Maswali na ushauri kwa Malinzi


Kwangu binafsi mheshimiwa sioni kama kuna baya lolote mlilolifanya kwakua kwa mara ya kwanza ndio nimeona sheria imefuatwa katika kamati zote za tff tokea ianzishwe,huo ni ushindi mkubwa na heshima kwako,ushauri wangu leo utaambatana na mapitio ya baadhi ya matukio ya kiuongozi hapo tff.
1)Mpango wa maboresho ya timu ya taifa kwangu mimi ulikua ni bora na mlifanya vibaya kuuacha kwakua hamkuupa muda kuacha ufanye kazi,tatizo kubwa hapa mnafanya kazi kwa kuangalia waandishi wanaandika nini kwenye magazeti na kwenye makala zao uchwara,leo hii waandishi haohao kwa kupitia mlango wa nyuma wameanzisha ndondo cup halafu wachezaji haohao wa maboresho ya stars watang'ara kule na wao watajitokeza kwenye magazeti na redio zao kujisifu kuwa wameibua vipaji,vipaji gani?,ni hivyo ninyi mlivyoviacha kwakua wao waliponda.
2)Mpango wa kuanzisha ligi daraja la pili ni mzuri lakini hakikisheni mnawatafutia wadhamini hili ni pamoja na ligi daraja la kwanza,na hapo ndipo mtakapoona ubora wa ligi na wachezaji watakuwa fiti,halafu hapohapo ningekushauri pia muanzishe kombe la shirikisho ambapo mtajumuisha na hizi timu za daraja la pili na la kwanza,wadhamini wakiwa haohao wa stars au hata wizara ya michezo hii itasaidia kuibua vipaji vingi na hata kocha wa timu ya taifa atakuwa na uwanja mpana wa kuchagua timu ya taifa kwakua wachezaji watakuwa wengi na fiti pia.
3)Hili la ratiba sijui nini kilitokea lakini mmekosea na pia mjipange ili lisijirudie.
4)Achana na siasa za waandishi na wapambe kuhusu masuala ya taifa stars,suala la kuhujumiwa hili litakuharibia malengo yako mengi kwakuwa halina ukweli ndani yake,stars haikufanya vizuri tokea mwaka 1980 mimi sijazaliwa,mwl nyerere ni rais,wahujumu wapatikane leo miaka 34 baadae si kweli,miaka yote ya nyuma FAT ilikuwa malumbano na migongano amani imepatikana juzijuzi kwanini tusifikirie hapo,mipango endelevu ndio msingi wa maendeleo sehemu yote ile haya mambo siku hizi hayana nafasi.
5)Mwisho hiyo mipango uliyoeleza hapo wakati unamjibu mchangiaji ya kuanzisha vituo 25 vya michezo ambavyo nafikiri vitatilia mkazo soka la vijana ikianza chukueni ule ushauri ulio bora kutoka kwa yeyote iwe mwandishi au nani na acheni kuchanganyikiwa na maoni ya waandishi uchwara wa magazeti wengine wanastress za uchaguzi.
HONGERA KWA KAMATI BORA KABISA YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI,NI HAYO TU,HESHIMA KWAKO MKUU.
 
Last edited by a moderator:
unachoshindwa kuelewa kwmba tff hawana maamuz yoyote juu ya kagame cup

Hivi unajua kweli mambo ya Soka ama unaongea unazi tu?

Mashindano ya Kagame yapo chini ya CECAFA na CECAFA inaundwa na vyama vya soka vya nchi husika

timu yoyote ya Tanzania inayoshiriki mashindano ya CECAFA inawakilishwa na TFF,
kwa taarifa yako
1. majina ya timu zote zinazoshiriki Kagame Cup huwa yanapelekwa na TFF
2. majina ya Wachezaji wote watakaoshiriki mashindano ya Kagame yanawakirishwa na TFF
3. Mabadiriko yoyote ya Timu itakayoshiriki mashindano ya Kagame yanakuwa chini ya TFF
4. CECAFA walipoitoa Yanga, waliwaambia TFF walete timu nyingine na wala Azam hawakujipeleka wenyewe Rwanda, TFF ndio walioichagua Azam,
5. TFF wangeweza kuchagua timu yoyote nje ya Azam kwa vigezo vyovyote na CECAFA wasingekataa
 
{kuna tatizo gani ikichaguliwa azam ? kwa hyo ulitka tff waichague hta mbeya city ilimradi roho yako iridhike acha chuki mkuu na ubaguzi azam km ilivyo timu na yenyewe ina haki sawa na timu nyingineo}
 
