Duh!! umekuwa brainwashed na propaganda za kimagharibi ambazo zimekupa upofu wa kuona mbali na kukupa mahaba yao!!!!
Hizi propaganda zipo kimkakati ambao ni kudumisha na kuimarisha utawala kimagharibi katika ulimwengu huu katika nyanja muhimu mfano uchumi,kisiasa, utamaduni na kijamii.
Kinapoonekena kwamba kuna kitisho dhidi ya mfumo wa kimagharibi hapa ndipo nguvu ya propaganda inavyoonekana. Kupitia filamu,muziki,mavazi,michezo n.k watu wengi wameaminishwa kuwa dunia ni lazima iendeshwe kimagharibi jambo ambalo siyo kweli na upotofu mkubwa.
Swali : Je, unaamini kuwa mfumo wa kimagharibi ni lazima ufuatwe na watu wote duniani??. Jibu kwa kutumia fikra tunduizi .
Mwisho: Tujifunze kuutafuta ukweli kwa kutumia fikra tunduizi na siyo kumezeshwa kila kitu.Russia,China,Iran na Wamagharibi wote wanatumia Propaganda kueneza na kuimarisha Mifumo yao!!!! Je, sisi tupo wapi????