Maswali na ushauri kwa Malinzi

Maswali na ushauri kwa Malinzi

Mr President Malinzi

Nimesoma kwa masikitiko makubwa saana jinsi swala la Yanga kupeleka timu ya vijana lilivyokuwa handled na TFF baada ya maagizo ya katibu wa CECAFA, Mr MUSOKE.

1) Mashindano yamepangwa katika wakati mgumu, kwa timu washiriki
2) Kama nia na lengo ni kuibua wachezaji, sasa kosa la Ynga ni lipi?
3) Inamuhusu nini MUSOKE kusema haiwezekani Yanga ije na kocha mwingine?

Rejea yote haya, ni fedheha kubwa jinsi TFF ilivyolishughulikia hili swala.

Afisa wa TFF, aliyeshiriki kutoa uamuzi na kuwapeleka AZAM, anastahili kusimamishwa kazi au Ajiuzulu, haiwezekani ifike Musoke aanze kuamua jinsi ya uendeshaji na ujenzi wa soka katika taifa letu.

Hii ni aibu kwa nchi, wewe kama Rais wa TFF, onyesha kutokubali kuingiliwa katika masuala ambayo hayana sheria.

Baada ya Yanga kukataliwa Tanzania hatukuwa tayari kupoteza uwakilishi.
 
Ni udhaifu pia wa uongozi wa TFF. 'Mtu akikuambia jambo la kipumbavu, nawe ukalikubali, anakudharau' (J. K.Nyerere, n.d.). CECAFA wamewaambia jambo la kipumbavu TFF kuwa Yanga hawana sifa ya kushiriki mashindano eti kwa sababu wanapeleka kikosi B huku TFF wakijua fika kuwa wale ni wachezaji halali wa Yanga. Kwa kitendo cha TFF kukubali upumbavu ule, CECAFA imewadharau kana kwamba TFF haina viongozi ndiyo maana CECAFA iliwataka TFF wawaandikie barua Yanga na wao kukaa pembeni nje ya tatizo. Nashangaa ni kwa nini viongozi wa TFF hawajaomba radhi hadi sasa kwa kukubali upumbavu ule. CC. Jamal Malinzi (Mkuu una utetezi gani katika hili?).

Makoye Matale politics za mpira ukanda wetu ni zaidi ya uzijuavyo.
 
Last edited by a moderator:
Baada ya Yanga kukataliwa Tanzania hatukuwa tayari kupoteza uwakilishi.

Kulikuwa na umuhimu kupoteza ushiriki, kama tunataka wajue tunataka kufanya nini? utapataje timu ya vijana kwa mipango hii? Hivi unajua mara nyingi Brazil kwenye kombe la Latin America mara nyingi wanajaza 75% vijana kuwa taarisha kwa world cup?

Haya mashindano sasa ndo utaona kwa nini ukanda huu unasua sua, mtu mzima anauliza mbona Maximo haji,?
 
Kipaji Halisi hili la Yanga na cecafa siai kama federation we tried our best kuokoa situation na hili Yanga wanajua,walichoamua cecafa ndo hicho.

Hapa kuna walakini inakuaje cecafa ikatae wachezaji walio na leseni zilizotolewa na chama cha soka cha husika na chama hicho hicho kishindwe kuitetea klabu husika!
 
Last edited by a moderator:
Malinzi
Naomba nitoe ushauri wangu kwa ajili ya kukuza mpira wa Tanzania
1. Kwanza idadi ya timu za premier ziongezeke ili wachezaji wacheze mechi nyingi zaidi
2. Kuanzishwe ligi nyingine ya timu za vijana za vilabu vyote vinavyoshiriki ligi kuu na ligi daraja la kwanza na ligi hiyo iende sambamba na ligi kuu
3. Uongozi wa TFF utafute wadhamini na kuwe na makato ya asilimia flani katika mechi zote za premier ili kuendesha ligi ya vijana
4. Kuwe na mkakati maalumu wa kupandisha vijana kwenye premier kila mwaka kwenye usajili wa vilabu hii itatuwezesha kupata timu bora ya taifa na yenye uzalendo.
Naomba niambie kati ya haya lipi linawezekana na lipi haliwezekani na kwa sababu zipi mkuu?

isaryalande yote manne ni muhimu na yanafanyiwa kazi:
1.Kuanzia msimu 2015/16 ligi kuu itakuwa na timu 16 badala ya 14
2.Tunandaa ligi ya umri chini ya miaka 20,itakwenda sambamba na ligi kuu,ila mkondo mmoja
3.Taratibu za mapato ya ligi kutumika for youth football development yanafanyika
4.Tayari kanuni za ligi kuu zinaruhusu vijana kupandishwa daraja madirisha yote ya usajili
nakushukuru sana kwa mchango wako.
Kubwa vilabu vyetu vihimizwe kuwa na programu nzuri na endelevu za mpira wa vijana.
 
