Maswali ya dini polisi yakomeshwe

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2010
Posts
2,182
Reaction score
308
Leo nimejikuta mikononi mwa polisi, miongoni mwa maswali yaliyonikela ni kuulizwa dini yangu.

Kwa mazingira ya sasa swali hili inabidi lisiulizwe kwani udini unashika kazi na dini inaweza kukukosesha haki yako.

Kama swali hili ni la mhimu polisi basi na waislamu walikuwa sahihi kuomba liongezwe kwenye dodoso za sensa
 
Kuna kauhusiano fulani kati ya dini ya mtu na aina fulani fulani za makosa. Yaani ukutwe umejivika au umebeba mabomu halafu usiulizwe dini yako? Anyway, ungetueleza kilichokufikisha huko polisi tungeweza kudadavua vizuri zaidi.
 
Hata Mahakamani kabla ya kutoa ushahidi unaulizwa dini yako ili uape kwa kutumia kitabu cha dini yako. Kuna sehemu suala la kuulizwa dini yako halikwepeki labda izuiwe kuapa Mahakamani na hata affidavit huwa kuna sehemu zinatofautiana kutokana na dini ya mtu.
 
Wanauliza kwa sababu maalumu!!! UNaweza kushikiliwa polisi halafu ukakutwa na umauti huko huko!! Inapotokea hamna ndugu waliojitokeza, basi utazikwa na serikali kwa imani ya dini yako ambayo umeitaja!! So, kama wewe ni Mkristo halafu ukakamatwa Zanzibar kisha baada ya kuulizwa dini ukataja Muislam kwa kuzani utapendelewa kwavile Mwislamu mwenzao basi fahamu siku ukifa utazikwa kama Abdulrahman na sio kama Joseph!
 
swali la dini ni muhimu sana,ni serikali hii ya ccm tu,kwa kuwa haitaki haki kwa wote ndio maana awalitaki,unaacha kuuliza dini unauliza kabila,huu si ujinga.ospitali unaulizwa kabila,inasaidia nini?
 
kuulizwa dini ni muhimu sana..be proud of your religion...........
 

Sioni ubaya wa swali hilo, uenda police wana lengo zuri tu wajue dini yako ili wasikutendee au wasikujumuishe kwenye mambo ambayo dini yako hairuhusu. NB; Hakuna connection kati ya swali hilo polisi na maswala ya sensa.
 
Ki ukweli ni muhimu kwani kuna baadha ya haki ambazo nimuhimu kuzipata, Mfano kwa sisi WAISLAM ni muhimu kupata muda wa Kuswali kwa vipi ndi vyote vya swala kwani kuwa mahabusu sio sababu ya kukufanya ushindwe kumtumikia Mungu wako.
 
Nashukuru wadau kwa michango yenu, dudus nilifika polisi kwa sababu ya traffic offense kuna mtu aliukwaruza mkokoteni wangu hivyo ikatulazimu tukwende polisi kusuruhishwa.

Hata hivyo nilijuta kwani nilipoteza muda na gharama zaidi wa kutaka kupata haki yangu, kuna kitu nimejifunza kuwa Haki inagharama kubwa sana Tanzania, kwanza ukubali kupoteza muda halafu ukubali kusutwa kwa kejeli na madongo kedekede halafu uwe mvumilivu kwelikweli kwani unaweza kujikuta wewe ndiye mkosaji kama mtesi wako ataongea vizuri na pilato
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…