Maswali na ushauri kwa Malinzi

Mkuu dfk kadito mawakala wanaotambulika na fifa toka tanzania ndio hao hao hata mi nimeona majina hayo hayo kwenye mtandao wa fifa
Nimeona kwenye website ndio. Ila kuna mawakala wawili kutoka Tanzania wamewasiliana nami wakisema wako chini ya TFF, lakini siwaoni majina yao (mwingine anaishi nchi jirani). Hili ni swali muhimu kwasababu uongo huu unawaletea matatizo vijana wengi sana. Kuna mawakala wengine wanawakamua vijana walipe hela ili wawasadie. These things need to be transparent.

Mwaka jana kuna watu walituma barua TFF wakijifanya ni maWakala wa Thailand wana ushirikiano na Liverpool. TFF wakatangaza vijana wachangamkie deal. Kukawa na sign of fee hao watu inabidi walipwe. Kuna mzazi mmoja akanifuata akaniambia, kwanini usimpeleke huyu kijana Thailand. Nikamsikitikia sana. Nikamwambia, kwanza mpira wao uko chini kama TZ tu. Pili, wakala anayekuomba hela aprocess mambo ya usafiri ni mwizi. Tatu, kwanini upitie Thailand ili ufike Liverpool? Yule mzazi aliona kama nambania. Baada ya wiki 2 hivi, TFF wakatangaza kwamba hao jamaa ni wasanii.

Kwahiyo, mwache bwana Malinzi ajibu, inawezekana wapo wengine ila tovuti ya FIFA haiko updated.
 
Habari mkuu nimekuelewa

Kuna jambo moja niliwahi kuliskia ile tff iliyopita ikisema au kuliongelea pia nitaomba angalau maelezo yako kutokana na uzoefu wako '' ile TFF nakumbuka na nilishawahi kuwanukuu walisema kuwa leseni za uwakala FIFA inatakiwa kila baada ya miaka fulani im not sure kama kila baada ya miaka mi3 au m4 wanatakiwa mawakala kufanya tena mtihani kama wanataka kuendelea na leseni zao pia im not sure kama hii ni kwa nchi zilizochini kidogo kama tanzania au duniani kote kwa ujumla, hili mkuu nina uhakika nalo kwani nilishwahi kuwanukuu wakisema hivyo, mara ya mwisho niliwahi kucheki hiyo website ya fifa na majina yalikuwepo toka tanzania walikuwa ni Damas Ndumbaro huyu ni wakili nazani, Hamid Bakhressa, Mehdi Remtullah na huyo bwana John ndumbalo nakumbuka leseni amepata kama mwaka mmoja na nusu au miwili iliyopita kwa kumbukumbu zangu sasa yawezekana hayo majina ya wengine hayapo kwenye website ya fifa labda hawakufanya mtihani wa kuendelea kumiliki leseni zao kama walivyowahi kusema tff, mkuu kwa hili sina hakika sana labda kama unaweza kutufafanulia kutokana na udhoefu wako na ufahamu wa mambo haya

Otherwise kazi njema

nb. mkuu kule kwenye THREAD yako tunasubiri kusikia toka kwako umetukimbia kidogo



 
1.Team yetu ya Taifa iliyo teuliwa jana kwenda kucheza soka Namibia imeteuliwa na nani?
2.Kwa nn mnamuingilia kwenye kazi yake Kocha Paulsen aliye na mkataba hai na TFF?
3.Upo tayari kuvunja mkataba na kumlipa fidia kocha huyu?
4.Mchezaji Mduma wa Mwanza kachaguliwa kwa vigezo gani?

Nasubiri majibu tafadhali
 

Kweli kbs Jamal malinzi tunahitaji majibu kama ni kweli tff ndio imeteuwa hii timu naanza kupoteza imani na uongoz wako...
 

Malafyale,aliyeteua kikosi cha kwenda Namibia ni kocha mwenye leseni class A ya CAF.
Sababu za kisheria haziruhusu TFF kuongelea mkataba wa mwalimu Kim.
Kesho saa nne asubuhi nitaongea na media kuhusu TAIFA Stars technical bench.
 
Last edited by a moderator:
Malafyale,aliyeteua kikosi cha kwenda Namibia ni kocha mwenye leseni class A ya CAF.
Sababu za kisheria haziruhusu TFF kuongelea mkataba wa mwalimu Kim.
Kesho saa nne asubuhi nitaongea na media kuhusu TAIFA Stars technical bench.

Majibu yako as usual ni mepesi mepesi sana kiongozi Malinzi
1.Huyo kocha mwenye leseni grade A aliyeiteua hii team hana jina?Mbona kiongozi wa TFF alipo ongea na media alibabaika kusema haya unayotuambia hapa?
2.Safari yako ya Mwanza hivi karibuni ndiyo imetuletea huyu mchezaji wa mtaani toka Mwanza?
 
Last edited by a moderator:

Malafyale nilipofungua hii thread nia yangu haikuwa kuanzisha uwanja wa malumbano.
Huyu mtoto unayemponda ushawahi kumwona anacheza?Kwa taarifa yako Airtel rising star africa finals Nigeria last year alikuwa ndiye top scorer na ni left footed.
 
Last edited by a moderator:
Malafyale nilipofungua hii thread nia yangu haikuwa kuanzisha uwanja wa malumbano.
Huyu mtoto unayemponda ushawahi kumwona anacheza?Kwa taarifa yako Airtel rising star africa finals Nigeria last year alikuwa ndiye top scorer na ni left footed.

