mkuu
Jamal Malinzi, nina maswali mawili siku ya leo
1. Tunafahamu fika ligi ya mabingwa wa mikoa inaendelea katika vituo 3 kama sijakosea, kituo cha mbeya, hapa Morogoro nilipo na kule Mwanza, je kuna jitihada gani za makusudi katika kuangalia upatikanaji wa vipaji kupitia michuano hii? binafsi nimeshuhudia mechi zote za hapa Morogoro, na nimeona Taifa lina hazina kubwa ya vipaji katika soka, je kuna maofisa wa TFF waliopo katika vituo hivi kuspot talent au ndio hii michuano mikubwa itapita hivi hivi
2. kwanini WEBSITE ya TFF haijapa kipaumbele hii michuano ya mabingwa wa mikoa katika eneo la upashanaji habari , nimepitia website ya TFF mara nyingi sijaona updates za matokeo ya mechi hizi kutoka vituo mbalimbali, sijaona picha kama wanavyofanya ktk mechi zengine na cha mwisho kikubwa zaidi sijaona misimamo ya timu katika vituo hivyo vitatu, je kukosekana kwa taarifa hizi muhimu si kuwanyima wadau wa mpira habari muhimu? maana hata vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kwa uchache sana juu ya michuano hii, na mpaka sasa sijaona gazeti lolote lililotoa misimamo ya timu katika vituo mbalimbali
ni hayo tuu kwasasa mkuu