Mkuu, vilabu hivi sasa vimebaki na sifa kuu tatu.Tunakushukuru sana kuwa karibu na jamii unayoitumikia. Kwa kweli soka letu linahitaji kuondokana na dhana ya usimba na uyanga
Jamal malinzi
Hiyo 5% unayosema mnataka iende kwenye mpango wa maendeleo ya soka la vijana kupitia tff ningewaelewa kama mngeweka kanuni ya kulazimisha vilabu kutumia 5% ya hizo pesa za udhamini kuwekeza kwenye timu zao za vijana na kuitaka bodi ya ligi kuhakikisha kunakua na ligi ya timu za vijana angalau ungeelewaka na familia ya soka lkn kwa huo mpango wenu mmefeli
Pole mkuu...tunaumia wengiKiukweli huyu JM anatuangusha sana sote tuliokuwa tunampigania achukue madaraka pale TFF, yaani tunaona AIBU sasa. Maana maswali ya waliokuwa wapinzani wetu ni kwamba "mnamuona mtu wenu?". Aisee najuta kuwa upande wa JM bora ningekuwa neutral TU.
20126!!!!!!!!! Halafu huyu ni raisi????!!!
acheni chuki binafs!!mbona mr presdent anamalengo ya mdamref!! hongera sana jamali malinzi mwanzoni nilikua nakuping ila baada ya kutoa huo ufafanuzi nimeelewa malengo yako!!.........
upuuzi mtupu....wizi...na utengenezaji mianya ya wizi na rushwa....ubabe na ukanjanja tu....nothing new....kama siasa tu
Hiyo 20126 ni nini??....
Kigogo, masikrodiga Kipaji Halisi Mjasiria Akili mwangalimungu Wa Kwilondo Masuke nguvu Mawenzi makoyo matale na wengine wote mliochangia hii mada,kwa niwashukuru kwa kuonyesha your concern kuhusu hii kanuni mpya ya mashindano:Naomba sasa niwafahamishe yafuatayo:
1.Kuibua,kukuza na kuendeleza vipaji ni gharama kubwa sana na zoezi hili ideally lilitakiwa lifanywe na vilabu vya madaraja yote kuanzia vya ligi kuu hadi madaraja ya chini.Unfortunately hili linafanyika kwa kiwango cha chini sana.
2.Wadau wa mpira hasa kupitia media wamekuwa wakidai mpira unaporomoka kwa kuwa hatujawekeza katika mpira wa vijana.Uwekezaji huu ni mkubwa kuanzia hatua za kuibua,kulea na kuendeleza vijana.Majuzi tumefanya program ya maboresho ya timu ya Taifa,vijana kumi na moja toka program hii leo wanacheza ligi kuu,bila shaka ni tumaini kuu la Taifa stars ya kesho
3.Mfuko wa kuendeleza soka la vijana vyanzo vyake havitakuwa fedha za TFF peke yake,sisi tunachofanya ni kuandaa mbegu (seed capital) baada ya hapo umma wa watanzania utahamasishwa kuchangia mfuko huu ambao utakuwa huru katika kujiendesha (hautaendeshwa na sekretariet ya TFF).
4.Program za vijana zinaanza mwaka huu hivyo hatuna muda wa kusubiri,mwaka huu kitaifa tutakusanya watoto umri chini ya miaka 12 na kuwahamishia kwenye Academy.lengo letu ni kuwa na timu imara umri chini ya miaka 17 mwaka 2019 ambapo Tanzania ita host fainali za Afrika umri chini ya miaka 17.Tunaamini program tuliyonayo itatufanya 2023 tucheze Afcon finals na tuingie fainali za world cup 20126.Hatuwezi kuongoza TFF bila malengo maalum.
Naomba suala la maendeleo ya mpira wa vijana tulitenge kabisa na siasa za mpira,mpira unahitaji fedha,mpira unahitaji sacrifice kwa wote wanaoutakia mema.
Baada ya kuyasema haya naamini tutashikamana pamoja katika kuinua mpira wetu.Muda wa kuongea kuhusu mpira wa vijana umekwisha sasa ni vitendo,katika hili TFF hatutarudi nyuma.
ahsanteni
Kumbe ndo maana anaharibu kabisa soka kwa sababu akili yake imejaa katerero, hujuma, wizi, udhulumati, unyang'anyi na ubabe usio na maana.
Ndugu Malinzi mnaweza kuwa mmefikiria sana na mkaona ni sahihi kuchukua fedha za udhamini kutoka kwenye vilabu lakini kama mtaamua kutumia nguvu bila kuwashawishi wahusika kwa hoja zenye nguvu mtaleta mgogoro ambao wadhamini wanaweza kuamua kujitoa au vilabu kuamua kuwa ligi yao ambayo haiko chini ya TFF wala CAF wala FIFA na bado vinaweza kupata washabiki pamoja na wadhamini ingawa mshindi hatacheza mashindano yoyote ya CAF.
Kama mnadhani ya kwamba program hiyo ni mwarobaini kwa soka letu ni bora mngetafuta namna nyingine ya kupata hela kwa ajili ya kuendesha hiyo program. Kuna mgawo wa makato ya gate collections kama vile Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu, Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, asilimia kumi mnayopewa na wadhamini wa ligi kuu, udhamini wa TBL (Kilimanjaro) kwa timu ya Taifa, tafuteni namna mchote huko.
Fuateni makampuni yawadhamini, yako mengi na kila mwaka yanatangaza faida kwa nini hizo faida msiende kuziomba japo kidogo, maana nimejaribu kukokotoa na nikapata kiasi cha kama milion 120 na kidogo ambazo mtazipata endapo mtafanikiwa lengo lenu kwa mwaka hizi hela japo kwa vilabu ni nyingi sana lakini kuna makampuni hiyo hela ni ndogo mno kuitoa yafuateni tu.
Kama mnaona kushawishi makampuni ni kazi kubwa basi ifuateni Serikali kupitia wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo si ndo kazi yake watenge hela huko kwa ajili ya maendeleo ya michezo kwa vijana wake, kwa nini mnataka vilabu vifanye kazi yenu au kazi ya wizara?
Nawashauri viongozi wa Yanga wajitoe katika hii move ya kudai haki ya vilabu ikiwa ni kisasi kwa kahaba mkuu SSC na mabinti zake, waliwasaliti Yanga katika udhamini wa Azam TV leo ndio wanazinduka kuibana TFF. Jamal Malinzi songa mbele, Alluta Continua! SSC et al., wanachuja mbu huku wakimeza ngamia, kama wako serious, tuanze na Azam TV waboreshe udhamin kwanza then Jamal Malinzi et al.
Jamal Malinzi:
Very nice words, typical of those of a conman (tapeli)! It is simply NOT the duty of tff to oversee youth development! It is the duty of clubs. You have done nothing to force clubs to have youth development programmes. PLEASE STOP IT!! IF YOU THINK YOU CANNOT LEAD TFF WITHOUT THE 5%, RESIGN!!!!