Wasaalam ndugu zangu WaTanzania.
Ningependa niende moja kwa moja kwenye mada yangu.Toka ACT WAZALENDO ijiunge na serikali ya Zanzibar kumekuwa na minong'ono mingi sana na kuonekana kama ACT ni wasaliti kwa WATANZANIA.
CHADEMA waliitisha kamati kuu kuwajadili kina MDEE kwa kukubali kuingia BUNGENI wakati KATIBU MKUU AKIWA HAJAPELEKA MAJINA.
Je, mbona hawakumjadili yule dada aliemtoa Kessy jimboni na wakati wenyewe hawautambui uchaguzi huu kama wa huru na haii?
Je, kosa la kina mdee ni kwenda bungeni huku majina hayajapendekezwa na katibu mkuu au kosa la kina mdee ni kukubali kuhalalisha uchaguzi?
Je, ni mwaka gani toka mfumo wa Vyama vingi uanze ambao UPINZANI wameshawahi kuyakubali matokeo ya uchaguzi kuwa yalikuwa huru na haki?
Je, kama wapinzani wanaona Uchaguzi huu ni hovyo zaidi ya zilizopita kwahyo kuna kuvumilia maovu ambayo hayaathiri maslahi yao na kutokuvumilia yanayoathiri maslahi yao?
Je, kama Mbowe,Zitto n.k wangechaguliwa majimboni wasingetambua matokeo haya?
Je, uwepo wa mbunge wa kuchaguliwa bungeni ambae CHADEMA hawajamchukulia hatua nini tafsiri yake?
Je, CHAMA kinapata ruzuku au hakipati kama kinapata je kinapata kwa vigezo vipi?
Mbona kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa walisusia baada ya wagombea wao kukatwa mbona uchaguzi mkuu hawakususia baada ya wagombea wao kukatwa.
Je, walitegemea muujiza gani katika huu uchaguzi na wakati kila wakati wanasema TUME YA UCHAGUZI sio huru na haki.Na kila mara wanasema polisi na vyombo vingine vya usalama vinawasaidia CCM?
MWISHO KABISA NISEME WATANZANIA HASAAA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NA WASHABIKI WAO ACHENI UNAFIKI.
KWA UPANDE WANGU ACT WAZALENDO WAPO SAWA KABSA MAANA KUMSUSIA FISI BUCHA NI KOSA KUBWA SANA.