Maswali na ushauri kwa Malinzi

Mwaikimba Alitunyima Uhondo Sie tulioshindwa Kufika Ipinda-Mbeya..By the way Namtakia Maisha mema ya Ndoa na Mkewe (Rukia-was my school mate)..

Nilikuwepo kwenye hii harusi!Kijana wangu Mwaikimba katupa heshima hapa kijijini kwa kuachana na "ukapera"
 
Tuwe na subira ndugu zangu,mchakato unaendelea.
 
Revocatus Kashaga nakushukuru kwa kuliona hilo kuwa kwenye ligi ya mabingwa wa mikoa kuna vipaji,na sisi tulilijua hilo ndio maana kila kituo kuna mtu anatuangalizia vipaji.
Kuhusu website ya TFF ninakiri ina mapungufu makubwa na yanafanyiwa kazi,muda si mrefu itakuwa na uhai na itachangamka kuliko ilivyo sasa ikiwa na live updates.
 
ndugu rais, hongera kwa matokeo ya timu yetu kwa kuwatoa zimbabwe.
1. nn mipango ya ofisi yako juu maandalizi ya mechi ijayo?
2. hv mna mkakati gani wa kuwajenga kisaikolojia wachezaji kutolewa na sifa pindi wanapopata matokeo mazuri na kupata promo kubwa kutoka media mbalibali hasa magazeti?
3. nn majibu ya mwalimu juu ya tatizo la upingufu wa ufungaji magoli mengi hasa tukiwa uwanja wa nyumbani?
 
huwezi kuweka mipango hadharani, huko ni kuwatafunia au kuwafaidisha maadui hasa katika zama hizi za teknolojia ya juu na teknohama kwa ujumla
 
Rais Jamal Malinzi na watz wote hongereni sana kuvuka kiunzi hiki;mechi HAIKUWA easy kama labda wengi wanavyodhani hasa dakika 20 za mwisho,kwa kweli vijana walipambana na waheshimiwe!!

Ni imani yangu Kocha atafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza!Naiona kwa wazi kabisa safari ya Morocco mwakani
 
Last edited by a moderator:
Kama ambavyo huwa wanafanya wenzetu wa Afrika ya kaskazini wazimbabwe nao waliamua maproo wawe wasije Dar badala yake wapumzike waje watuchinjie Harare,uliwaona kina Katsande jana mambo yao.Kikosi cha Zimbabwe jana kilisheheni mastaa wa ulaya na ligi kuu ya PSL.
tunashukuru tumevuka salama,tujqipange kwa "mambas".
 


NOOJ maneno kidogo vitendo vingi.
 
Tumekwisha peleka barua CAF tunasubiri mrejesho.
Safi sana...kwahiyo serikali imetoa BARAKA zote...vipi uboreshwaji wa viwanja ..wizara ya Fedha au kupitia wizara ya michezo ...imeanza kutenga fungu/fedha kwa ajiri ya maandalizi ya kuboresha Viwanja?[ kama tutapewa nafasi]

Pia huu msaada wa kukarabati viwanja toka FIFA unahusisha PITCH tu na si sehemu zingine..kama Vyoo..Vyumba vya kubadilishia wachezaji na waamuzi..achilia mbali MAJUKWAA?
 
HONGERA SANA TANZANIA, MAENDELEO NI HATUA Jamal Malinzi

Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 122 hadi nafasi ya 113 kwa
mujibu wa orodha ya FIFA iliyotolewa hiyo jana.
Katika nchi za CECAFA Uganda inaongoza ikifatiwa,Ethipoia na Kenya Wakati barani Afrika nchi ya Algeria ikiibuka Kinara kwa kshika nafasi ya kwanza.
 
Last edited by a moderator:
Jamal Malinzi nina uhakia kocha wetu anaona mechi kama hizi za wapinzani wetu ili kufanyia kazi makosa yao!!

Insha allah akisaidia tukimtoa The Mambas inabidi tujipange vyema mno maana nawaona Zambia hapa na Japan wanacheza soka saafi sana!Ingawaje wenzetu wana wachezaji wengi ulaya lkn tukijipanga tunawaweza tu!Draw Lusaka na ushindi Dar ndiyo strategy

Full time:Zambia kapoteza kwa Japan,ni 4-3!Very entertained game!Zambia sio warahisi kuvuna points lzm tujipange kuanzia sasa!!
 
mkuu Jamal Malinzi kuna msemo wa kizungu unaosema"JUSTICE DELAYED IS JUSTICE DENIED" kwanini nasema hivi ndugu wambura aliwakilisha rufaa yake huko tff takribani wiki mbili sasa, na eti jana ndio kamati imekaa kupitia hiyo rufani na cha ajabu mpaka sasa hakuna majibu yeyote kutoka kwenye kamati, je kuna kigugumizi gani kufanya maamuzi ya haraka? huku kuchukua mda mrefu sana hauoni kuwa kunaleta maswali kwa wadau kuwa kuna maelezo hiyo kamati inangoja au wanapimia upepo umekaaje ili ndio watoe majibu?
ni vyema majibu yakatolewa kwa haraka na haki ionekana kutendeka kama vile FIFA walivyowatendea haki nyie bila kuangalia watu wangesemaje
 
Last edited by a moderator:

Ishu ya wambura I can term it as sensitive when it comes to soccer in Tanzania. Lazima Judge ajielekeze vizuri kwa umakini mkubwa kwenye sheria na si kukurupuka. Kumbuka kuna wadau wengi including particularly football hooligans! Ni wadau! Jaji asipokuwa makini anaweza ku-ruin his reputation!
 
Fainali za afrika za vijana finalists ni timu nane tu,hivyo unahitaji viwanja viwili vizuri tu na viwanja vinane vya mazoezi,vyote hivyo tunavyo.
msaada wa FIFA inategemea member association inaomba nini ila limit ni dola laki tano,ndio maana huko nyuma FIFA walitujengea hostel karume.
 
Ninaamini kikao cha kamati ya rufaa ya uchaguzi kitatupatia majibu ya rufaa ya Bw Wambura leo.
 
Ninaamini kikao cha kamati ya rufaa ya uchaguzi kitatupatia majibu ya rufaa ya Bw Wambura leo.

Kuna uzi humu kuwa Wambura ameshinda. This is great! Haki imetendeka. Sishabikii Wambura, ila ujinga wa mashabiki wa Simba na Yanga ukomeshwe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…