{kuna tatizo gani ikichaguliwa azam ? kwa hyo ulitka tff waichague hta mbeya city ilimradi roho yako iridhike acha chuki mkuu na ubaguzi azam km ilivyo timu na yenyewe ina haki sawa na timu nyingineo}

Naomba niwe wazi kwako Sikuelewi unasimamia wapi na unataka kujua nini?
mi nimemalizana na wewe Mkuu
 
Rais jamal...hili suala la vilabu kutakiwa kukatwa shilingi 500 kwa kila tiketi...kutoka ktk fedha za mgawo wa wadhamini...?...LIMEKAAJE..?.

Chanzo...Mwananchi la leo..uk 32..
 
Rais jamal...hili suala la vilabu kutakiwa kukatwa shilingi 500 kwa kila tiketi...kutoka ktk fedha za mgawo wa wadhamini...?...LIMEKAAJE..?.

Chanzo...Mwananchi la leo..uk 32..

huo ni wizi mpya umeanza.....
 
Jamal malinzi,
Kwa nn kila siku mnazidi kuja na mambo mapya bila kushirikisha wadau
Mmekuja na kanuni mpya kwenye ligi kuu bila kushirikisha vilabu matokeo yake mmeingeza vitu ambavyo hawavitaki ukiacha hilo
Mnajua kabisa mikataba ya wadhamini vodacom na azam inasema nini ghafla mnaibuka na kutaka kukata asilimia 5 ya pesa za vilabu hamuoni mnaweza kuwakimbiza wadhamini?
Mikataba inajieleza kila kitu nani anapata nini lkn bila kuwashirikisha wenye fedha zao mnaibuka tu mnataka kuwadhulumu hivi mpo hapo kww maslahi ya soka kweli?
Yani kwa kanuni mpya za makato DRFA wanapata mapesa mengi kuliko hata bodi ya ligi
Hii aibu
 

ahsante nashukuru kwa ushauri
 
Sijui kama utaweza kutushawishi kwenye swala la 5% mnazotaka kudhulumu vilabu kwenye pesa za udhamini
Kama ishu ni youth development kwa nn msiwalazimishe vilabu watilie mkazo hili na nyie kuwasimamia kiukamilifu ikiwepo kutafuta wadhamini wa uhakika ni sio nyie kuingia kwenye kazi ambayo si yenu
 
Last edited by a moderator:

nitakua na maswali baada ya huo mkutano...tunasemaga..'subira huvuta heri'....
 
Kama nilivyosema mwanzo sidhani kama utaweza kutushawishi kuhusu uamuzi wa kimabavu wa kukata 5% kwa majibu mepesi eti mwenyekiti wa bodi ya ligi makamu wake na katibu walikuwepo mkipisha kwani hawa ni wajumbe wa kamati ya utendaji wa tff? Hata kama walikuwepo walikua na uwezo wa kuwapinga? Ua walikuja baada ya mashauriano na wenzao?
Kama sina hakika kama toka muingie ofisini mmeweza hata kuvuta mdhamini mpya zaidi ya wale wale walioachwa na kina tenga kama kweli mnamipango ya vijana kwa nini msishawishi wadhamini wapya wakaja kuwasaidia kwenye huo mpango
Hapo kuna kitengo cha masoko kina kazi gani mpaka sasa kimefanya
Kifupi mmeanzisha mgogoro mkubwa mno ambao hamtaweza kuukabili ni hiki ni kituko kingine katika utawala huu mpya
Kama wadhamini wapo serious muda wowote hatutashangaa wakivunja mikataba na kuwaachia mipango yenu isiyo na dira na faida kwao
 