Last edited by a moderator:
Hapa kuna walakini inakuaje cecafa ikatae wachezaji walio na leseni zilizotolewa na chama cha soka cha husika na chama hicho hicho kishindwe kuitetea klabu husika!

ndugu yangu hapa tutakesha,naomba ukubali tu kuwa maji yamekwisha mwagika,tugange yajayo
 
Anzisheni ligi za shule, kuanzia primary, kwa wilaya hadi taifa na mzi-fund team na waalim wa soka shuleni.

Vipaji vianze kuibuliwa kuanzia mtu anapoanza darasa la kwanza.

Bila hivyo, hata miaka 100 ijayo hamtafika fainali za Afrika wacha za Dunia.

Kinachotakiwa muwe na plan, iliyojaa uwazi na mapato na matumizi yanayoonekana wazi, na muweke board ya soka kila shule kutokana na hao hao wazazi na si watu kutoka TFF. TFF wawe wasimamizi tu wa hiyo plan na kutoa technical know how. Nakuhakikishia hakuna mtu ambae atakataa kusaidia team ya shule ya mwanawe.

Aaah, nione mjukuu wangu kavaa jezi ya shuleni kwao, halafu nisiwe fan wa hiyo shule? Na hapo ndipo mtakapotuona akina mama tukijazana viwanjani kuwa support watoto / wajukuu zetu. Fikiri.

Achaneni na haya mavilabu, yameshakuwa vituo vya ulaji na kujitafutia umaarufu na matajiri watashindana kuyaendesha, nyinyi mnatakiwa focus yote iwe primary schools.

Nakwambia mkianzisha hiyo ligi ya primary chools, kila darasa na ligi yao, I mean, lakwanza ligi yao, la pili, tatu, nne, tano, sita, saba.

Utaona jinsi shule za sekondari za kulipia zinavyokuja kuwapa offer za scholarship watoto wanaomaliza darasa la saba, kwa soka tu.

Jaribuni muone, Tena Jamal Malinzi hii plan nnayokupa itakufanya uwache historia Tanzania, kuwa wewe ndiye uliyelifufua soka. Bila hivyo, bure tu.

Usisahau kukumbuka kuwa hii ni plan iliyotolewa na FaizaFoxy wa JF na muiite the FaizaFoxy Soccer Plan.

Simple and achievable plan.
 
ndugu yangu hapa tutakesha,naomba ukubali tu kuwa maji yamekwisha mwagika,tugange yajayo

Mh kijiografi na kihistori tuna nafasi ya kuwa wanachama wa chama cha soka kusini mwa afrika COSAFA,na mara nyingi jamaa washatuinvite ktk mashindano lkn kwa interest za uongozi uliopita walikuwa wakikataa kushiriki,mh kama una nia ya dhati ya kukuza mpira wa nchi yetu ungekaa na wizara husika ili tujitoe cecafa na kujiunga COSAFA,hii nafasi iwapo km wangekuwa nayo kenya siku nyingi wasingekuwepo cecafa km walivyojitoa zambia na malawi,yote kwa yote mh itendee haki nchi yetu kwa kujitoa cecafa
 
Anzisheni ligi za shule, kuanzia primary, kwa wilaya hadi taifa na mzi-fund team na waalim wa soka shuleni.

Vipaji vianze kuibuliwa kuanzia mtu anapoanza darasa la kwanza.

Bila hivyo, hata miaka 100 ijayo hamtafika fainali za Afrika wacha za Dunia.

Kinachotakiwa muwe na plan, iliyojaa uwazi na mapato na matumizi yanayoonekana wazi, na muweke board ya soka kila shule kutokana na hao hao wazazi na si watu kutoka TFF. TFF wawe wasimamizi tu wa hiyo plan na kutoa technical know how. Nakuhakikishia hakuna mtu ambae atakataa kusaidia team ya shule ya mwanawe.

Aaah, nione mjukuu wangu kavaa jezi ya shuleni kwao, halafu nisiwe fan wa hiyo shule? Na hapo ndipo mtakapotuona akina mama tukijazana viwanjani kuwa support watoto / wajukuu zetu. Fikiri.

Achaneni na haya mavilabu, yameshakuwa vituo vua ulaji na kujitafutia umaarufu na matajiri watashindana kuyaendesha, nyinyi mnatakiwa focus yote iwe primary schools.

Simple and achievable plan.

FaizaFoxy ahsante kwa wazo jema,we are also thinking along those lines.Nchini mwetu tuna shule za msingi yapata 19600,our plan ni kuandaa mtaala wa kufundisha mpira nchini ili kila shule ifundishe mpira unaofanana na tuhakikishe kupitia TAMISEMI kila shule inakuwa na mwalimu wa mpira/michezo pamoja na kupata mipira ya size stahili (size 3 na 4).Pia ni muhimu kuwa na tournament za uhakika za mpira wa watoto na vijana.Yote kwa yote huwezi kutenga vilabu kwa sababu baada ya kuvuka umri wa miaka 17 lazima vijana hawa wapate vilabu vya kuchezea.
 
