Mimi nilimfuta ZZK akilini nilipojua anamiliki Hummer! Hili ni gari ya anasa, ni gari za kina messi, drogba, 50cent-watu ambao unaweza ukasema "wanachota" pesa. Si gari ya kutumia mwakilishi wa wananchi maana ni gari ya kuonyeshea jeuri ya pesa. Naomba ieleweke kwamba sina pingamizi kwa viongozi wetu kutumia usafiri bora utakaowawezesha kufika hata vijijini, ninapinga anasa maana ktk anasa watu hulewa na wakilewa huwatapikia waliowabeba.
Ndio, mtu mlevi wa madaraka hana maono, atataka tu kutuonyesha kwamba nae anaweza akapambana akawa kiongozi wa juu ktk nchi yetu. Watanzania hawahitaji wala kustahili kuwa na kiongozi mwingine anayetaka tu historia ije isome jina lake kati ya viongozi waliowahi kuliongoza taifa letu. Hatutaki urais wa mtu binafsi "kujinoma". There is no time for personal victory in this country, never again!