Matajiri kumi Tanzania ni hawa

chabuso

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Posts
6,380
Reaction score
5,884
Hawa ni Matajiri kumi Tanzania, kutokana na survey ya Bongoland wanane ni watanzania wenye imani ya kislam wenye asili ya kiasia, wawili tu ndio wakristo na hao ndio wenye asili ya Kiafrika...,Kwanini watanzania wenye asili ya Kiafrika wako kidogo katika kumiliki utajiri wa Tanzania...

 
​ukitaka kujua kuwa Mwenyezi Mungu amekubariki zaidi muangalie wa chini yako
 
waarabu wanasystem nzuri yakukuzana kiuchumi kama familia au ukoo..unaweza ukapewa mtaji na familia yako ukaanza maisha...lkn wabongo unapewa hela ya msosi tu kama unashida...na hata tushazoea ukienda kwa ndugu hauombi mtaji unaeleza shida tu......ndo mana unakuta kunamatajiri mjini lkn kijijini kwao kwenye ukoo kunawatu wanateseka kimaisha lkn msosi hawakosi....ndomana wanasema Tanzania huwezi kufa na njaa lkn utakufa na umaskini.....
 

indeed umenena vema
 
Hao waasja ni mfumo wao wa kurithishana mali ndo mana hapo unamwona gulam na Mohammed dewji hata manji nae za kuzikuta,ila ingawa wamezikuta hongera kwa kuzikuza.
 
Mbona hamna Muhaya hata mmoja? Hiyo orodha ni fake maana haiwezekani Mtu anakwambia milioni 10 ni hela za mboga halafu wasiwemo hapo.
 
Mkuu sijamuona diamond hapo,na yeye nakumbuka alisema ana more than bilion bank mwaka 2013,kwa sasa atakuwa na bilioni nyingi,kwanini awajamuweka.
 
Nazani ni tatizo la siasa za bongo. Hawa waarabu ma waindi wanajua kuwatumia wanasiasa wetu bilaza na waroho wa kupata utakiri mchwara.
 
Halafu hao matajiri wawili wakristo kwenye asili ya kiafrika hapo ni wachaga tu je INA maana nyie wachaga ndo mnaongoza kwa utajiri Tz??
 

Umegusa ukweli kwa 100%. Hizi nywele ngumu ni shida. Yaani mtu akishapata mali anafurahi sana kuona ndugu zake wakiteseka ,kujikomba, kujinyenyekesha kwake wakiomba msaada. Yeye kwake ni fahari....
 
Mbona hamna Muhaya hata mmoja? Hiyo orodha ni fake maana haiwezekani Mtu anakwambia milioni 10 ni hela za mboga halafu wasiwemo hapo.

Ali Mufuruki ni muhaya. Anamiliki sehemu ya maduka ya Woolworths kwa Tz na Ug pamoja na makampuni mengine ndani ya kundi makampuni la Infotech. Mtu mtaratibu sana.
 
Hawa ni Matajiri kumi Tanzania, kutokana na survey ya Bongoland wanane ni watanzania wenye imani ya kislam wenye asili ya kiasia, wawili tu ndio wakristo na hao ndio wenye asili ya Kiafrika...

Chabuso umekosea. weusi wapo watatu. Mmoja, Ali Mufuruki, ni muislamu. Ulihisi nae muarabu? Wengi hawamjui maana hana makeke hata. Anatengeneza hela tu mdo mdo.

Vyovyote vile, tusiangalie rangi ya ngozi bali mchango wa mtu katika ubora wa Taifa letu. Sio kila mweusi ana jema kwa Taifa na si kila mweupe ni mbaya.

Mwishowe, hiyo orodha ni ya lini? Mo Dewji ndo manyota sasa hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…