Nimeona zinazoitwa kuwa hoja za TFF kukata asilimia tano za udhamini. Kwangu mimi hilo ni porojo (rhetoric) na sio hoja. Kinachojaribu kufafanuliwa na porojo hilo ni uhalali wa TFF kisheria kukata mapato hayo. Lakini porojo hilo halijaribu kushawishi sababu za bajeti ya mfuko wa kuendeleza vijana kuchangiwa kwa 5% na fedha za udhamini. Kwani jukumu la vilabu au wadhamini ni kuendeleza vijana? Hilo ni jukumu la TFF na lipo daima. Huku Zanzibar kuna ligi za Juvenile, Junior na Central. Zinaendeshwa na Kamati zao mahsusi, ambazo zina mipango yake ya kujiendesha. Akina Cannavaro na aggrey Morris ni mazao ya utaratibu huu (wakitokea 'vitimu' vya AC Milan na New Nistu). Huko ndio kuendeleza vijana. Si sahihi TFF kutumia uwezo iliyojipa wa kutunga kanuni za Ligi kwa kujipendelea huku mkiviumiza vilabu. Mnaweza kuwa na uwezo, madaraka na mamlaka ya kufanya yote hayo. Lakini hiyo ni sawa na absolute power, which corrupts absolutely. Chondechonde, hekima itawale na sio kiburi. Mpeni Mungu kilicho cha Mungu, na Kaizari kilicho cha Kaizari. Vinginevyo tusishangae wadhamini nao wakasita kugharimia vilabu kwa sababu fedha zao zinatumika nje ya makubaliano. Sikatai TFF ina nia njema katika hili, lakini njia ya jehanamu imejaa tele nia njema.
 

mwangalimungu nashukuru umeliona hili la umuhimu wa youth football development.Leo unaongelea vilabu kuendeleza soka la vijana,hivi ukiondoa Azam ni klabu gani ya premier league ina academy?
 
Last edited by a moderator:
Makato ya 5% kutoka fedha ya wadhamini wa ligi kuu itawaletea mgogoro ambao hamjautarajia kabisa, vilabu vinalalamika jinsi makato ya gate collections yalivyo makubwa bado hamjaweka sawa hilo mnahamia tena kwenye fedha zao za udhamini, na kama hili mtafanikiwa sitashangaa tena mtakapoamua kukata na fedha zao za udhamini binafsi wa kila klabu. Kaeni upya mfikirie na kutafuta vyanzo vingine. Labda Ndugu Malinzi uniambie hivi ilikuwaje Safari Lager wakaacha kudhamini ligi kuu?
 
mwangalimungu nashukuru umeliona hili la umuhimu wa youth football development.Leo unaongelea vilabu kuendeleza soka la vijana,hivi ukiondoa Azam ni klabu gani ya premier league ina academy?
Swala la Youth Football Development halipaswi kuwa ni mzigo wa vilabu. Vinaweza kuwa na sera ya kutotumia kabisa vijana na kutumia masongwangwe (magalacha - galasticos) moja kwa moja. Je, kwa Katiba, sheria na kanuni za sasa za TFF hilo lingekuwa ni kosa? Youth development lilipaswa kuwa ni sera ya TFF yenyewe, ambayo baadaye ingetungiwa sheria na hatimaye kanuni. Ilipaswa kuwa ajenda ya uchaguzi kwa yeyote anayetaka kuongoza TFF, ajenda ambayo ingesema waziwazi ni vipi angegharimia Youth Development iwapo atachaguliwa. Kuchaguliwa kwake kungemaanisha kwamba wadau, vikiwamo vilabu, wameridhia mikakati hiyo. Tungewashangaa kulilalamikia hilo wakati wa utekelezaji utapofika, kama tunavyoishangaa TFF inavyokurupuka hivi sasa kulazimisha makato hayo bila ya kuliazimia hilo waziwazi wakati wa kampeni za kuingia madarakani. Nina hakika hamkuwa wawazi na wakweli kulisema hilo wakati huo kwa sababu mlijua msingechaguliwa na vilabu. Maana yake ni kwamba hivi sasa mnaviendea kinyume. Kuna njia nyingi za kuchangia maendeleo ya soka la vijana bila ya kuvikamua vilabu pekee. Mlipaswa kwanza kuomba ushauri wa wadau, wakiwamo wana JF, juu ya namna bora ya kufanya hivyo. Kwahivi mnavyofanya, mnakuwa ni watawala na sio viongozi; kana kwamba vilabu viko chini yenu ilhali ni wanachama wenu. Mnaweza kuamua hivyohivyo kwa makocha na marefa?
 
watanzania watu wa ajabu huwa wanataka timu zao wacheze kama timu za ulaya au misri au afrika magharibi bila kujua uandaaji wa mchezaji ulianzia wapi. hata hivyo vilabu vinavyolalamika ukiuliza wana timu wa vijana hawana wanaokota kutoka mitaani
shime vilabu tff inawaandalia wachezaji kuliko kung'ang'ania akina okwi na kupata timu bora ya taifa nawaombeni mkubali hiyo asilimia tano hoja ni kuwataka tff kuomba kuongeza wadhamini au waliopo waongeze dau
 
uliahd akichaguliwa atatafta wafadhili for youth na ligi za wanawake,wafdhli wenyewe ndo wamekuwa virabu?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…