Maswali na ushauri kwa Malinzi

halafu sio kiingilio tu, tiketi zinanunuliwa kwa kieletroniki ,kwa M-Pesa! Sasa jamani ni watu wangapi wanaweza kufanya hivo...yaani kwa kifupi WAMEFELI!
 
halafu sio kiingilio tu, tiketi zinanunuliwa kwa kieletroniki ,kwa M-Pesa! Sasa jamani ni watu wangapi wanaweza kufanya hivo...yaani kwa kifupi WAMEFELI!
chickmaget uongozi kweli ni kazi kubwa,watanzania kila siku mnalalamika mnataka tiketi za elektroniki,leo zinaletwa mnasema hamzitaki,lipi hasa tunalitaka,kununua tiketi ukiwa sebuleni nyumbani kwako au kupanga foleni juani?
 
Last edited by a moderator:
Mechi hii tiketi zinauzwa electronically na gharama yake ni kubwa kuliko kuuza manualy,inabidi gharama zifidiwe.
 
Mheshimiwa malinzi kuhusu ile project ya kuanza kuandaa mashindano kuanzia under 13 inabidi muitilie mkazo Sana kwani naamin hili ndyo itakuwa suluhisho la kudum la kupata timu ya uhakika ya taifa...nilikuwa naomba kujua project hii inaanza lini na nini mkakati yenu kuhakikisha project hii inakuwa na mafanikio
 
chickmaget uongozi kweli ni kazi kubwa,watanzania kila siku mnalalamika mnataka tiketi za elektroniki,leo zinaletwa mnasema hamzitaki,lipi hasa tunalitaka,kununua tiketi ukiwa sebuleni nyumbani kwako au kupanga foleni juani?

sio kwamba hatuzitaki...hapana! Issue ni kwamba mmeziharakisha mno. Hamjaelimisha watu jinsi inavofanya kazi , kwamfano mimi binafsi hata sijui jinsi ya kununua. Halafu pia hamuoni mngeacha kwanza mechi hii muhimu ipite kisha ndo muanze kutumia?
 
Last edited by a moderator:
Jamal Malinzi...leo asubuhi nimeona mkurugenzi wa ufundi wa timu za vijana...hasa U-17...Sterwart Hall akilalamika kuwa timu za vijana hazina hela...maandalizi duni kuelekea mechi na vijana wenzao wa south africa...

Source :chanel ten...
 
I wish ungejua tanuru ninalopitia kuhakikisha timu umri chini ya miaka 17 na 20 girls/boys na Twiga Stars zinashiriki michuano ya kimataifa. Hakuna udhamini na bado tunaziweka kambini tunazisafirisha Nairobi, Lagos, JBurg etc. Badala ya kulaumiwa tungepongezwa kwa kufanya tunachokifanya.

Kenya wamejitoa Africa U17 kisa gharama.
 
Jamal malinzi Ishu hapa sio gharama pekee why iwe mpesa tu? Unasema mtu kukaa sebuleni kwake kununua tiketi sawa jambo zuri lkn kuna tigo pesa,airtel money na zpesa lkn cha ajabu ni mpesa tu ndio inayitumika hamuini mmewapa wakati mgumu wasio na mpesa? Halafu hata marangazo yake ni kama hayapo
 
,,pole mkuu wangu ..hapa sikulaumu ila nilikua nataka kujua zaidi..kuhusu hizo timu jinsi mnavyoziandaa
Nitaongea na media Ijumaa hii, nitafafanua.
,,..itakua vizuri pia...kila la kheri...

.....helo helo TANZANIA....NAIAMINIA TANZANIA>>NAIAMINIA TAIFA STARS...
 
Mjasiria Akili itakuwa ni bahati mbaya kama hujapata taarifa za namna ya kununua tiketi.Tumeweka matangazo kwenye radio,blogs za akina michuzi,millard ayo,shafii,zubeiry etc,matangazo daily news,mwananchi,bingwa,tanzania daima etc.Bei ya tiketi ni sh 7000.- tu na unanunua hivi:
andika *150*00# kisha andika 4 kuandika namba ya kampuni andika 4 tena kisha ingiza namba ya kampuni 173399 baada ya hapo andika 7000 kisha andika 7000 tena na baadae bonyeza moja kuthibitisha malipo,utaletewa ujumbe na maxmalipo,au nenda kibanda chichote cha maxmalipo ununue au nenda steers au TFF karume au PPF tower utauziwa tiketi.
karibu tushangilie Taifa stars!!!
 
Last edited by a moderator:
Rais swali langu hapa ni kwa nini mpesa pekee wakati kuna tigo pesa,airtel money na zpesa je kwa walio nje ya vodacom hawawezi kununu tiketi sebuleni kwao
 
Rais swali langu hapa ni kwa nini mpesa pekee wakati kuna tigo pesa,airtel money na zpesa je kwa walio nje ya vodacom hawawezi kununu tiketi sebuleni kwao
swali zuri lkn nadhani jibu litakua ..Vodacom ndio wadhamini wakuu..so wamewapa kipaumbele....
ila tusubiri@Jamal Malinzi mwenyewe aje kutujibu vzr
 
swali zuri lkn nadhani jibu litakua ..Vodacom ndio wadhamini wakuu..so wamewapa kipaumbele....
ila tusubiri@Jamal Malinzi mwenyewe aje kutujibu vzr

Kwani vodacom ni wadhamini wa Ligi kuu au wadhamini wa TFF na Timu ya TFF nadhani kwenye hili mheshimiwa Malinzi muwe huru hao vodacom huo mkataba wao hauwabani TFF....I stand to be corrected.
 
Kwani vodacom ni wadhamini wa Ligi kuu au wadhamini wa TFF na Timu ya TFF nadhani kwenye hili mheshimiwa Malinzi muwe huru hao vodacom huo mkataba wao hauwabani TFF....I stand to be corrected.

Mkuu kwa mikataba hii ya kisiri siri tena ya kurithi..huwezi jua..hebu cheki jibu la rais hapa chini..

hahahaaha kibiashara swali tata hili!
 
Mpira wa miguu Tz Utaweza endeleaa kama Yanga Simba Na TFF vitapoteaaa Hapaa Duniani!!!.
 
Mpira wa miguu Tz Utaweza endeleaa kama Yanga Simba Na TFF vitapoteaaa Hapaa Duniani!!!.

Na hapo ndipo Timu ya Taifa itaanza kufurukuta kwenye anga za kimataifa kuliko porojo za sasa zinazoendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…