Mataifa 11 barani Ulaya yafanya makubaliano ya kufungua mipaka yao kwa ajili ya kuanza kupokea watalii

Mataifa 11 barani Ulaya yafanya makubaliano ya kufungua mipaka yao kwa ajili ya kuanza kupokea watalii

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Taarifa ya pamoja iliyotolewa na tovuti ya kidiplomaisa ya Ureno imesema, mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 11 za Ulaya wamekubali masharti ya kufungua tena mipaka na kurejesha uhuru wa mawasiliano kati ya wakazi wa Ulaya.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wawakilishi kutoka Ujerumani, Austria, Bulgaria, Cyprus, Croatia, Hispania, Ugiriki, Italia, Ureno na Slovenia walishiriki kwenye mkutano kuhusu kurejesha uhuru wa mawasiliano na mzunguko kati ya Umoja wa Ulaya uliofanyika kwa njia ya video.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Bw. Heiko Maas amesema, Ujerumani itaondoa tahadhari ya utalii ndani ya Umoja wa Ulaya kuanzia tarehe 15 Juni, ili kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kupokea idadi kubwa ya watalii wakati wa msimu wa joto.

Lakini hatua kadhaa za zuio zitachukuliwa katika sekta hiyo kutokana na kuwa mlipuko wa COVID-19 bado haujamalizika.
 
Pamoja na Rwanda kurekodi visa zaidi ya 1000 ukilinganisha na visa 409 Tanzania, Rwanda yaruhusiwa kupokea watalii kutoka Ulaya.

Mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana juu ya kile yanachokiita “orodha salama” kwa mataifa 14 ambayo yataruhusiwa kwa safari zisizo muhimu kuanzia Julai, huku Marekani ikiwa haimo kwenye orodha hiyo.

Baraza la Umoja wa Ulaya limesema hapo jana kwamba nchi hizo salama ni Algeria, Australia, Canada, Georgia, Japan, Montenegro, Morocco, New Zealand, Rwanda, Serbia, Korea Kusini, Thailand, Tunisia na Uruguay.

Kundi hilo la mataifa 27 linatazamiwa kutoa muongozo unaolegeza au kuruhusu safari za matembezi ama kibiashara kuanzia kesho leo Jumatano kwa mataifa hayo.

Tunavuna tulichopanda?
 
Heading yako inaonyesha kana kwamba Tz tumetajwa moja kwa moja tusitembelewe.List yenyewe mataifa ya Africa ni manne tu.Hata Uganda na kuisifia kote haipo.

Nia yako ni uiponde Tanzania tu!
 
Back
Top Bottom