Maswali na Majibu kuhusu gari aina ya Toyota Voltz

Maswali na Majibu kuhusu gari aina ya Toyota Voltz

Habari wadau, napenda kujuzwa na wazoefu wa hii gari (Voltz), kwenye rafu roads, mafuta na uimara.

Asante

1955693_Screenshot_2019-01-02-15-25-47-698_com.facebook.katana.jpg
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu toyota volz ni gari nzuri sana na imara pia ila uimara wake haufiki kwa Rav 4 old.
Utumiaji wake wa mafuta uko poa kwani ina cc1790 ambayo kawaida inakula 1lt/8-11km kutegemea na mwendo wa dereva.
Kwa upande Confitability iko poa sana ndani ina muundo kama Harrier.

Spear zilikuwa adimu kidogo ila kwa sasa naona zimeongezeka so usijali kuhusu hilo.

Nb:Kama barabara unayopita haina shida kipindi cha masika chukua yenye 2 wheel bt kama ni njia zetu zile yenye 4 wheel itapendeza bt ulaji wa mafuta unaongezeka pia.ukiwa na swali uliza tu maana naijua vilivyo hii gari
Umeeleza vizuri naomba pia ufafanuzi mzuri kati ya Toyota Noah field tourer ya 4wheel na 2wheel ktk
1. Fuel consumption
2. Uimara wake
3. Mambo ya kuzingatia ktk services

Kumbuka matumizi yake ni mizunguko barabara aina zote lami,v umbi, milima na corrugated road masafa mafupi na marefu pia kwa nyakati tofauti.

Unaweza ongeza mengine mhimu ambayo sijayaweka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Voltz iko poa. Kinaniudhi tu vile kina taa moja ya reverse. Sijui Toyota na General Motors walikula maharage gani wakati wa kukitengeneza.
 
Habari zenu wazeee wa chimbo. Nawatakia mapendo mema daima kati yenu

Kama kichwa kinavyojieleza
GARI : Toyota voltz 2003
ENGINE : 1790cc
MKANYAGIO : MANUAL
RANGI : Nyeusi
NAMBA YA GARI : DFZ
MAHALI ILIPO : DAR ES SALAAM
UIMARA NA UBORA : Ipo katika hali nzuri sana
SABABU YA KUUZA : Nataka kubadilisha aina ya gari
BEI : MILIONI KUMI NA MOJA NA NUSU (11.5M)


1550140256857-png.1022116



1550140385392-png.1022118
 
Back
Top Bottom