Last edited by a moderator:
Mh kijiografi na kihistori tuna nafasi ya kuwa wanachama wa chama cha soka kusini mwa afrika COSAFA,na mara nyingi jamaa washatuinvite ktk mashindano lkn kwa interest za uongozi uliopita walikuwa wakikataa kushiriki,mh kama una nia ya dhati ya kukuza mpira wa nchi yetu ungekaa na wizara husika ili tujitoe cecafa na kujiunga COSAFA,hii nafasi iwapo km wangekuwa nayo kenya siku nyingi wasingekuwepo cecafa km walivyojitoa zambia na malawi,yote kwa yote mh itendee haki nchi yetu kwa kujitoa cecafa

uanachama wetu cecafa ni wa kisiasa na kihistoria kuanzia enzi za Gossage tukipigania uhuru.Mwaka huu tuliwaomba cosafa watualike nafasi ikawa ngumu (wamealika Ghana ).Hata hivyo usidhanie kote ni shwari,changamoto za uongozi ziko kila mahali,ni kukabiliana nazo tu.
 
Nimebaki na maswali lukuki baada ya kusoma jibu hili toka kwa Rais wa TFF.

Hilo jibu maana ake ''Kuna mengi nyuma hatuyajui kuhusu CECAFA Na suala zima la Yanga''

Mi Binafsi Nimeelewa sana.
 
FaizaFoxy ahsante kwa wazo jema,we are also thinking along those lines.Nchini mwetu tuna shule za msingi yapata 19600,our plan ni kuandaa mtaala wa kufundisha mpira nchini ili kila shule ifundishe mpira unaofanana na tuhakikishe kupitia TAMISEMI kila shule inakuwa na mwalimu wa mpira/michezo pamoja na kupata mipira ya size stahili (size 3 na 4).Pia ni muhimu kuwa na tournament za uhakika za mpira wa watoto na vijana.Yote kwa yote huwezi kutenga vilabu kwa sababu baada ya kuvuka umri wa miaka 17 lazima vijana hawa wapate vilabu vya kuchezea.

Hayo ya mtaala ni mawazo (samahani sana) ya kijinga, time consuming na unachievable at all.

Nnachokwambia mimi ni very simple and straight forward. Kila shule ya msingi inakuwa na timu saba. Na wazazi ndio wanaziendesha, ukiwaita wazazi kesho, wiki ijayo tayari una team saba na mipira na kila kitu, na kila mmoja atajitahidi kwa njia yake, na vitu vitaanza kesho, hiyo bureaucracy ya mitaala ndiyo mnazidi kurudisha nyuma soka, soka linahitaji action siyo maneno.

Nyinyi watu mbona fikra zenu zinakuwa kwenye mambo yasiyotekelezeka? hivi huwa mnafikiri kinyume-nyume?

Be practical.

Wacheni kujitafutia manjia ya ulaji, tafuteni njia za kukuza soka.
 
ndugu yangu hapa tutakesha,naomba ukubali tu kuwa maji yamekwisha mwagika,tugange yajayo
Nakukubali kitu kimoja tu kuwa active JF, hadi mimi wa Mlooo Mbeya nakusoma ila maswala ya Mengine ya soka wewe ni walewale tu.

Toa jibu la msingi hadi Yanga inaondolewa kagame na Msonye TFF mlifanya juhudi gani kama wasimamizi na watetezi wa soka la Tanzania.?
 
uanachama wetu cecafa ni wa kisiasa na kihistoria kuanzia enzi za Gossage tukipigania uhuru.Mwaka huu tuliwaomba cosafa watualike nafasi ikawa ngumu (wamealika Ghana ).Hata hivyo usidhanie kote ni shwari,changamoto za uongozi ziko kila mahali,ni kukabiliana nazo tu.

Hatuna haja ya kuomba mualiko wa mashindano,sisi tuna vigezo vyote vya kuwa wanachama wa cosafa,tunachotakiwa ni kuomba uanachama,nafahamu kama changamoto za uongozi zipo kila mahali lkn haya magumashi cecafa ya kutegemea mapato ya mlangoni cdhani kama na cosafa yatakuwepo
 
Hayo ndio yanawafanya msikosoleke, sasa kama ya kijinga nisikwambie ya kijinga? staha katika ukweli? ndio maana mpaka leo ni kichwa cha mwendawazimu.

Usipoukubali ukweli hutaendelea hata siku moja. Ujinga ni ujinga tu hauna jina lingine.
tatizo hawajui hasira za wadau mitaani.
 
Back
Top Bottom