Maswali na ushauri kwa Malinzi

Maswali na ushauri kwa Malinzi

guti kabla ya kufikia maamuzi juu ya ni idadi gani ya wachezaji wa kigeni tuwaruhusu kusajiliwa na vilabu huwa tunakaa na vilabu vyote na kufanya kikao nao maana wao ndio wadau wakuu.Kikao cha mwisho tulikubaliana wawe watano tu.Jambo hili bado linaweza kujadilika.

Da yani hapo mheshimiwa tutakuwa wasindikizaji kwenye mashindano ya kimataifa mpaka dunia itaisha,hivi hatuoni hata kwa wenzetu afrika huko.mimi naamini virabu ndio vinaitangaza nchi kuliko timu ya taifa.
 
Last edited by a moderator:
Malinzi nimekuuliza kuhusu fdf naomba kujulishwa

Lakini naona sijibiwi

Philip Dominick FDF ni Football Development Fund.Huu ni mfuko maalum uliobuniwa na TFF ili uwe kiungo kati ya TFF na wadau katika kukusanya rasilimali za kuendesha program za mpira wa watoto,vijana na wanawake.Mfuko huu uanzishwaji wake umesimamiwa na Mwenyekiti mwanzilishi Leodegar Tenga,Katibu Henry Tandau na wajumbe Epbraim Mafuru,Mh Zarina Madabida,Mh Tarimba Abbas na Mwenyekiti mstaafu wa klabu ya Simba Mzee Ayoub Chamshama.
Mfuko huu utahamasisha wadau mbali mbali kuchangia maendeleo ya mpira wa vijana,wadau hawa ni pamoja na Serikali,Halmashauri,makampuni binafsi na ya umma,taasisi za dini nk

Kumbuka as it stands today timu yetu ya Twiga stars inayoondoka weekend kwenda Zambia haina support zaidi ya TFF,program za vijana kwa ajili ya fainali za Afrika umri chini ya miaka 17 mwaka 2017 na 2019 hazina support yoyote,hivyo kuna haja ya ku mobilise resources kwa ajili ya mipango endelevu kama hii.
 
Nashukuru sana kwa majibu mana nilipata ukakasi kuona pesa nyingi ya mapato mlangoni inaelekezwa fdf
 
Last edited by a moderator:
j malinzi hivi kwanini marefa wetu wengi wao mapolisi askari magereza wanajeshi na wenye vyeo vya chini kabisa mafundi umeme yaani ni waganga njaa huoni hili ni kuja kutafuta rushwa kwenye mpira?
 
RAIS kwenye shilikisho lako unaloliongoza wewe kuna baadhi ya dalili za rushwa kwa baadhi ya kamati hasa ya WAAMUZI umechukua hatua gani mpaka sasa.
 
Jamal Malinzi naona ktk tv channel ten..kuwa akaunti.za tff zimefungwa kisa hakulipa kodi za makocha wa kigeni walifundishaa taifa stars...
 
Last edited by a moderator:
RAIS kwenye shilikisho lako unaloliongoza wewe kuna baadhi ya dalili za rushwa kwa baadhi ya kamati hasa ya WAAMUZI umechukua hatua gani mpaka sasa.
Rais mbona hunijibu?
 
ikizu na wakimataifa matatizo ya refereeing ni gonjwa sugu.

Sababu zake kuu ni mbili,moja uwezo binafsi wa mwamuzi unaosababisha maamuzi ya kimakosa hii ni pamoja na mwamuzi kutokuwa na kasi ya kutosha kwendana mechi husika au kutokuwa na umakini wa kutosha lakini pili ni ukosefu wa maadili.Hili la pili ndilo janga la kitaifa ambalo sote tunapaswa kulipiga vita kwa nguvu zote.Mtandao wa rushwa mpirani ni lazima tuutokomeze.

Namba yangu ya simu ni 0754815543 napatika kwa simu,sms na whattsup.Email yangu ni president@tff.or.tz. Kama unaweza kunisaidia tukamnasa mtoa/mpokea rushwa rushwa mpirani utakuwa umetoa mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya mpira.

