Maswali na ushauri kwa Malinzi

Mr President J. Malinzi,

Naomba nikurudishe tena kwa swala la OKWI, hili swala hatimaye leo limefikiwa tamati, lakini ili kulinda heshima na utendaji uliotukuka wa taasisi unayoiongoza kama raisi nadhani kuna umuhimu utolee ufafanunuzi swala hili. Kuna maswali yafuatayo kuhusu swala hili:

1) Ni kitu gani na kilichofanya TFF imsimamishe OKWI wakati tayari alikuwa amepata ICT?
a) Je kuna ICT za kuchonga au za mchoro?
b) Je kumepata kutokea ICT imetolewa kimakosa? naomba mfano

2) Kama chama cha soka cha Uganda, kilithibitisha , ni kitu gani kimewafanya musiwaamini?
3) Ni kipengele gani na ni nani aliyeleta pingamizi?

Naomba utufafanulie, nadhani kwa kuwa kimeeleweka sheria hazitakuzuia kutoa ukweli juu ya hili
 

Hon. Jamal Malinzi, wana JF na Watanzania wa ujumla wanasubiri majibu kwa maswali haya. Ni vyema suala la Okwi ukalitolea ufafanuzi katika vyombo vya habari kwa mfumo wa Press Conference ili kuondoa dhana iliyojengeka miongoni mwetu kuwa TFF hawakumtendea haki Okwi na timu ya Yanga kwa kumzuia kucheza huku akiwa na ITC.
 
Mr President Malinzi,

Samahani kwa kukuchosha kwani najua una mambo mengi kulijenga soka letu na kusafisha nyumba (TFF). Nimesoma kuwa umetangaza kuwa mashindano ya Taaifa Cup yanaanza kutimua vumbi Feb 22, kusaka wachezaji wa timu ya taifa. Napata tatizo,

1) Hivi kweli tayari mikoa imejiandaa hata kuendesha hayo mashindano mikoani kusaka timu ya mkoa? I mean kutafuta kombaini ya wilaya hatimaye kombaini ya mkoa.
2) Je league zitasimama? kama hapana vipi hawa wachezaji walioko kwenye hizi timu?

Timu huchaguliwa na mwalimu atakayeifundisha, na mchezaji hachaguliwi kwa mashindano mamoja, vipi kwa wale ambao watatolewa round ya kwanza? utajuaje kipaji chake?

Kwa nini TFF, isifunje kwanza benchi zima la ufundi na kusuka jipya na kumpa uhurtu mwalimu asake wachezaji nchi nzima taratibu?

Tusifanye haraka, bbadala ya kujenga kuna hatari tukaiua kabisa timu ya taifa.
 

Ikiwezekana wachezaji wa kigeni wawe hata timu nzima. Wachezaji wa kitanzania wana tatizo la kutoheshimu vipaji vyao kama chanzo cha ajira (mfano uchezaji wa ndonndo), kudhibiti wachezaji wa kigeni kunafanya iwe rahisi kwa mchezaji wa hovyo tu kuwepo katika ligi kuu na hivyo kupelekea kuwa na timu ya taifa dhaifu.

Mapendekezo yangu kusiwe na ukomo wa wachezaji wa kigeni ili kuwapa hamasa ya kujituma wachezaji wa ndani...
 
Last edited by a moderator:

Ahsante mkuu.

Hoja yangu inahusu namna TFF inavyoweza kuongeza mapato yake kupitia mauzo ya jezi za timu ya taifa. Pengine watu waliopo ndani ya TFF wanafahamu hili lakini wamejitoa fahamu labda kwa kuwa wananaufaika na utaratibu uliopo. Timu za Taifa zinatumia jezi na vifaa vya UHLSports, lakini haiko wazi kama shirikisho lina mkataba wowote na kampuni hiyo na hupata faida kiasi gani kutokana na mauzo ya jezi kwa washabiki, kuna usiri ambao unatia shaka.

Timu ya taifa ni timu ambayo inashabikiwa na watu wote, wakati mwingine na hata watu wasio wapenzi sana wa soka kwa hiyo nafasi yake ya kuuza jezi ni kubwa kuliko klabu yoyote hapa nchini, uzoefu kidogo hesabu zangu fupi zinaniambia kuwa TFF inaweza kuuza nakala milioni moja za jezi kwa mwaka (NDIO, MILIONI MOJA NCHI NZIMA), kwa faida ya Sh. 1000/= (naamini itakuwa ni zaiidi ya hapo) kunaweza kupatikana zaidi ya Tsh. Bilioni moja kwa shirikisho. Hili litawezekana kama kutakuwa na uwazi, pamoja na mikakati ya kweli ya kuboresha mapato ya shirikisho.

Huo ni mfano wa karibu na haraka ambao nimeweza kufikiria, lakini idara ya masoko ya shirikisho inawezaa kukaa na kuja na miradi kadhaa ambayo italifanya shirikisho kuwa na mapato yake lenyewe na kuacha kunyonya bajeti ya serikali.

Ahsante tena, hoja yangu si lazima ijibiwe.
 
