Ligi inaelekea ukingoni,ili kuongeza ushindani msimu ujao wadau na wapenzi wa mpira mnaonaje tukiipanua ikawa ya timu 16 badala ya 14 za sasa?
Tatizo sio idadi kuongezeka tu. Tuongeze udhamini kwa hizi timu pia. TFF ijaribu angalau kila timu ya premier league iwe na mdhamini binafsi makampuni yako mengi tu sidhani hata ka mkataba wa 50m itashindikana. Pia vodacom nao waboreshe udhamini wao. Kutoa jezi tu haitoshi. Suala la jezi lingebaki kwa klabu ili nayo ipate kuuza jezi zao ktk kuongeza pato. Wao watoe vifaa vingine n pesa izidi maradufu. From there ligi itakuwa na ushindani.
Ligi inaelekea ukingoni,ili kuongeza ushindani msimu ujao wadau na wapenzi wa mpira mnaonaje tukiipanua ikawa ya timu 16 badala ya 14 za sasa?
Mkuu unajua ulichoandika? Kama wachezaji wa Yanga walifukua hirizi uwanjani kuna tatizo gani hapo? Je hirizi ni mahali pake uwanjani?
Hapakuwa na hirizi eneo walilokuwa wanafukua, walifanya hivyo kwa kuwa waliaminishwa na mashabiki kuwa eneo hilo lina hirizi wakati hakuna kitu.
Sijaiona ripoti hiyo mzee wa Yanga, lakini kitendo cha hao wachezaji kufanya kitendo hicho inaonyesha timu yako inavyoamini ushirikina.
Washauri wenzako kuwa soka ni mchezo wenye nidhamu.
Sote tunaishi Tanzania, tunafahamu vema mazingira yetu. Pia kuna timu zimepigwa faini kwa vitendo vinavyoashiria ushirikina. Hivi uko Tz wewe?
Mh. rais, hilo ni wazo jema sana. Kwa sasa ligi yetu ni nyepesi mno kufuatia uchache wa timu. Ushindani ndani ya ligi sio halisi kwa vile bingwa huamuliwa baada ya mechi chache sana. Hii pia ina athari kubwa kwa wachezaji wetu kwa vile hawapikwi vya kutosha.
Maoni:
1. Hii iwe ni hatua tu katika kuelekea kurejesha ligi yenye timu 18-20.
2. Jaribuni kuona namna ya kuboresha zawadi ya ligi ili kuvifanya vilabu vitamani kuipata zawadi hiyo.
3. Angalieni ni jinsi gani ya kuvisaidia vilabu kupata udhamini wa uhakika ili tujenge ligi bora badala ya kola mdhamini kukimbilia Simba na Yanga tu.
4. Kada ya waamuzi isisahaulike. Tuanze kwa kujiuliza ni kwa nini hatutoi waamuzi kwenye michuano ya CAF?
Ninaamini tukijipanga vema, Tanzania ina nafasi kubwa ya kuwa na ligi bora kabisa afrika mashariki na kati.
Ligi inaelekea ukingoni,ili kuongeza ushindani msimu ujao wadau na wapenzi wa mpira mnaonaje tukiipanua ikawa ya timu 16 badala ya 14 za sasa?
Angalizo isije kuwa wazo linakuja sbb ya maamuzi ya rufaa iliyoipa nafasi stendi united na kuiengua mwadui sasa mkatafuta jinsi ya kuirudisha mwadui na kuongeza nyingine
Mjasiria Akili kilio cha kuongeza idadi ya timu za VPL hakikuanza leo,ni cha siku nyingi.
adakiss idadi gani ya timu inafaa kwa premier league,hilo ndilo swali langu,hitaji la kuongeza udhamini ni kweli na liko wazi.
Itawezekanaje kwa sasa wakati mdhamini anadhamini timu 14
Ndugu Rais wetu wa TFF mimi naunga mkono hoja yako timu ziongezwe msimu ujao zifikie 16 ila utaratibu wa kuzipata timu 2 za kukamilisha idadi hiyo uwe hivi
1.kwanza zile tatu za kushuka zishuke kama kawaida.
2. Zipande timu 5 badala ya 3.
3. Timu zilizoshika nafasi ya pili kila kundi (zipo 3) yani mwadui united, african lyon na jkt mlale nadhani zipambanishwe kupata timu mbili zitakazo ungana na Ndada FC, Polise Morogoro na stand United ya shinyanga kupanda ligi kuu.
Ndugu Rais unazungumziaje hizi tuhuma za AZAM kuhonga timu pinzani? inasemekana RUVU SHOOTING ilihongwa management yote kabisa.
Ndugu Malinzi,
Kuna uwezekano mkaamua kusimamia suala la vilabu kuwa na timu za watoto kwa nguvu kidogo? Au mtaendelea kuviacha vilabu vikicheza ligi bila kutimiza matakwa ya kisheria (sheria za soka).
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
ndugu yangu rushwa/hongo ni sawa na kutembea na mke/mme wa mtu,kikubwa ni kupata ushahidi kwa mambo yanayofanyika kwa siri.Kusema tu kuwa umesikia hivi na vile mwisho utashtakiwa kwa defamation.Siwezi kumhukumu mtu kwa maneno ya kusikia.
Ndugu rais nilitegemea nyie TFF wenye mpira wenu mtaanza uchunguzi kwa majibu yako mnataka kuletewa ushahidi hapo kwenye ofisi zenu katu hicho hakiwezi kutokea nadhani TFF inatakiwa kwenda extra mile juu ya hizi tuhuma na kuanzisha uchunguzi ikiwezekana kuanzisha kitengo maalumu cha kiinteligensia sio kusubiri ushahidi kama unavyotaka iwe ndiwe.
Lakini pia mnaweza kusaidiana na vyombo vinahusika na makosa ya rushwa kama PCCB kwa kuwapa semina na mafunzo viongozi wa mpira wa vilabu juu ya athari za rushwa kwenye soka, angalia kilichowatokea ITALIA ligi yao haina mvuto tena, je unakumbuka kilichowatokea ufaransa na ligi yao baada ya Marseille kushushwa daraja sasa ili suala si la kuangalia au kutolea majibu mepesi mepesi otherwise tuwe tumeamua kubaki tulipo, bora liende.
MKALIKENYA hivi wewe unadhani tumelala usingizi? We subiri....iko siku.