mike2k
JF-Expert Member
- May 12, 2016
- 1,571
- 3,448
- Kwa nini Kim na rafiki yake kipenzi, Simone Harouche walibaki chumbani wenyewe bila mlinzi wakati wakijua wana vito vyenye thamani kubwa na kujipiga picha kwenye mitandao ya kijamii?
- Kwa nini hakukuwa na kamera za CCTV katika nyumba hiyo ambayo ni ya gharama kubwa. Nyumba hiyo inalipiwa karibu Sh 60milioni kwa wiki.
- Kwa nini awepo mlinzi mmoja tu kulinda hoteli hiyo ya gharama ambayo nyota wakubwa kama Madonna na Leonardo di Caprio hupanga? Nyumba hizo zina mpishi maalum, dereva na watumishi wengine.
- Majambazi waliwezaje kuingia kwenye mlango wa hoteli hiyo wakati unalindwa na mitambo maalum. Milango haikuonyesha kama mtu alilazimisha kufungua au kuvunja kitasa.
- Ni taarifa gani mlinzi aliyekuwepo lindo siku hiyo alikuwa nazo kuhusu Kim na wenzake hadi alipobanwa na kufungwa na majambazi akazitoa?
- Kwa nini mlinzi wa Kim Pascal Duvier aliondoka na kumuacha mwanamitindo huyo peke yake. Majambazi walijuaje kuwa Kima yupo peke yake?
- Kwa nini Kim aliruhusiwa kuondoka Ufaransa saa chache baada ya kuvamiwa