Sikujua kama sisiemu imekosa kabisa wenye akili kiasi hiki? Yani hata wa kujifikiria tu kama kumleta singasinga kuna impact gani ya kisaikolojia kwa wanachama wao? Taswira ya chama chao kwa umma itakuwaje? Yani mtu waliyemfunga wao wenyewe na kumlipisha mamilioni kwa plea leo kaja kama mmoja wa wafadhili wakuu wa mama yao?
Hii ni kufuru na kuwadharau sana wanachama wao kwamba hata nini kitokee hawana cha kufanya, kama ambavyo wamejipendekeza kugombea na hamna wa kuwafanya lolote, kama nyumbu tu simba anapokuja kuchukua ndugu yao wanatazama tu kule porini!