Mkuu toyota volz ni gari nzuri sana na imara pia ila uimara wake haufiki kwa Rav 4 old.
Utumiaji wake wa mafuta uko poa kwani ina cc1790 ambayo kawaida inakula 1lt/8-11km kutegemea na mwendo wa dereva.
Kwa upande Confitability iko poa sana ndani ina muundo kama Harrier.
Spear zilikuwa adimu kidogo ila kwa sasa naona zimeongezeka so usijali kuhusu hilo.
Nb:Kama barabara unayopita haina shida kipindi cha masika chukua yenye 2 wheel bt kama ni njia zetu zile yenye 4 wheel itapendeza bt ulaji wa mafuta unaongezeka pia.ukiwa na swali uliza tu maana naijua vilivyo hii gari