Under-cover
JF-Expert Member
- Nov 13, 2023
- 1,834
- 3,042
Mimi ni nina maswali kadhaa kuhusu hizi imani zetu hizi, naomba kwa wenye uelewa wanijibu 🙂,
1.Tunaamini Mungu anajua kila kitu , mambo yaliopita, ya sasa, na yajayo sio?, ok ivi ni kwanini wakati wa uumbaji wake aliamua kumuumba lusifa ambaye baade aligeuka kuwa shetani, je hakujua kuwa hiki kiumbe nachokiumba kitakuja kuleta madhar duniani au kukengeuka?,
2. Kama shetani aliweza kuishawishi theruthi moja ya malaika mbinguni na wakamuasi Mungu tena waliyekuwa wanamuona ,je huyo huyo atashindwa vipi kumpotosha binadamu kupitia hayo hayo maandiko ?
3. Mwanzo dhambi haikuwako kabisaa huko mbinguni , ila baadae ililuja jitokeza kupitia kwa malaika wa sifa lusifa aliyekuwa mtakatifu , vipi kwa wale wanaoamini katika ulimwengu ujao kuishi maisha matakatifu na yasio na shida, je hakkutatokea tena ukengeufu kama mbingu ya mwanzo, maana hata wale watakatifu malaika walitenda dhambi na wakafukuzwa.
4. Nilisoma katika biblia sikumbuki ni kifungu gani, kinasema, Nawafahamu walio wangu toka kuumbwa kwa ulimwengu, hapa Mungu alikuwa ana maana gan?, kama toka mwanzo wa ulimwengu hatima ya mtu inajulikana kwa Mungu, sasa kwanin watu wajiangaishe kuutafuta uzima wa milele wakati ni kama kila kitu kilishakuwa planned , ni kusubiri tu wapi mtu ataangukia alipoandikiwa?
5. Iv Mungu anafanya kazi kwa watu wa aina gani? kuna msabato, m roman, mlokole, kkkt, pentekoste, na hapa kila mmoja anamuona mwenzake kapotea, lakini huwezi kusema katika hayo madhehebu yote ukakosa baadhi ya watakatifu , na hapa kila mmoja anakwambia ana ongozwa na roho mtakatifu, napenda kuchukulia mfao hawa walokole na wasabato mara nyingi huwa kila mmoja anasema ana roho mtakatifu anamuongoza, na naamin wapo walio na roho mtakatifu, swali je kama mna roho mtakatifu kwanini mmetengana , kwanin kila mmoja anamuona mwenzie kapotea?
HAYO NI MASWALI BAADHI TU KWANZA.