo, upimaji wa ujuzi wa mwanafunzi katika lugha hiyo ufanyike katika somo hilo. Kwa masomo mengine, maswali yaulizwe katika lugha nyepesi itakayoeleweka kwa wanafunzi wote. Mfano, kama swali linataka kupima ufahamu wa mwanafunzi kuhusu sababu ya kutokea kwa jambo, neno “causes” litumike badala ya kutumia maneno magumu ya kiingereza.
Kero hii imekatisha ndoto za Watanzania wengi sana hapa nchini, tuungane kusema, Inatosha.