Majuzi Hollyman alifungua thread ya aina hii.Nia na lengo lake lilikuwa ni zuri,namshukuru.Nimeamua nifungue mwenyewe hii thread ili iwe ni uwanja wa kudumu wa kuniuliza maswali,kutaka ufafanuzi na pia kutoa ushauri kuhusu maendeleo ya mpira wetu.Kwa ruhusa ya moderators ninaomba uwe ni ukurasa wa kudumu hapa jf.
Jamal Malinzi
Rais wa TFF
Dar es salaam 04/Feb/2014
Kwangu binafsi mheshimiwa sioni kama kuna baya lolote mlilolifanya kwakua kwa mara ya kwanza ndio nimeona sheria imefuatwa katika kamati zote za tff tokea ianzishwe,huo ni ushindi mkubwa na heshima kwako,ushauri wangu leo utaambatana na mapitio ya baadhi ya matukio ya kiuongozi hapo tff.
1)Mpango wa maboresho ya timu ya taifa kwangu mimi ulikua ni bora na mlifanya vibaya kuuacha kwakua hamkuupa muda kuacha ufanye kazi,tatizo kubwa hapa mnafanya kazi kwa kuangalia waandishi wanaandika nini kwenye magazeti na kwenye makala zao uchwara,leo hii waandishi haohao kwa kupitia mlango wa nyuma wameanzisha ndondo cup halafu wachezaji haohao wa maboresho ya stars watang'ara kule na wao watajitokeza kwenye magazeti na redio zao kujisifu kuwa wameibua vipaji,vipaji gani?,ni hivyo ninyi mlivyoviacha kwakua wao waliponda.
2)Mpango wa kuanzisha ligi daraja la pili ni mzuri lakini hakikisheni mnawatafutia wadhamini hili ni pamoja na ligi daraja la kwanza,na hapo ndipo mtakapoona ubora wa ligi na wachezaji watakuwa fiti,halafu hapohapo ningekushauri pia muanzishe kombe la shirikisho ambapo mtajumuisha na hizi timu za daraja la pili na la kwanza,wadhamini wakiwa haohao wa stars au hata wizara ya michezo hii itasaidia kuibua vipaji vingi na hata kocha wa timu ya taifa atakuwa na uwanja mpana wa kuchagua timu ya taifa kwakua wachezaji watakuwa wengi na fiti pia.
3)Hili la ratiba sijui nini kilitokea lakini mmekosea na pia mjipange ili lisijirudie.
4)Achana na siasa za waandishi na wapambe kuhusu masuala ya taifa stars,suala la kuhujumiwa hili litakuharibia malengo yako mengi kwakuwa halina ukweli ndani yake,stars haikufanya vizuri tokea mwaka 1980 mimi sijazaliwa,mwl nyerere ni rais,wahujumu wapatikane leo miaka 34 baadae si kweli,miaka yote ya nyuma FAT ilikuwa malumbano na migongano amani imepatikana juzijuzi kwanini tusifikirie hapo,mipango endelevu ndio msingi wa maendeleo sehemu yote ile haya mambo siku hizi hayana nafasi.
5)Mwisho hiyo mipango uliyoeleza hapo wakati unamjibu mchangiaji ya kuanzisha vituo 25 vya michezo ambavyo nafikiri vitatilia mkazo soka la vijana ikianza chukueni ule ushauri ulio bora kutoka kwa yeyote iwe mwandishi au nani na acheni kuchanganyikiwa na maoni ya waandishi uchwara wa magazeti wengine wanastress za uchaguzi.
HONGERA KWA KAMATI BORA KABISA YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI,NI HAYO TU,HESHIMA KWAKO MKUU.
Last edited by a moderator: