huyu muhaya huyu anapenda sana show off
Malinzi,
Rejea mjadala kuhusu timu ya Taifa, mawazo yangu ni kama ifuatavyo
1) kwanza ili kujua ni mfumo au utaratibu gani tuufuate katika kuijenga timu yetu ya taifa, mimi nakuomba kwa kuwa umemteua mtu mfulani kuwa msaidizi au mshauri wako wa mambo ya mpira, hivyo natumaini huyu mtu analipwa na TFF. sasa huyu mtu nakuomba umpe kazi afanye utafiti yakinifu wa nchi zote za Taifa za Africa, ambazo timu zao zimekuwa na mafanikio. Aaandike ripoti na kuiwakilisha kwako, na wewe kama itawezekana uishushe hapa, hii itatusaidia kutupa mwanga na kujua ni mfumo upi tunaweza kutumia. Pia hapa unawezaq kupata watu ambao wanaweza kufanya kazi na huyu jamaa kwa kupeana malengo, nani ashughulikie nchi hii, na mwingine hii.
Tujiulize nchi kama Rwanda, Burkina farso, na Uganda mbona zimeweza kuwa na timu nzuri katika muda mfupi? Hata Zimbambwe , tumeona juzi walivyoweza kufanya vizuri achilia mbali Libya pamoja na matatizo yote.
2) Idadi ya wachezaji wa kigeni.
Hili swala ni kweli limeathiri kwa kiasi kikubwa nchi kama UK, lakini kwa upande mwingine hakuna ukweli, tujiulize ni tangu lini wachezaji wa kigeni wameanza kufurika kwenye timu za England? Na je kabla ya hapo timu ya Taifa za UK , na hasa England zimekuwa na mafanikio? Jibu utakuta si kweli. Tatizo la UK, na England per se, mfumo wa ufundishaji kutoka academy ni dhaifu mno, hebu tazama tu vipaji ambavyo huzalishwa na academy ya Ajax amsterdam ulinganishe na wachezaji wa Engaland, wengi wao ni media tu ndo imekuwa ikiwakuza.
Tukija kwa hapa kwetu, wachezaji hawa wa kigeni wameongeza saana ushindani na kuifanya ligi yetu kuwa kivutio hata kwa jirani zetu. Kitu kinachoweza kufanywa ni kuwa timu iruhusiwe kusajiri si zaidi ya wacheza 5, lakini uwanjani isichezeshe zaidi ya wachezaji watatu kwa wakati mmoja.
MKUU MALINZI
VIPI KUHUSU ITC YA GEORGE MTEMAHANJI tangu mwaka jana mpaka leo kimya ameshindwa kujiunga na timu na kuanza kucheza mpira ITALY na USWISSI, Vipi mkuu au ndio mpaka ailipie hapo TFF ndio atapewa ITC
Ni kweli,ukipanua ligi ghafla ubora wa ligi kwa maana ya ushindani nao utashuka ghafla,ni jambo la kwenda kwa hatua.Jamal Malinzi
kwahili twende taratibu,
tuongeze zifike 16 then 18 then 20. na sio haraka haraka.
pia isije ikawa mambo ya kuwa mwaka huu hakuna kushuka daraja, hatutaki kusikia hili ni bora kuboresha ligi daraja la kwanza na kuhakikisha badala ya kupanda watu wawili wapande wanne lakini kushuka wawili kila mwaka ni lazima.
Tumeamua kuanza na fainali za afrika wavulana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019,hii itatupa uzoefu wa kuandaa mashindano makubwa zaidi.Rwanda nao walianza na under 17 sasa 2016 wananda CHANTutaandaa lini mashindano haya
1.CHAN
2.Mataifa ya Africa(Africon)
3.Kombe la mataifa ya Africa kwa vijana
--------------------------------------------------------
1.Mataifa ya Africa kwa wanawake
-Wakubwa
-Vijana(wasichana)
Au tuombe kuandaa kombe la dunia la akina mama
kwamekwax naomba details zozote kuhusu hii ITC ili nifuatilie,nitumie kwa email jamalmalinzi@yahoo.com
Tumeamua kuanza na fainali za afrika wavulana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019,hii itatupa uzoefu wa kuandaa mashindano makubwa zaidi.Rwanda nao walianza na under 17 sasa 2016 wananda CHAN
Yombayomba umejenga hoja nzurisana kuhusu umuhimu wa timu za majeshi kwa mustakabali wa mpira wetu.FIFA club licencing regulations na tuliambiwa lazima iwe kwenye katiba zetu na tulifanya hivyo.Hii kanuni kama ulivyosema inapiga marufuku umiliki wa timu zaidi ya moja kwa mmiliki mmoja.Jambo hili mimi naona ni la kisheria,vyema kamati yetu ya sheria kwa kushirikiana na wadau wengine ikaliangalia kwa kina.
Wazo la kuleta marefa wa nje yanga vs simba ni la siku nyingi,ngoja tuzidi kulifanyia kazi.Lakini je lazima wawe wazungu?
JM kwanini Azam hawaruhusiwi kutumia uwanja Wa chamaz wanapocheza na simba na yanga?hii c saw a kabisa..
Uundwaji wa kamati kumi na saba za TFF ni kwa mujibu na agizo la katiba ya TFF.Mkuu Habari
Mkuu malizni nimeona tff imetoa kamati na majina ya wajumbe ok ni sawa
Il mbona naona kamati za tff zimekuwa nyingi na wajumbe wa hizo kamati wengi . hii uoni kama inakuwa mzigo mkubwa kwa tff hasa kwenye malipo ya wajumbe kwenye vikao na shughuli zingine uoni umuhimu wa kupunguza kamati au na idadi ya wajumbe kwenye kila kamati
Uundwaji wa kamati kumi na saba za TFF ni kwa mujibu na agizo la katiba ya TFF.
Wenye mamlaka ya kubadili utaratibu huu ni mkutano mkuu wa TFF.