Mataifa ambayo ni vigumu kuyavamia kijeshi duniani

Hiyo namba 7 imevamiwa juzi tu na bado wavamizi wanateka maeneo hivyo iondoe kwenye orodha.
 
Ukitaka kujua hakuna mpangilio wa maana ebu cheki hio Bhutan sifa zake
Yaani hizi data ni ovyooo
 
Japan kabla ya ww2 walikuwa vizuri sana kijeshi.

Nawasifu waliamua kuachana na huo ujinga wa vita na wanafanya maendeleo tu, wakirudi kijeshi sidhani Asia kuna atakayewafikia, hata China haitowaweza.
China itoe mzee.
China hii sio China ile,hata Japan angeendeleza ubabe ila kuikuta China hii sahau.
China ni nightmare.
 
Kwa Israel ninaitoa kwenye list naiweka Mongolia.
Israel imeshavamiwa mara kibao na hata hiyo iron dome yake inayosifiwa imeonesha failure kaskazini mwa Galilaya kwa kushindwa kuzuia makombora ya kundi la wapiganaji wa Hizbollah.
Hiyo imepelekea wakaazi takriban laki tatu wahame kaskazini mwa Israel kuja kanda ya kati ya Israel.

Sababu ya kuiweka Mongolia badala ya Israel ni kwasababu Mongolia ipo katikati ya China na Russia.
Na Mongolia ni mshirika kiuchumi na kijeshi wa nchi zote mbili China na Russia.
Ili uivamie itakubidi uvuke anga la China au Russia kitu ambacho haiwezekani.

Kwa Bhutan ningeiweka China,kwasababu licha ya sababu za kijiografia walizozieleza India sio mwanachama strong in millitary wise.
 
Hivi vita bado sana mpaka Russia afirisike safari hii, alijifanya klabu bingwa (Real Madrid) sasa hadi atashushwa daraja.
 
Japan Watu hawamzungumzii ila alitoa kichapo sana, na walikuwa Makatili Netanyahau ni mtoto
Kumbe umesoma kuwahusu vyema, jamaa walikua hatari wale.
Hadi US kuamua kuwatwanga nuclear si mchezo.

Ile nuclear ya kwanza pale Hiroshima jamaa hawakukata tamaa, walipopigwa ya pili ikabidi wanyooshe mikono juu.

Walikuwa na roho ngumu mno, na wale marubani wao 'kamikaze' ni kujitoa mhanga tu. Hawaogopi kufa.
 
China itoe mzee.
China hii sio China ile,hata Japan angeendeleza ubabe ila kuikuta China hii sahau.
China ni nightmare.
Fuatilia vizuri history ya Japanese.
Hao viumbe ilikuwa species nyingine.

China hio iliyosema ina attack ndege ya Pelosi baadae kumbe ni mkwara, enzi za Japan hio ndege ingepigwa.

Shambulizi la Pearl Harbor walichokifanya ilikuwa kama movie hata US alishindwa kuelewa hao viumbe wanajiamini kitu kipi.

Hao jamaa waache waachane na vita. Walikuwa si watu walikuwa shetani.

Kwenye technology Japan itakuwa inaizidi China hasa electronics, nakubali China kuna vitu inaizidi Japankwenye tech hasa telecommunications, energy n.k, ika robotics n.k China haina nafasi kwa Japan.
 
Mkuu unaleta leta stori za zilipendwa,sawa tunajua Japan ilikua na jeshi imara kabla ya WW 2.
Ila kwasasa China ina jeshi imara kuliko Japan mkuu.
Sio infantry,sio kimakombora ,sio kwa fighter jets wala sio kwa submarines.
Sababu inayomfanya China atoe mikwara mingi ni uchumi tu.
Na ukitizama China haikuwa na sababu haswa ya kumlipua Nancy Pelosi alipotembelea Taiwan,taifa lenyewe China bado hawajalichukua bado.
Embu rejelea Korea war 1959 unadhani nani alimpa nguvu North Korea akaishinda South korea ambayo ilikua na msaada wa kijeshi wa USA kama sio China!?
Rejelea pale South China sea,US alipeleka meli vita na aircraft carrier akimuahidi Phillipines atamkombolea visiwa vyake,China alipo deploy dongfeng ballistic missiles 2018 hakuna meli vita ya USA ilikatiza na kupita South China sea.

Tunakubali Japan alikua ni taifa lenye nguvu hapo kabla.
Ila China ni nightmare mkuu.
China iachwe kama ilivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…