dfk-agent
Senior Member
- Aug 5, 2013
- 131
- 163
Nimeona kwenye website ndio. Ila kuna mawakala wawili kutoka Tanzania wamewasiliana nami wakisema wako chini ya TFF, lakini siwaoni majina yao (mwingine anaishi nchi jirani). Hili ni swali muhimu kwasababu uongo huu unawaletea matatizo vijana wengi sana. Kuna mawakala wengine wanawakamua vijana walipe hela ili wawasadie. These things need to be transparent.Mkuu dfk kadito mawakala wanaotambulika na fifa toka tanzania ndio hao hao hata mi nimeona majina hayo hayo kwenye mtandao wa fifa
Mwaka jana kuna watu walituma barua TFF wakijifanya ni maWakala wa Thailand wana ushirikiano na Liverpool. TFF wakatangaza vijana wachangamkie deal. Kukawa na sign of fee hao watu inabidi walipwe. Kuna mzazi mmoja akanifuata akaniambia, kwanini usimpeleke huyu kijana Thailand. Nikamsikitikia sana. Nikamwambia, kwanza mpira wao uko chini kama TZ tu. Pili, wakala anayekuomba hela aprocess mambo ya usafiri ni mwizi. Tatu, kwanini upitie Thailand ili ufike Liverpool? Yule mzazi aliona kama nambania. Baada ya wiki 2 hivi, TFF wakatangaza kwamba hao jamaa ni wasanii.
Kwahiyo, mwache bwana Malinzi ajibu, inawezekana wapo wengine ila tovuti ya FIFA haiko updated.