Mkuu naomba msaada mwaka 2019 dec nilipigwa Tsh 8,000,000/- na kampuni moja (sitaitaja) ya kudrill visima. Alikuja jamaa mmoja toka Tanga akapima eneo akaniambia maji yapo. Akaniletea hiyo kampuni tulikubaliana sh laki moja kwa kila mita moja.wao walivyopima walisema maji yanapatikana mita 120. Hivyo nilitoa advance 7,000,000/- wakaja kudrill. Lkn hadi mita 120 walizosema maji hayakuoatikana. Tukaongeza mita 30 zaidi bado hatukupata maji. Tukakubaliana tuongezee milioni moja kwa ajili ya mafuta ili wajaribu eneo jingine. Niliwalipa hizo fedha lkn hawakujaribu eneo jingine wakadai magari yao yanawra kukwama hivyo watarudi baadae maana kilikuwa kipindi cha mvua. Lkn hadi leo hawajarudi. Niliwahi kuwafuata ofisin kwao wanatupiana mpira wao na mpimaji aliyepima na kusema maji yapo. Ukienda kwa mpimaji anakwambia niwadai heka yangu.