Matajiri wengi wapo katika kundi hili. Soma kama unataka kuwa tajiri

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Watu wanaoamini katika mambo makubwa wanaitwa wabunifu wa maono makubwa au watu wenye maono makubwa.

Hawa ni watu ambao wanaamini na kutafuta kutimiza malengo ya juu au malengo makubwa ambayo wengine wanaweza kuyaona kama changamoto au yasiyowezekana. Sifa zao ni pamoja na:

1. Ubunifu
– Wanakuwa na uwezo wa kufikiria nje ya mipaka ya kawaida na kutengeneza suluhisho za ubunifu kwa changamoto mbalimbali.

2. Uthubutu – Wanathubutu kufuata malengo makubwa hata kama yanaonekana magumu au yasiyowezekana kufikia.

3. Kujituma – Wana ari ya kufanya kazi kwa bidii na kutokata tamaa hata wanapokutana na vikwazo.

4. Maono ya mbali – Wanatazama mbali zaidi na kupanga kwa kuzingatia matokeo ya muda mrefu badala ya mafanikio ya muda mfupi.

5. Uongozi – Wana uwezo wa kuongoza na kuwahamasisha wengine kushiriki katika kutimiza maono hayo.

6. Imani na matumaini – Wanakuwa na imani thabiti katika uwezo wao na matumaini kwamba wanaweza kufikia malengo hayo makubwa.

7. Uvumulivu – Wanavumilia changamoto na kushikilia maono yao kwa muda mrefu mpaka wafanikiwe.

Watu wa aina hii mara nyingi hutambulika kama viongozi, wajasiriamali, au watu wanaoleta mabadiliko makubwa katika jamii au sekta zao.
 
Yeremia 27:5 BWANA anasema yeye
Ndiye aliyeumba dunia wanyama na vyote vilivyomo naye humpa amtakaye kama imfaavyo

Japo kuwa kuna utajiri mwingine ni wa majin, mizimu, ufisadi,dhuluma na utapel na uuaji ambao hauusian kabisa na BABA wa mbingun
 
Hahaha, kalagabao. Mentaliti hii ya kuamini mauchawichawi imeenea sana miongoni mwa vijana wengi ambao wanaamini kuwa mafanikio ya kifedha yanatokana na uchawi, wizi, ubadhirifu nk na kwamba sio rahisi mtu kufanikiwa kifedha kwa njia halali.

Huu ni ugonjwa mkali sana wa kisaikolojia unaowakumba vijana unahitaji tiba mara moja; vinginevyo, unaweza kumfanya mtu awe fukara hadi kifo, kwa sababu anaamini pasipo uchawi hakuna utajiri.

Jitahidi kupata fedha za kutosha zitakazokusaidia kutatua changamoto za jamii yako na pia kukuwezesha kufanya ibada, kwani hakuna ibada isiyohitaji mali. Soma vitabu mbalimbali vikuelimishe zaidi...
 
Mkuu kwenye kitabu cha mafanikio kuna kurasa husomwq kimyakimya, aliyesema ni rahisi kwa Ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa Mungu wala hakukosea kabisa.
Labda kama unazungumzia utajiri wa kumudu chakula milo mitatu, kuwa na nyumba ya kuishi tu na usafiri sawa hapo unaweza ukafika level hizo bila kuvunja katiba.
Ila kuwa na dili za Bilioo lazima upige dili za smuggling, dili haramu, ukwepaji kodi, wizi na mwisho wa siku unaangukia kwenye money laundering and counterfeit ili kuhalalisha utajiri wako mbele ya macho ya jamii na mifumo ya Serikali.
 
Kwaiyo kukwepa kodi ni dhambi
 
Back
Top Bottom