Maswali magumu kwa atheist

Jackwillpower

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2017
Posts
2,467
Reaction score
3,687
Mungu alimuuliza Ayubu maswali ambayo yalilengwa kwa wanaosema Mungu hayupo. Kama Kuna Atheist anaweza kujibu ajitokeze.

Ayubu 38

1 Ndipo Bwana akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema;

2 Ni nani huyu atiaye ushauri giza kwa maneno yasiyo na maarifa?

3 Basi jifunge viuno kama mwanamume, maana nitakuuliza neno, nawe niambie.

4 Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama una ufahamu.

5 Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake – hakika unajua! Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?

6 Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,

7 Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?

8 Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, hapo ilipotoka kwa nguvu kama kwamba imetoka tumboni mwa nchi.

9Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake, na giza zito kuwa nguo ya kuifungia,

10 Nikaiagiza amri yangu; nikaiwekea makomeo na milango.

11 Nikasema, utafika mpaka hapa, lakini hutapita, na hapa mawimbi yako yenye nguvu yatazuiliwa?

12 Je, umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza? umeyajulisha mapambazuko mahali pake?

13 Yapate kuishika miisho ya nchi, waovu wakung'utwe wakawe mbali nayo?

14 Hubadilika mfano wa udongo chini ya mhuri, vitu vyote vinatokea kama mavazi.

15 Na waovu nuru yao huzuiliwa isiwafikie, na mkono ulioinuka huvunjika.

16 Je, umeziingia chemchemi za bahari, au umetembea mahali pa siri pa vilindi?

17 Je, umefunuliwa malango ya mauti, au umeyaona malango ya kuzimu?

18 Umeyafahamu mapana ya dunia? Haya sema, ikiwa unayajua hayo yote.

19 Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru? Na giza pia, mahali pake ni wapi?

20 Upate kuipeleka hata mpaka wake, upate kuyaelewa mapito ya kuiendea nyumba yake?

21 Hukosi unajua, maana ulizaliwa wakati huo, na hesabu ya siku zako ni kubwa!

22 Je, umeziingia ghala za theluji, au umeziona ghala za mvua ya mawe.

23 Nilizoziweka akiba kwa wakati wa misiba, kwa siku ya mapigano na vita?

24 Je, nuru hutengwa kwa njia gani, au upepo wa mashariki hutawanywaje juu ya nchi?

25 Ni nani aliyepasua mfereji kwa maji ya gharika, au njia kwa umeme wa radi;

26 Kunyesha mvua juu ya nchi isiyo na watu; juu ya jangwa asiyokaa mwanadamu.

27 Kuishibisha nchi iliyo kame na ukiwa, na kuyameza majani yaliyo mororo?

28 Je, mvua ina baba au ni nani aliyeyazaa matone ya umande?

29 Barafu ilitoka katika tumbo la nani na sakitu ya mbinguni ni nani aliyeizaa?

30 Maji hugandamana kama jiwe, na uso wa vilindi huganda kwa baridi.

31 Je, waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia, au kuvilegeza vifungo vya Orioni?

32 Je, waweza kuziongoza Sayari kwa wakati wake au waweza kuongoza Dubu na watoto wake?

33 Je, unazijua amri zilizoamriwa mbingu? Uaweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia?

34 Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni, ili wingi wa maji ukufunikize?

35 Waweza kuutuma umeme, nao ukaenda, ukakuambia, Sisi tupo hapa?

36 Je, ni nani aliyetia hekima moyoni? Au ni nani aliyetia ufahamu rohoni?

37 Ni nani awezaye kuyahesabu mawingu kwa hekima? Au ni nani awezaye kuzimimina chupa za mbinguni?

38 Wakati mavumbi yagandamanapo, na madongoa kushikamana pamoja?

39Je, ntamwindia simba mke mawindo? Au utashibisha njaa ya simba wachanga,

40 Waoteapo mapangoni mwao, wakaapo mafichoni wapate kuvizia?

41 Ni nani anayempatia kunguru chakula, Makinda yake wanapomlilia Mungu, na kutangatanga kwa kutindikiwa na chakula?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu ambaye anataka wanadamu wote tuseme na tukiri yeye yupo,
Alishindwaje kuumba binadamu wenye Kujua yeye Yupo????

Mungu muweza wa vyote alishindwaje kuumba binadamu wasio jiuliza uwepo wake??

Kama Mungu anaweza yote ange ondoa ufahamu Akilini mwa wanadamu kusema "Yeye hayupo" na angeweka ufahamu wa sisi kukiri tu "yeye yupo"..

