Maswali muhimu unayotakiwa kumuuliza Single mother kabla hujafanya maamuzi magumu

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
MASWALI MUHIMU UNAYOTAKIWA KUMUULIZA SINGLE MOTHER KABLA HUJAFANYA MAAMUZI MAGUMU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Post hii usije ichukua kama nimekuambia Kaoe single mother. Nope! Mimi kama Kakaako, Babaako, tayari nilishakueleza kijana chini ya miaka 45 hutakiwi kuoa single mother kwa namna yoyote ile.
Hata angekuwa mzuri kama malaika.
Hata angekuwa na sifa ipi.
Hata angekuwa ametoa Figo kwaajili yako.

Post hii ni kwaajili ya wale wenye miaka juu ya miaka 45.

Najua binti zangu, dada zangu, mama zangu hawapendi ninapozungumzia jambo hili. Lakini nafanya hivi kwaajili ya vijana wasio na hatia ambao nao wanastahili kufurahia.

Maswali muhimu ambayo utatakiwa kumuuliza Single mother kabla hujafanya maamuzi magumu;

a) Uhusiano wako na Baba mtoto wako ukoje kwa sasa?
Swali hili unalenga kujua mawasiliano, mipaka na kama mapenzi yao bado yapo au hayapo.
Ikitokea amejibu hawasiliani naye kabisa. Huyo hafai kabisa.

Haiwezekani mwanamke wa maana, wife material, anayejitambua, aishi na mtoto wa mwanaume alafu asiwasiliane na huyo mwanaume hata kisa mtoto. Huyo hafai. Ni aidha anakudanganya. Na kama hakudanganyi basi anaroho mbaya.

Akisema wanawasiliana, basi fuatilia wanawasiliana mara ngapi na kuhusu nini. Uliza hilo.

b) Ni ipi nafasi yangu katika Maisha ya Mtoto wako?
Swali hili ni suala la mtego, linaloibua nia yake ya ndani bila ya yeye mwenyewe kujijua.
Hapa Unataka kujua kama anakuona kama:
mume, baba wa kambo, mtoaji wa fedha(sponsa tuu), au mtu wa kumsaidia na kusogeza siku ziende.
Kisha muulize, Mtoto akikosea, utakuwa na nafasi gani ya kumrekebisha?

Swali hili ni mtego ambao wanawake wengi wasio na sifa hawachomoki. Wanafeli.
Kwanza, wataonyesha uhalisia kwamba hutakuwa na nguvu yoyote na mamlaka asilimia moja.

c) Umejifunza nini kutoka kwenye uhusiano uliopita?
Huu ni kama mjeledi. Ni swali la kisaikolojia na hapohapo la kiintelejensia.
Wanaume wengi wanakosea kuuliza, kwa nini uliachana na Baba mtoto wako au ex wako? Hili swali lipo moja kwa moja sana. Usimuulize swali mtu kwa namna hiyo.

Unapouliza alichojifunza, hapo atataja makosa na tabia zake na sio za ex wake.
Mtu hujifunza anapofanya makosa au kwenye jambo asilolijua.

d) Ikitokea Mimi na Mtoto wako tukagombana, utatatua vipi hilo?
Swali hili linatoa picha mamlaka na mipaka itakavyokuwa ndani ya nyumba.
Jibu la swali hili, kwa mwanamke wife material lazima atajibu kwa kuzingatia HAKI. Ajibu hatajuwa upande wa mume au wa mtoto. Ila atakuwa upande wa Haki.

e) Nani atagharamia Mahitaji ya mtoto?
Swali hili usione aibu kuliuliza.
Ni swali muhimu na litatoa picha ya ubinafsi wa mwanamke huyo.
Akijibu kwamba ukipenda ua penda na ua lake. Piga chini usifikiri mara mbili.

Akisema, wewe ni mwanaume lazima umhudumie mtoto hata kama sio wako. Piga chini.

Akijibu jukumu la huduma litabaki juu ya baba mzazi na yeye. Na wewe utatoa kwa hiyari yako ukitaka. Unaweza kumfikiria.

f) Ni mambo gani huwezi kuvumilia kwenye ndoa, na ni mambo gani uko tayari kuyarekebisha?
Swali hili ni muhimu, kisaikolojia linatoa picha tabia ya huyo mwanamke kwenye mambo ya migogoro yupoje.

