Matajiri malizeni mgomo wa madereva

Matajiri malizeni mgomo wa madereva

LIKUYU SEKA

Member
Joined
Nov 15, 2013
Posts
53
Reaction score
24
Ni wasaa mwingine watanzania wenzangu tukibadulishana mawazo katika mtandao huu adhimu kwa mada motomoto,natumai mungu amewajalia heri katika shughuli zenu za kila siku ..

Wote ni mashihidi kuwa katika kipindi cha mwezi Wa nne na Wa tano tumeshuhudia mgomo Wa madereva Wa mabasi ya abiria,pamoja na malori ya mizigo ambao ulitikisa taifa kwa wananchi Wa kawaida akina mwache apotee wakihaha kwa kukosa usafiri kutoka eneo moja kwenda Jingine na Mkoa mmoja kwenda Mkoa mwingine,wengine wakishindwa kusafirisha wagonjwa na wengine wakishindwa kufika kwenye usaili na mambo mengine hakika ilikuwa ni adha kubwa kwa watu.

Msingi Wa mgomo huo ni madai ambayo ya madereva ambayo ni ya muda mrefu miongoni mwa .madai hayo ni pamoja na mikataba ya kudumu ya kazi ambayo itawapa nguvu kisheria na kuwafanya wasinyanyaswe tena na matajiri zao,kupinga kurudi tena darasani kwa kile walichosema ada kuwa kubwa lakini pia kutoonekana mantiki ya wao kurudi darasani tena kwakuwa hata wakisoma hakuna kinachoongezeka kwao.

Kwenye andiko hili nitajikita kutazama hoja ya mikataba,kimsingi binafsi naunga mkono hoja yao ya kudai mikataba ni hoja nzito na inayopaswa kutafutiwa jibu kwa haraka kwa mustakabali Wa maisha ya madereva hawa,nimekuwa nikijiuliza kuhusu suala hili kwa undani zaidi ..maswali tata ninayojiuliza ni pamoja na mosi Hivi hawa madereva anayepaswa kuwapa mikataba ni nani???serikali au wamiliki Wa mabasi?????pili
Na je ni lini huyo anayepaswa kutoa mikataba atatoa????Tatu ni kuwa je ni kweli madereva wote hawana mikataba??na kama wanayo inafananaje???kwa Maana ina vipengele gani hasa...

Maswali haya nimekuwa nikijiuliza kwakipindi kirefu lakini nimefanikiwa kupata majibu ya machache kati ya hayo ambayo kimsingi tunahitaji kuwa wakweli ili kufikia muafaka..

Wataalamu Wa sheria wanatafsiri neno mkataba kama makubaliano ya hiyari baina ya pande mbili zinazotaka kuwa na makubaliano,tukija kwenye mkataba Wa kazi maana yake ni makubaliano ya mwajiri na mwajiriwa na mara zote huwa makubaliano ya dhati kwa pande husika,hii hutokea kwa waajiri wote na waajiriwa bila kujali ni sekta gani utofauti hutokea kutokana na ajira husika,mathalani mkataba Wa daktari na mwalimu huwa na utofauti .

Dhana ya mkataba kwenye ajira mara zote huangukia kwa mwajiri husika,sasa tukirudi kwenye hili la madereva kimsingi Matajiri wenye mabasi ndio wanapaswa kutoa mikataba na si inavyofanyika sasa,hili linapaswa kufahamika kwa uwazi Kwa watu wote ni wakati muafaka serikali kuweka wazi jambo hili.


Mgomo uliofanyika Mara ya pili tulishuhudia ukizimwa kwa staili ya funika kombe mwanaharamu apite ni ukweli usiopingika serikali haina ubavu Wa kumaliza hoja ya mikataba ya ajira wanayotaka madereva,ni kwabahati mbaya ukweli unapindishwa katika hili nafikiri ni wakati sasa serikali kusema ukweli na kuwaambia matajiri Wa mabasi,daladala na malori Kuwapa mikataba wafanyakazi wao.


Nimechokoza mjadala ...
 
Hoja yako ingepata nguvu zaidi kama ungeipeleka sehemu ya habari mchanganyiko or kwenye business ingekua poa sana lakini hapa kwenye jukwaa la Katiba naona kama umeipotezea njia!thanx
 
Back
Top Bottom