Swali la msingi hapa halijajibiwa na labda ninyambulishe kama ifuatavyo:
Huyo kijana unayedai ni talented kaonwa na kocha gani?
Je kocha aliyeteua team hii ndiyo kamleta kijana huyu left footed?Kocha huyu ni nani?
Unapo ongea na media kesho upo tayari kutaja aliye teua team hii?
 
Last edited by a moderator:
Malafyale nilipofungua hii thread nia yangu haikuwa kuanzisha uwanja wa malumbano.
Huyu mtoto unayemponda ushawahi kumwona anacheza?Kwa taarifa yako Airtel rising star africa finals Nigeria last year alikuwa ndiye top scorer na ni left footed.

Jamal hakuna anayetaka malumbano hapa jibu hoja..Huyo kocha hana jina? Kwann hutak kumtaja?acheni ubabaishaji bana tulianza kuona Mwanga ila naona unataka kuturudisha enzi za kina ndolanga....
 
Last edited by a moderator:
Kim umeshamtimua eeeh!
Haya tuletee kocha atakayepaisha soka letu.
 
Malinzi tuambie kilichojiri kuhusu kim poulsen maana ulisema saa tatu asubuhi tutapata taarifa
 
Malinzi tuambie kilichojiri kuhusu kim poulsen maana ulisema saa tatu asubuhi tutapata taarifa

Mwalimu Kim tumefanya mashauri ya pamoja na kukubaliana asiendelee kuwa kocha wa timu yetu ya Taifa.Mwalimu mpya atatangazwa siku chache zijazo.
 
Mkuu Malinzi Habari yako

Ok kuhusu huyo bwana mdogo wa copa coca cola hamuoni kwamba ingesahihi kwake kuitwa kwenye timu ya taifa ya vijana kani huko ndio ingekuwa kwake rahisi kucheza mechi nyingi zinazohusisha hiyo timu kuliko kwa umri wake kumpeleka moja kwa moja timu ya wakubwa , hapo kwa wakubwa nazani hata nafasi yeye kucheza mechi za starz itakuwa finyu , kuna maana gani kuwa na itmu ya vijana ya taifa

mkuu nimeona umesema kuwa kocha mpya target ni AFCON 2015 hivi mkuu kweli inawezekana maandalizi ya michuano ya mwaka kesho tunaandaa timu mwaka huu huoni kama itakuwa yaleyale tunarudi kule kule inawezekana kweli kuandaa timu ya kufanya vizuri ndani ya kiezi isiyopungua 10


Mwalimu Kim tumefanya mashauri ya pamoja na kukubaliana asiendelee kuwa kocha wa timu yetu ya Taifa.Mwalimu mpya atatangazwa siku chache zijazo.
 

sio mbaya kuitwa starz na si lazima acheze kuwa pale yeye ni kujifunza vitu vingi.. Na kuitwa starz hakumfanyi ashindwe kuitwa timu za vijana.. Nadhani unakumbuka theo walcot 2006 aliitwa wordcup ikiwa hata hajawai kuitwa timu za vijana, lakin taratibu akaitwa U20. Kwahyo tambua kuitwa direct national team haikuzuii kuitwa tim za vijana
 

well said Rockcity native thanks
 
Last edited by a moderator:
Naona muda si mrefu boss atasign-OUT,

Upepo unaelekea tofauti na alipo yy!
Maswali magumu, majibu mepesiii kama karatasi!

#Inaboa sana!
 
Mh.Malinzi naomba niambie ni sbb gani za msingi zimesababisha TFF kuvunja mkataba na Kim,kwa makubaliano ya siri na sio ya uwazi?au kwasbb Kim alikuwa kipindi cha Mh.Tenga,na wewe unataka utafute wa kwako?Huoni kwamba huu ni ubinafsi?Pia,huoni kwamba 'taifa stars'ikibolongo lawama ni zako?Mwisho,napenda kukushauri kwamba hebu jitahidi kuyaheshimu mambo mazuri uliyoyakuta chini ya Mh.Tenga,kamwe usijifanye mjuaji yasije yakakukuta ya kosha David moyes,usione haya kuomba ushauri kwa Mh.Tenga ili nawe ukumbukwe kama mwenzio.Kazi njema Mh.
 
Kim Kwa Mtazamo Wangu, Binafsi Namuunga Mkono Malinzi Na Body Yake, Kwa Kumfuta Kazi!! Kwani Uwezo Wake Umeishia Hapo Alipotufikisha!! Ila Ushauri Wangu, Waendelee Na Zile Program Za Soka La Vijana Na Wtt Wadogo!! Ndio Suluhu Yake!! Tuwekeze Huko Nguvu Zote!! Tuachane Na Haya Majina Makubwa Waliolewa Sifa Za Usupasta!!! Pia Ligi Yetu Iongezewe Ushindani, Kwa Kuongeza Idadi Ya Timu Shindani, Sio Washiriki Tu!! Kusiwepo Na Kusimama Kwa Ligi Miezi 3, Huku Hakuna Mashindano Yoyote Yale!!
 
Mwalimu Kim tuliamua kukatiza mkataba kwa sababu za msingi tu. Bahati mbaya watanzania wengi hawajui kuwa hata aliyemtangulia Kim yaani kocha Jan Poulsen naye mkataba wake ulisitishwa na alilipwa fidia,the only difference ni kuwa tumeamua kuwa wawazi katika hili. Kuhusu sababu za kukatisha mkataba na Kim sio vizuri kumjadili mtu ambaye hawezi kuja hapa kujitetea. Kaka yangu Tenga ninakutana naye mara nyingi na tunaongea mengi kwa maendeleo ya mpira wetu.Kila nikitatizwanna jambo huwa ninamtafuta na ana msaada mkubwa sana kwangu,ninamshukuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…