Naungana na wakimataifa kwa observation kuwa waamuzi wetu wengi ni walimu na askari wakati UEFA/FIFA unakuta baadhi ya waamuzi wao ni madaktari,wansheria na wasomi wengine wa aina hiyo (ingawa na masajinti wa polisi kina Howard Webb wamo).Katika hili ni vyema tuwashawishi wasomi nao wachukue taaluma hii na tutawatia moyo kwa kuondoa fujo viwanjani na kuongeza posho kwa waamuzi.
 
Jamal Malinzi .

Vijana WA Maboresho watatumia jezi zipi dhidi ya Malawi....?

Vipi kuhusu jezi za timu ya taifa ....ulituambia imepatikana muda mrefu sasa.Zoezi tangu November...

Tupatie kauli ya uhakika kutoka Ofisini kwako juu ya huu mchakato huu unaositasita.Ili tu tujue ni lini itawekwa hadharani....!
 
Last edited by a moderator:
kwanza awapokonye simba point 3 apewe prison kwa kumchezesha ajibu alikuwa na kadi 3 za njano ndio tutajua kama kuna TFF
 
Jamal Malinzi .

Vijana WA Maboresho watatumia jezi zipi dhidi ya Malawi....?

Vipi kuhusu jezi za timu ya taifa ....ulituambia imepatikana muda mrefu sasa.Zoezi tangu November...

Tupatie kauli ya uhakika kutoka Ofisini kwako juu ya huu mchakato huu unaositasita.Ili tu tujue ni lini itawekwa hadharani....!

DemiGod la jezi mpya limekamilika,subiri tukio la uzinduzi soon
 
Last edited by a moderator:
Rais wakati wa sakata la mashine za electronic likichukua kasi juu ya wizi uliokuwa unafanyika msimamizi wa mbeya,tanga, mororogoro na kagera walilalamika sana lakini kwa upande wa Dar es salaam alikuwa anasifia huo mfumo mimi mpaka leo sijajua nini kilikuwa nyuma ya pazia kwa huyu jamaa.
Rais nini kinaendelea kwa huyu mtu mbali na hatua zilizochukuliwa na serikali kwa upande wako?
 
J malinzi nakuuliza ratiba ya vpl haieleweki
pili hata ukipitia mtandao wa tff vpl haionyeshi
tatu baada ya kulalamikiwa mtandao wa tff ulisema utafatilia mbona hatuoni kitu
 
mkuu muwe mnaupdate website yenu. mnatia aibu. ni chanzo cha mapato kile ujue!?
 
Jamal Malinzi.
Pole kwa majukumu.
Kuna suala ambalo linanishangaza sana hasa suala la takwimu. Huwa najaribu walau kufuatilia ni mchezaji gani ambae amecheza mechi nyingi zaidi (most caps) katika timu ya Taifa mpaka leo sijui. Pia nani aliyefunga magoli mengi zaidi (most goal scorer) pia nalo sijui. Ni kwanini inakuwa hivyo. Kuna baadhi ya wachezaji wao hucheza kwa bidii ili kuvunja record fulani. Je kwa hili unasemaje? maana naami japo wewe ni Rais wa TFF huenda hata hujui hayo.
 
SaaMbovu TFF tayari tumeajiri mtu maalum wa kusimamia ukurasa wa "archive" kwenye tovuti mpya ya TFF ambayo ipo kwenye hatua za ujenzi.Ikikamilika na kuzinduliwa utaona mabadiliko.
 
J malinzi tunaomba hawa marefarii wa vpl wawe waangalifu kutoumizwa wachezaji ambao kwa sasa wanashiriki mechi za kimataifa yanga inabidi itolewe onyo kwao na timu zinazocheza wote
 
Kwako raisi wetu!
Vipi kuhusu tatizo la kusaka vipaji has a ktk mikoa isiyo na timu VPL? Natoa mfano wa mikoa kama Iringa na Kigoma, huko kuna vipaji lakini TFF haiviangalii. Je, TFF ina mkakati gani endelevu Lusaka vipaji huko na kuwainua vijana wa kitanzania?
 
Back
Top Bottom