Maswali na ushauri kwa Malinzi

Hivi FIFA ina uwezo gani kuingilia hata ofisi?
 
Ngoja tusubiri tarifa rasmi za kimichezo leo.
 
Wadau nimeiona hii kwenye Facebook page ya mwanaspoti
FIFA imeitaka TFF kuanza mchakato wa kuhamisha ofisi katikati ya Jiji na kurudi Ilipokuwa awali na ndani ya masaa 24 mchakato huo uwe umeanza

Kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 10/aug TFF tulipokea na kuwa na ujumbe wa wataalam sita toka FIFA.Wataalam hawa walikuwa ni wa ufundi,utawala,masoko na maendeleo ya mpira.Jukumu kubwa la ujumbe huu ilikuwa ni kutathmini muundo na utendaji wa shirikisho lengo likiwa ni kutafuta namna bora ya kuongeza ufanisi katika utendaji wa shirikisho.Wadau mbali mbali walikutana na ujumbe huu akiwemo Mh Waziri mwenye dhamana ya michezo,wadhamini wa sasa na wa zamani,vyombo vya habari,vilabu vya ligi kuu,viongozi wa TFF wa mikoa,watendaji wa TFF n.k.
Baada ya kukutana na wadau kadhaa kikao cha pamoja kilikaa kati ya kamati ya utendaji ya TFF na ujumbe wa FIFA na kufanya mapitio ya kile FIFA walichokiona.Maeneo makuu yaliyopitiwa ni pamoja na utawala na fedha,maendeleo ya mpira,mashindano na timu za Taifa.Mwisho wa kikao maazimio yalipitishwa juu ya mpango endelevu wa shirikisho na moja lilikuwa ni kuboresha mazingira ya utendaji kazi na usimamizi wa maendeleo ya mpira.Katika kipengele hiki ilionekana ni busara TFF irudi Karume lakini iboreshe mazingira ya ofisi ili yakidhi mahitaji ya kufanyia kazi .Aidha kwa kuzingatia mahitaji ya kiuchumi ya shirikisho FIFA wamekubali kushirikiana na TFF ,kupitia miradi yake mbali mbali, katika kuanzisha na kujenga miradi ya kiuchumi Karume.TFF itahakikisha hili linafanyika.
 

Hon. Eng. President Jamal Malinzi pamoja na mapungufu yako uliyonayo kama binadamu mwingine, you are the man of this time.

Asante kwa kuliweka sawa hili jambo la kurejesha ofisi za TFF pale Karume.
 
Last edited by a moderator:
Hon. Eng. President Jamal Malinzi pamoja na mapungufu yako uliyonayo kama binadamu mwingine, you are the man of this time.

Asante kwa kuliweka sawa hili jambo la kurejesha ofisi za TFF pale Karume.

Hivi zilihamia wapi..
 
Last edited by a moderator:
Vema na huu ndio uongozi kuwa mwepesi wa kujibu
 
komeko heshima kwako mkuu, hawa simba na yanga ndo wanaharibu soka letu, miaka 70 hakuna maendeleo ya maana!
 
Fifa yairudisha TFF Karume

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limekerwa na matumizi mabaya ya fedha ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kulitaka kurejesha ofisi zake kwenye Uwanja wa Karume.

Uongozi mpya wa TFF ulihamishia ofisi zake kwenye jengo la PPF Tower jijini Dar es salaam ukisema kuwa ungejenga jengo la kisasa kwenye uwanja huo mkongwe ambako ndiko makao yake makuu.

Fifa yairudisha TFF Karume - Michezo - mwananchi.co.tz
 
Anza mchakato wa kuhakikisha sera ya michezo inabadilika na Michezo yote iwe ni proffessional na iwe sehemu kubwa ya kukuza biashara.
 

Belo usipoteze matumaini,ninaongoza mpira katika mazingira magumu,lipo kundi dogo linataka niongoze mpira kwa kutatua crisis badala ya kuhangaika na mpango kazi wa maendeleo,usitishie shaka nina uwezo wa kulikabili,tutashinda na mpira utasonga mbele.Wanaodhani Malinzi atakata tamaa wajue hawatafanikiwa.Karume complex tutaijenga,youth development programme tutaijenga,mpira wa wanawake tutaujenga na Tanzania itang'ara kimataifa.
 
Last edited by a moderator:

Actions speak louder than words!
 
Rais@Jamal Malinzi...naomba ufafanuzi juu ya HABARI..za Tanzania kupitia tff kuomba kuwa mwenyeji wa AFCON...nimeona ktk moja ya group kule Facebook.....pia leo hii gazeti la MWANANCHI limelipoti kuwa KENYA kupitia rais wa fkf kuwa EAC tunaomba kuandaa AFCON kwa pamoja....je huu mpango ni wapamoja au sisi NIA yetu ni kuandaa wenyewe..?..
 
Hili la viwanja VIPI..?! kwa mfano jamhuri morogoro hata huu wa sabasaba.. Ni muhimu kuboresha MIUNDOMBINU YA MICHEZO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…