Malinzi,
Rejea mjadala kuhusu timu ya Taifa, mawazo yangu ni kama ifuatavyo
1) kwanza ili kujua ni mfumo au utaratibu gani tuufuate katika kuijenga timu yetu ya taifa, mimi nakuomba kwa kuwa umemteua mtu mfulani kuwa msaidizi au mshauri wako wa mambo ya mpira, hivyo natumaini huyu mtu analipwa na TFF. sasa huyu mtu nakuomba umpe kazi afanye utafiti yakinifu wa nchi zote za Taifa za Africa, ambazo timu zao zimekuwa na mafanikio. Aaandike ripoti na kuiwakilisha kwako, na wewe kama itawezekana uishushe hapa, hii itatusaidia kutupa mwanga na kujua ni mfumo upi tunaweza kutumia. Pia hapa unawezaq kupata watu ambao wanaweza kufanya kazi na huyu jamaa kwa kupeana malengo, nani ashughulikie nchi hii, na mwingine hii.
Tujiulize nchi kama Rwanda, Burkina farso, na Uganda mbona zimeweza kuwa na timu nzuri katika muda mfupi? Hata Zimbambwe , tumeona juzi walivyoweza kufanya vizuri achilia mbali Libya pamoja na matatizo yote.
2) Idadi ya wachezaji wa kigeni.
Hili swala ni kweli limeathiri kwa kiasi kikubwa nchi kama UK, lakini kwa upande mwingine hakuna ukweli, tujiulize ni tangu lini wachezaji wa kigeni wameanza kufurika kwenye timu za England? Na je kabla ya hapo timu ya Taifa za UK , na hasa England zimekuwa na mafanikio? Jibu utakuta si kweli. Tatizo la UK, na England per se, mfumo wa ufundishaji kutoka academy ni dhaifu mno, hebu tazama tu vipaji ambavyo huzalishwa na academy ya Ajax amsterdam ulinganishe na wachezaji wa Engaland, wengi wao ni media tu ndo imekuwa ikiwakuza.
Tukija kwa hapa kwetu, wachezaji hawa wa kigeni wameongeza saana ushindani na kuifanya ligi yetu kuwa kivutio hata kwa jirani zetu. Kitu kinachoweza kufanywa ni kuwa timu iruhusiwe kusajiri si zaidi ya wacheza 5, lakini uwanjani isichezeshe zaidi ya wachezaji watatu kwa wakati mmoja.