Wanyama wanatumia zaidi milango ya fahamu katika kuishi kwao, na hasa mnuso (smell). Ukimchukua kwa mfano mbwa ukaenda naye kwa miguu hata km. 20, halafu ukamtoroka, mbwa yule atarudi nyumbani. Atatumia zaidi harufu - atapita sehemu zile mlizopita mpaka atafika nyumbani.
Wanyama hawaplani kama mwanadamu katika maisha yao lakini wana kitu kinaitwa silika (instinct). Hii inawasaidia kuitikia hali mbalimbali wanazokumbana nazo. Kumbe hawawezi kupanga mipango ya baadaye (yaaani ya kuja kutekeleza kwa mfano kesho) - kama afanyavyo binadamu kwani hawana akili na utashi. Kutafakari pia hawawezi. Ila kuna aina fulani ya kumbukumbu (inayojificha katika milango ya fahamu ya wanyama) ambayo kwa mazingira fulani inaweza kumfanya ku-react kwa namna inayotegemewa. kwa mfano, mbwa ukimpiga, anabaki na identity ya ubaya (uadui) wako kwa njia ya harufu yako. Kumbe akikuona siku nyingine, ile harufu ya wewe akishainusa mara moja anahisi kwamba wewe ndo yule uliyempiga au kumtendea ubaya. Na mara ata-react negatively dhidi yako au kwa kubweka, au kukushambulia.
Wanyama wanaweza ku-lie instinctively siyo rationally. Mfano, mdudu aitwaye kifa-uongo au hata kobe. Kifa-uongo ukimgusa anakauka kabisa kana kwamba amekufa (anadanyanya - mzima sana tu). Hii ndo namna yake ya kujilinda. Lakini hafanyi hivyo kwa kutumia akili, bali silika. Vivyo hivyo kobe, ukimshambulia anaficha kichwa kwenye gamba na kukauka kana kwamba ni mfu kumbe anajihami.
Nadharia ya ku-cheat ina presuppose uwepo wa ujuzi, utashi na uamuzi. Mnyama hawezi ku-che