Matajiri Kenya kueleza vyanzo vya mali zao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Uhuru Kenyatta: Maafisa watakaohusishwa na ufisadi watatimuliwa serikalini

Unapotajwa katika kesi ya ufisadi na kupelekwa mahakamani utalazimika kuondoka serikalini , amesema rais Uhuru Kenyatta.

''Nitachukua hatua ya kumuondoa afisa yeyote wa serikali atakayekuwa na kesi ya kujibu mbela ya mahakama'', aliongezea.

Akizungumza wakati wa hotuba kwa taifa siku ya Alhamisi Uhuru amesema kuwa amekuwa katika shinikizo ya kuwafuta maafisa wa serikali.

Hakutakuwa na afisa atakeysazwa katika vita dhidi ya ufisadi .

Hatahivyo amesema kuwa serikali itafuata njia za kisheria katika kuwashtaki wahusika.

Ufisadi serikalini

Amesema kuwa vita dhidi ya Ufisadi havitafanywa kupitia pingamizi na taarifa za vyombo vya habari.

"Vitendo vyetu havitakuwa vya shutuma...demokrasia yetu inafuata sheria hivyobasi mchakato wa kuwachukulia hatua wanaofanya makosa ni muhimu katika kutekeleza wajibu huo''.

Mapema Uhuru Kenyatta alifutilia mbali uteuzi wa jaji Joseph Mutava. Hii ni baada ya mahakama ya juu kupendekeza kuondolewa kwake kutokana na uovu aliotenda.

Aidha Amesema kuwa watu matajiri kupitia kiasi ambao maisha yao haiendani na kodi wanayolipa watalazimishwa kusema ni wapi walikotoa fedha ama mali hiyo, alisema katika machapisho yake katika mtandao wa Twitter.

''Haturudi nyuma katika mapambano dhidi ya ufisadi kwasababu tumejitolea kuhakikisha vizazi vijavyo vinarithi Kenya iliyo imara inayoheshimu utawala wa sheria.

Alisema kuwafunga jela au kuwatoza faini watu waliyoba mali ya umma haitoshi, lazima warudishe mali hiyo.

''Suala la uadilifu linatarajiwa kuwa jambo la kawaida siku za usoni'' alisema Bw. Kenyatta.


Sent using Jamii Forums mobile app

BBC
 
Wote wana harufu ya ufisadi wa kutisha, maana ukiona matajiri watumishi wa serikali, wote wameupata kupitia siasa au ofisi za umma.

Kabla ya kuwa wanasiasa / mawaziri walikuwa hustlers lakini muda mfupi tu wa kuingia ktk ofisi za umma wanakuwa mamilionea ktk Kshs. au mabilionea ktk Tshs.

After Parliament successfully conducted vetting of new CSs,who were forced to reveal their wealth, a list of richest Cabinet Secretaries has emerged.

  1. Simon Chelungui KSh 796 million (Tshs. 14 Billion)
  2. Keriako Tobiko KSh360 million
  3. Charles Keter KSh352.8 million
  4. Ukur Yatani KSh 295 million
  5. Joe Mucheru KSh267 million
  6. Peter Munya KSh 264 million
  7. Ms Farida Karoney KSh200 million
  8. Sicily Kariuki KSh168.3 million
  9. Margaret Kobia KSh 165 million
  10. Monica Juma KSh 50 million
  11. John Munyes KSh 50 million
  12. Rashid Echesa KSh 40 million (Tshs. 800 million)
 
Asante kwa kufuata Kenyan news kwa makini. We are the biggest brother
 
Nilisikia Benjamin Mukapa ameficha yake Uswizi?
 
Naona Ruto anawindwa kama tembo

Sent from my SM-A605G using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…