Swali la chini yake, linahusu ni mambo gani anatamani kuyarekebisha? Swali hilo linalenga kujua tabia mzigo kwake. Lakini pia ni ishara ya kuonyesha anajitambua au hajitambui.

g) Kama tukioana, unataka maisha yetu ya familia yaweje baada ya miaka mitano?
Swali hili ni muhimu kwa sababu linatoa picha maono, ndoto, mipango yako na yake je vinaendana?
Anataka:
watoto wangapi?
kuishi wapi?
kufanya kazi gani?
kufanya biashara?
Kujenga nyumba?
malezi ya watoto yaweje?
uhusiano gani na ndugu?
mipaka gani kati ya familia yenu na watu wa nje?
Na mambo mengine kama hayo.

Nimechoka kuandika.

Nawatakia Sabato Njema.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Miruzi ni mingi hadi "masingo madha" wanachanganyikiwa.
Kwanini hawa viumbe hatuwaachi huru?
Unasema akisema hana mawasiliano na mzazi mwenzake piga chini,wakati huo huo mnasema singo madha asiolewe hadi aonyeshe kaburi la mzazi mwenzake... Tushike lipi sasa!
Tulio oa singo madha tushikamane,kwa umoja wetu tuendelee kuwajali na kuwalea watoto wao hadi baba walio terekeza hao watoto wajisikie aibu.
Nimechoka mimi
 
Hii ni Single mothers vs Broke Guys,
Single Mothers 5 vs Broke Guys hawajapata kitu,
The way wanavyorun kwenye vichwa vyenu ni wazi wana wakamua sana hadi mnatoka jasho,

🥂to all the Single mothers out there, you guys are strong endeleeni kutunyooshea hawa broke guys hadi watafute hela ndefu
 
Sasa ataonyesha kaburi la nani wakati mzazi mwenzie yupo hai
 
Hii ni Single mothers vs Broke Guys,
Single Mothers 5 vs Broke Guys hawajapata kitu,
The way wanavyorun kwenye vichwa vyenu ni wazi wana wakamua sana hadi mnatoka jasho,

🥂to all the Single mothers out there, you guys are strong endeleeni kutunyooshea hawa broke guys hadi watafute hela ndefu

Unatukana na kuwachamba waliochukua single mother kwa kuwaita broke guys?
 
Dodoso lote hilo la nini mkuu wakati vibint vibichi viko bwerere hata uwe na miaka 50 unajipatia sasa ya nini kuhangaika na mke wa mtu.kikao cha mwisho tulishakubaliana mpaka uone kaburi la baba mtoto cheti cha kifo toka mamlaka za serikali na picha mjongeo au video fupi siku ya mazishi jina la msalaba lifanane na kwenye vyeti au haukuweoo kwenye kikao mkuu
 
MASWALI MUHIMU UNAYOTAKIWA KUMUULIZA SINGLE MOTHER KABLA HUJAFANYA MAAMUZI MAGUMU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Post hii usije ichukua kama nimekuambia Kaoe single mother. Nope! Mimi kama Kakaako, Babaako, tayari nilishakueleza kijana chini ya miaka 45 hutakiwi kuoa single mother kwa namna yoyote ile.
Hata angekuwa mzuri kama malaika.
Hata angekuwa na sifa ipi.
Hata angekuwa ametoa Figo kwaajili yako.

Post hii ni kwaajili ya wale wenye miaka juu ya miaka 45.

Najua binti zangu, dada zangu, mama zangu hawapendi ninapozungumzia jambo hili. Lakini nafanya hivi kwaajili ya vijana wasio na hatia ambao nao wanastahili kufurahia.

Maswali muhimu ambayo utatakiwa kumuuliza Single mother kabla hujafanya maamuzi magumu;

a) Uhusiano wako na Baba mtoto wako ukoje kwa sasa?
Swali hili unalenga kujua mawasiliano, mipaka na kama mapenzi yao bado yapo au hayapo.
Ikitokea amejibu hawasiliani naye kabisa. Huyo hafai kabisa.

Haiwezekani mwanamke wa maana, wife material, anayejitambua, aishi na mtoto wa mwanaume alafu asiwasiliane na huyo mwanaume hata kisa mtoto. Huyo hafai. Ni aidha anakudanganya. Na kama hakudanganyi basi anaroho mbaya.

Akisema wanawasiliana, basi fuatilia wanawasiliana mara ngapi na kuhusu nini. Uliza hilo.

b) Ni ipi nafasi yangu katika Maisha ya Mtoto wako?
Swali hili ni suala la mtego, linaloibua nia yake ya ndani bila ya yeye mwenyewe kujijua.
Hapa Unataka kujua kama anakuona kama:
mume, baba wa kambo, mtoaji wa fedha(sponsa tuu), au mtu wa kumsaidia na kusogeza siku ziende.
Kisha muulize, Mtoto akikosea, utakuwa na nafasi gani ya kumrekebisha?