Hivyo mpaka kufikia binadamu wanahoji uwepo wa Mungu ina dhihirisha tosha kwamba huyo Mungu Hayupo....
 
Ulitaka Mungu aumbe maroboti?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulitaka Mungu aumbe maroboti?



Sent using Jamii Forums mobile app
Ange weza kuumba maroboti kama anataka amri zake na sheria zake zifuatwe bila kuvunjwa hata moja.

Badala yake ana umba viumbe visivyo tii maagizo na sheria zake Halafu analalamika hivyo viumbe ni viovu,vikaidi na visivyo fuata sheria,amri na maagizo yake...

Huyo Mungu muweza wa vyote alishindwaje kuumba binadamu wenye kuweza kutii maagizo yake tu??

Hivyo kama aliumba viumbe(Binadamu) visivyo tii amri zake kwa mapenzi yake mwenyewe hapaswi kuviadhibu kwa kutotii sheria zake, Badala yake angeumba viumbe anavyotaka vimtii wakati wote..

Hivyo huyo Mungu muweza wa vyote Hayupo na ameshindwa kuumba binadamu wenye kufuata akisemacho yeye.

Ange kuwepo, Tusinge kuwa tunabishana hapa ange kwisha tuzuia automatically.Hivyo Hayupo.
 
Mpumbavu ni Mpumbavu tu na haitatokea akajitambua ni Mpumbavu kwa mihongo, karne, milenia hata miaka asiyohesabika kwake maana upumbavu ni kipaji chake.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Mpumbavu ni Mpumbavu tu na haitatokea akajitambua ni Mpumbavu kwa mihongo, karne, milenia hata miaka asiyohesabika kwake maana upumbavu ni kipaji chake.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Huwezi kujibu hoja ngumu na nzito kama hizi kwa vile una "Fear of Unknown" na Hofu za kidini..

Kakojoe ulale.
 
Kazi kwelikweli huu mtanange ni mzito Cc Kiranga

Ila ndugu zanguni wapinga uwepo wa Mungu hv ni nani aliye umba huu ulimwengu na vilivyomo?
 
Kazi kwelikweli huu mtanange ni mzito Cc Kiranga

Ila ndugu zanguni wapinga uwepo wa Mungu hv ni nani aliye umba huu ulimwengu na vilivyomo?
Kwanza, Kwa nini Unadhani kuna aliye umba huu ulimwengu?

Kwa nini Hudhani ulimwengu unaweza kuwepo bila ku umbwa?

Yani ni kitu gani kina kufanya useme ulimwengu uliumbwa na sio ulimwengu, Hauku umbwa????
 
Kwanza kabisa, unaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo na kutatua Epicurean Paradox?

 
Jibu hayo maswali ili tujue hayupo

Sent using Jamii Forums mobile app
Logical non sequitur, hayo maswali yanaweza kuulizwa na watu hata kama Mungu hayupo.

Pia, kutoweza kujibu hayo maswali si uthibitisho Mungu yupo, to the contrary, kutoweza kujibu maswali hayo kunaweza kuwa ushahidi kwamba Mungu wako hayupo.

Tatua Epicurean Paradox tujue yupo.

Kama hata umeielewa.
 
Mimi kwa uelewa wangu najua akili zetu za binaadam ni ndogo sana kujua ukuu na sababu za Mungu kufanya haya yote tunayoyaona hivyo huko mbinguni ndio tutajua. Ni sawa na kuchukua maji ya bahari uhamishie kwenye kishimo kidogo
 
Kwanza, Kwa nini Unadhani kuna aliye umba huu ulimwengu?

Kwa nini Hudhani ulimwengu unaweza kuwepo bila ku umbwa?

Yani ni kitu gani kina kufanya useme ulimwengu uliumbwa na sio ulimwengu, Hauku umbwa????
Labda ww unafikiri kwanini ulimwengu upo hivi?

Unafahamu kila kilichopo na umbo kinachanzo chake?

Kwanini kweny ulimwengu unapinga chanzo chake.
 
Mimi kwa uelewa wangu najua akili zetu za binaadam ni ndogo sana kujua ukuu na sababu za Mungu kufanya haya yote tunayoyaona hivyo huko mbinguni ndio tutajua. Ni sawa na kuchukua maji ya bahari uhamishie kwenye kishimo kidogo
Agnostic
 
Kwanza kabisa kabla ya kuangalia mtanange, kwa nini swali lako linauliza "nani"?

Huoni kwamba hata swali lenyewe lina kasumba ya kulenga kwenye jibu unalolitaka?
Vizuri kwa kunikosoa swali langu

Labda nikuulize upya kwanini ulimwengu upo hivi? Je ni kipi chanzo cha ulimwengu huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…