Umekuja na matusi na si kujenga hoja? Kimekukera nini, as long as sheria inamruhusu sioni tatizo kugombea mkoa!
He is good upstairs! Alisoma Chemical and Processing engineering UDSM---80's, (miaka hiyo university iko moja) akitokea Ilboru shule ya vipaji.
Then West Germany (before unification) akasoma Masters field hiyo hiyo. Hivyo yuko vizuri kichwani.
Elimu ya mpira ni tofauti na ile ya darasani mkuu.
Huyu jamaa simtetei kwani naelewa anayo mapungufu yake lakini si sawa mkajifanya vipofu msioona kila kitu.
Tunaofatilia historia ya mpira hasa toka enzi za akina Mwidini Ndoranga na Michael Wambura wakiwa FAT enzi hizo mpaka ikaja kuitwa TFF chini ya L. Tenga na sasa chini ya J. Malinzi tunayo mengi ya kuongea.
Ni vizuri ikaeleweka kwamba mpira wa Tz ni jambo la kihistoria na nyakati zaidi kuliko uhalisia. Ni vizuri tukajua kiwango cha mpira wetu miaka ya 80's, 90's na kuendelea. Mpira wetu huwa unapanda na kushuka kutegemeana na mambo lukuki. Mfano, nakumbuka hata Tenga akiondoka kuna watu waliibuka na kusema jamaa kakomba pesa zote kanunua Benz na majumba kibao ya kifahari, kisa kapiga TFF.
Alichokifanya Tenga na anachokifanya Malinzi ni falsafa mbili tofauti katika soka letu, na mafanikio ya enzi za Tenga yana sababu zake nje ya Tenga kama ilivyo kwa Malinzi pia. Binafsi siwezi kusema timu ya Taifa kufanya vizuri 2006-2010 eti ilikuwa ni kwasababu ya TFF, siyo kweli. Na siwezi kuongelea ubora wa kipindi hicho na nisiwahusishe watu kama J. Kikwete, M. Maximo na B.Mkapa. Ukiwa na rais mpenzi wa michezo no.1, mkawa na kocha mwenye karisma kama Maximo, mkawa na uwanja mkubwa mpya kwa mara ya kwanza, mkawa na kocha mwenye kupewa kila anachokihitaji na mshahara mzuri kutoka kwa raisi wa nchi, mkawa na timu inayowezeshwa kwa safari, majaribio na vifaa, mkawa na rais anayehudhuria uwanjani kila mechi uwanjani halafu bado mwisho wa siku mpira usionekane, haiwezekani bwana. Na hili halihitaji ama kuwepo Malinzi wala Tenga.
Na ni muhimu tukakumbuka pia, kwamba 70% ya timu yetu uendeshaji wake uliitegemea serikali kwa vitu vingi sana, sasa mnapata wapi nguvu za kuisifia TFF, na kwa lipi? TFF inabaki na kazi ndogo sana ambazo mtu yeyote hata ningekuwa mie ningeweza kuongoza na mkanisifia sana, huu ndo ukweli na haina mbadala, TFF ilibaki ceremonially.
Sasa hebu tujuzane baada ya serikali kusema inasitisha kuendelea kumlipa Maximo (2009) na TFF wakasema hawawezi, bado ilibidi serikali imuhudumie kocha kwa mkataba wake wote (miaka3) mpaka ukaisha. Baada ya serikali kukabidhi majukumu kwa TFF tokea 2010 ni kitu gani kilisalia kwenye mpira wetu, onesheni ni mafanikio yapi yaliendelea kuwepo? Shamra shamra za watu mtaani juu ya timu yao zilionekana tena? Ile hari ya kila mtu kwenda uwanjani na vibendera mikononi na tshirt zao za timu yetu zilikuwepo tena? Kipindi hicho Malinzi alikuwepo tayari, kipindi hicho TFF haikuwepo, kwanini mambo yalianza kuzorota? Mie nafikiri tutumie mda huu tutafakari, tuelewe kila kitu na nyakati na historia yake.
Leo TFF inapata msaada hupi kutoka serikalini, leo kocha analipwa sh. ngapi, na nani? Ukimwangalia JPM ana ushawishi kiasi gani kwenye michezo kumlinganisha na JK!!!, na bado hamuelewi tu?
Ni vyema tufahamu, michezo ni jambo pana sana, ni mipango na hamasa, full stop. Nimalize tu kwa kuyatambua madhaifu ya TFF leo lakini si vibaya pia kuwapongeza kwa baadhi ya mambo kama vile kutengeneza utaratibu wa baadae wa kuinua michezo. Naamini kwa kuanzishwa ligi ya akina dada na leo iko vizuri A.Mash., kuwepo kwa ligi ya U.17, 20, kuwepo na academies ipo siku tutaelewa ni kwanini tunatakiwa kuanzia huko chini kama kweli tunataka siku moja kupata maendeleo ya mpira. Popote duniani, ni lazima mpira uanzie chini na watu waandaliwe, hakuna mafanikio ya over night katika soka. Lakini mbali ya hilo, naona vijana wakiingia katika ulimwengu wa ajira kupitia michezo pia.
Mwisho kabisa, ni vizuri penye ukweli usemwe wazi na si kila kitu kuvamia kwa kufata mkumbo. Mpira hauitaji siasa kama za kwenye majukwaa ya wanasiasa na mpira usipelekwe huko kamwe. Wenye kufahamu mpira wapewe nafasi waongelee mpira wetu.
Yangu ndo hayo kwa mwaka huu 2017.