Uchaguzi 2020 Maswali magumu kwa Tume ya Uchaguzi, NEC

Uchaguzi 2020 Maswali magumu kwa Tume ya Uchaguzi, NEC

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Wagombea wote (100%) walioenguliwa kwenye uchaguzi ni wa kutoka vyama vya upinzani tu. Maswali ya wananchi kwa tume yao ya uchaguzi ni:

1. Wagombea wote bila kujali vyama vyao ni watu wanaofahimika na kufahamiana, Je, tume ya uchaguzi kuna elimu/taarifa fulani muhimu ya uchaguzi ambayo haikuwapa wagombea wa vyama vya upinzani hadi wakosee kwa kiwango cha kuenguliwa?

2. CCM hakuna kabisa mgombea aliyeenguliwa, je, jambo kama hilo linatokeaje. Je, tume ya uchaguzi ni HURU kwelikweli?

3. Je, vyama vya upinzani vimeteua wagombea wasiokuwa na uelewa wa uchaguzi?
4. CCM imeteua wagombea wote wanaokubalika na Tume kwa kutumia njia gani?
5. Ni elimu ipi ya uchaguzi ambayo wapinzani hawakuwa nayo wakati wa uteuzi wa wagombea na ujazaji wa fomu za kugombea?

Katika hali ya kawaida ilitakiwa kuwe na mtawanyiko sawa (normal distribution curve) kwa wagombea walioenguliwa kwakuwa wagombea wote (sample) wana share common factors za kuwa wote ni watanzania, wamesoma shule na vyuo vilevile, wanaishi mitaa ileile, wanakula vyakula vilevile, nk, Ila tofauti yao kubwa ni vyama vya siasa tu wanavyovitumikia.

Bila shaka factor kubwa (confounding) ya tofauti hii tunayoiona (skewed) huenda inatokana na eneo la utendaji wa Tume ya Uchaguzi tu basi.

Kwavyovyote vile hii haiwezi kutokea kwa bahati mbaya tu (chance). Kama kuna mdau yeyote anaetaka kulitatua tatizo kupita bila kupingwa kwenye chaguzi lazima anzie kwenye Tume kurudi nyuma. Yaani Factors influencing utendaji wa Tume.
 
Tume haijui wajibu wake ni nini? Kazi ya msimamizi wa uchaguzi ni kuwaongoza wagombea ili waweze kuteuliwa kuwa wagombea, cha ajabu wasimamizi wanashindwa kuwasimamia wagombea wajaze fomu kwa usahihi.
 
Tume haijui wajibu wake ni nini? Kazi ya msimamizi wa uchaguzi ni kuwaongoza wagombea ili waweze kuteuliwa kuwa wagombea, cha ajabu wasimamizi wanashindwa kuwasimamia wagombea wajaze fomu kwa usahihi,
kuna mazingira kuwa kazi hiyo wameifanya kwa upande mmoja tu kwa bahati mbaya au kwa makusudi.
 
Tume haijui wajibu wake ni nini? Kazi ya msimamizi wa uchaguzi ni kuwaongoza wagombea ili waweze kuteuliwa kuwa wagombea, cha ajabu wasimamizi wanashindwa kuwasimamia wagombea wajaze fomu kwa usahihi,

Kuna mazingira kuwa kazi hiyo wameifanya kwa upande mmoja tu kwa bahati mbaya au kwa makusudi.
 
Maanake rufaa 55 zilipita ni 15 baki 40 + 18 = 58 majimbo yote hayo wamepewa bure CCM na tume ya uchaguzi, hii ni tume CCM wala siyo tume ya uchaguzi
 
Back
Top Bottom