Last edited by a moderator:
mr. TFF. President

hoja yangu inahusu kombe hl la vijana wa chini ya miaka 17 almaarufu kama (COPA COCACOLA)
idad kubwa ya vjana wanaoshiriki kombe hili na wana vipaj asili

Ila idadi ndogo ya vijana ndio huchukuliwa na timu zenye uwezo wa kuchukua watoto na kuwalea kama AZAM F.C NA SIMBA SC ambazo kdogo hujtahd kufanya hvyo.....
Je? Msaada gan hutoa TFF ili kusaidia kuhfadh wachezaj wa baadae
KWANI WENG HUISHIA KUCHEZA MCHANGANI NA WANA UWEZO MKUBWA KATIKA SOKA....
 

Tunakwenda hatua kwa hatua,ngoja tuanze na kuandaa fainali za afrika vijana umri chini ya 17
 

nakuelewa sana,lakini wengi wao bado wana la kuchangia kwa maendeleo ya mpira wetu,tusiwatupe.
 

Yombayomba klabu ya Yanga tumewapa nakala halisi ya barua ya FIFA waisome wenyewe,ina neno "without prejudice".
 
Last edited by a moderator:

ITC sio kigezo pekee cha kumruhusu mchezaji kucheza.Yanga tumewapa nakala halisi ya barua ya FIFA.Wakiisoma wataelewa kwa nini Okwi tulimzuia asicheze.Kama ni maelezo ya ziada acha wayatoe wao Yanga.
 

Tumetafakari sana juu ya jambo hili,hatua tuliyochukua ni ya dharura (crash programme) kwa ajili ya mashindano ya mwaka huu.Hatujavunja timu ya Taifa tunaiboresha.Kwa mashindano ya baadae kuanzia 2015 tutajipanga zaidi.Benchi la ufundi linafanyiwa kazi.
 

Mphamvu TFF haina mkataba wa aina yoyote na brand ya uhlsport.
Tunajipanga tuone ni kwa jinsi gani tutauza replica shirts za national team,lakini kwanza tutai design upya.
 
Last edited by a moderator:

MANI MISIMBO kwanza lazima tuandae data base ya vijana wetu nchi nzima ili iwe rahisi kuwafuatilia.
 
Last edited by a moderator:
Yombayomba klabu ya Yanga tumewapa nakala halisi ya barua ya FIFA waisome wenyewe,ina neno "without prejudice".

Mr President,

Nashukuru kunijibu, lakini kwa faida na maendeleo ya soka la Tanzania, nadhani mtakuwa hamjawatendea haki watanzania na wana Yanga. TFF, ndo muliwasiliana na FIFA, hivyo ni jukumu lenu kupitia wanasheria wenu kuitafisri hiyo barua, au kuomba waifafanue vizuri zaidi watu wa FIFA.

Ingekuwa Yanga wamewasiliana moja kwa moja na FIFA, nisingekukuomba utafute ufafanuzi. Kwani kwa mtu wa kawaida, atajua kuwa TFF, mmeshindwa kuielewa barua na mmeutua mzigo kinamna, ambao mliuchukua katika mazingira ya kutatanisha.

Nasema kutatanisha ni kwa sababu, huwezi kumzuia mtu kabla ya siku mbili, wakati amewasilisha nakala zinazotakiwa mapema kabisa.

TFF, inatakiwa iwasiliane na FUFA, na CUF, ndio maana niliorodhesha hayo maswali,. ambayo ungeyajibu moja baada ya lingine watanzania wengi tungeelimika.

Samahani kama nimekukweza
 

Mr President,
Nimekusikia, naomba nikukumbushe kitu kimoja, fatilia wote ambao timu zao zimepata kupita katika wakati mgumu, nini walifanya? mfano wa jirani wa karibu Zambia, nakuachia msaidizi na mshauri wako wa karibu alifanyie utafiti.

Tunatakiwa tuivunje timu yetu, na kocha aunde timu mpya kabisa, kwa kujipanga siyo kufurahisha kikundi fulani. Huu mfumo mliochukua, kwa hali ya uchumi wa sasa wa nchi yetu, usishangae watu wanaomba walipwe pesa ili amchangue kuingia kwenye hii timu. Time will tell you.
 

Mjadala wa Okwi TFF tusingependa uendelee,tulipofikia panatosha.Mengine yanabakia kwetu.
 
Sipendi kudhania hivyo.Ingawa sifahamu shughuli zako ni zipi ninakuomba na wewe ufuatilie mechi hizi,utakalo li observe nifahamishe kupitia 0754815543 au jamalmalinzi@yahoo.com
 
Hon. Jamal Malinzi naomba nikupongeze kwa jinsi unavyotenga muda kujibu maswali ya Wakuu hapa jamvini. Endelea na moyo huo wa kiungwana na Mungu akubariki ufanikiwe zaidi katika kazi zako zote.
 
Last edited by a moderator:
Huyu ni president wa kuigwa,unatenga muda kujadili na wadau,umechukua hatua kutaka kulinusuru taifa kuwa kichwa cha mwandawazimu,hata kama ukifeli kwenye crash programe sio mbaya umeonesha njia umeplay part yako kilichobaki ni wachezaji na kocha wao,big up,wenye majungu weka pembeni,halafu swala la watunza kumbukumbu sijui kama ofisi yako inawatu wa masijala,mh hawa watu ni muhimu ktk kila taasisi ushauri tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…