Swali hili ni mtego ambao wanawake wengi wasio na sifa hawachomoki. Wanafeli.
Kwanza, wataonyesha uhalisia kwamba hutakuwa na nguvu yoyote na mamlaka asilimia moja.

c) Umejifunza nini kutoka kwenye uhusiano uliopita?
Huu ni kama mjeledi. Ni swali la kisaikolojia na hapohapo la kiintelejensia.
Wanaume wengi wanakosea kuuliza, kwa nini uliachana na Baba mtoto wako au ex wako? Hili swali lipo moja kwa moja sana. Usimuulize swali mtu kwa namna hiyo.

Unapouliza alichojifunza, hapo atataja makosa na tabia zake na sio za ex wake.
Mtu hujifunza anapofanya makosa au kwenye jambo asilolijua.

d) Ikitokea Mimi na Mtoto wako tukagombana, utatatua vipi hilo?
Swali hili linatoa picha mamlaka na mipaka itakavyokuwa ndani ya nyumba.
Jibu la swali hili, kwa mwanamke wife material lazima atajibu kwa kuzingatia HAKI. Ajibu hatajuwa upande wa mume au wa mtoto. Ila atakuwa upande wa Haki.

e) Nani atagharamia Mahitaji ya mtoto?
Swali hili usione aibu kuliuliza.
Ni swali muhimu na litatoa picha ya ubinafsi wa mwanamke huyo.
Akijibu kwamba ukipenda ua penda na ua lake. Piga chini usifikiri mara mbili.

Akisema, wewe ni mwanaume lazima umhudumie mtoto hata kama sio wako. Piga chini.

Akijibu jukumu la huduma litabaki juu ya baba mzazi na yeye. Na wewe utatoa kwa hiyari yako ukitaka. Unaweza kumfikiria.

f) Ni mambo gani huwezi kuvumilia kwenye ndoa, na ni mambo gani uko tayari kuyarekebisha?
Swali hili ni muhimu, kisaikolojia linatoa picha tabia ya huyo mwanamke kwenye mambo ya migogoro yupoje.

Swali la chini yake, linahusu ni mambo gani anatamani kuyarekebisha? Swali hilo linalenga kujua tabia mzigo kwake. Lakini pia ni ishara ya kuonyesha anajitambua au hajitambui.

g) Kama tukioana, unataka maisha yetu ya familia yaweje baada ya miaka mitano?
Swali hili ni muhimu kwa sababu linatoa picha maono, ndoto, mipango yako na yake je vinaendana?
Anataka:
watoto wangapi?
kuishi wapi?
kufanya kazi gani?
kufanya biashara?
Kujenga nyumba?
malezi ya watoto yaweje?
uhusiano gani na ndugu?
mipaka gani kati ya familia yenu na watu wa nje?
Na mambo mengine kama hayo.

Nimechoka kuandika.

Nawatakia Sabato Njema.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Hoja zako zina maswali muhimu sana, hasa kuhusu mipaka na baba wa mtoto, nafasi ya mwenza mpya katika malezi, fedha, migogoro na mipango ya baadaye. Hayo ni mambo ambayo mtu yeyote anayefikiria ndoa anatakiwa kuyauliza na kuyajadili kwa uwazi.

Lakini sehemu ya kusema kijana chini ya miaka 45 “hatakiwi kuoa single mother kwa namna yoyote ile” hapo ndipo ninapotofautiana na wewe.

Ndoa haipaswi kuamuliwa kwa status ya mtu pekee, bali kwa tabia, utu, ukomavu, historia, mawasiliano, mipaka na uwezo wa watu wawili kujenga familia yenye afya. Kuna single mothers wenye maadili na uwajibikaji mkubwa, na kuna wanawake ambao hawajawahi kupata mtoto lakini bado wanaweza kuwa changamoto kubwa kwenye ndoa. Vivyo hivyo kwa wanaume.

Kwa hiyo maswali haya ni mazuri, lakini ningeyaweka kama maswali ya kumuuliza mtu unayetaka kumuoa, si single mother pekee.

Jambo kubwa zaidi ni kuangalia kama huyo mwanamke amefunga ukurasa wa uhusiano uliopita, ana mipaka sahihi na baba wa mtoto, anaelewa nafasi yako, na nyote mnakubaliana kuhusu malezi, fedha na mamlaka ndani ya familia.

Kwa kifupi: usiogope single mother; ogopa kuingia kwenye ndoa bila kuelewa mfumo wa familia unaouingia. Hapo ndipo wanaume wengi hukosea.
 
Back
Top Bottom