Matambiko sio Ushetani

Ndugu, nimecheka kidogo! Sio kwa kukudharau hapana! Bali umegusa mambo ambayo nilikwambia tayari nilishaya experience kwa zaidi ya miaka 30,

Hayo ya kumuona babu yako nilisha yafanya miaka mingi, Tena sio kumuona tu, tulikuwa tunakula nae na kushiriki mambo mengi pamoja nae! Na sio Babu tu hata ndugu wengine waliokufa zamani walitokea na kuongea nao na kula nao!

Tena hao mababu wazamani na ndugu waliokufa walikuwa wakitokea wanakwambia mambo ambayo unakuja kuyaona baadae! Mambo ambayo lazima yatokee na yanatokea kweli! Akikwambia kuna hili na hili Basi ujue piga ua lazima litokee kweli, na linatokea muda si mrefu! Ni kiasi tu cha kujiandaa na hilo jambo!

Kwahiyo nasema tena matambiko ni IBADA sio utamaduni tu! Tena ibada yenye matokeo! Iwe unajua au hujui, mambo ya mizimu kuwa kwenye damu hiyo sio kweli inategemea na ushirika wako na hiyo mizimu! Otherwise unaongelea scientific! Genetics au vinasaba ni kweli viko kwenye damu kwasababu wazee wetu ndio wametuzaa tumecoppy genetics zao! Lakini hapa tunazungumzia MIZIMU kama ROHO na sio scientifically!

Matambiko ni mambo ya kiroho (spiritual) na sio kisayansi (scientifically) hivyo roho haina genetics Bali mwili.
 
Kama ni hivyo basi tukubaliane hakuna shetani,,, [emoji848][emoji849][emoji19]
Uko sahihi, hakuna kitu kinaitwa shetani kwenye muktadha halisia, huyo ni mhusika wa kubuni tu kwenye hadithi za kutungwa na watu
 
No, Shetani si kitu halisia, ni dhana kwenye mawazo yako katika kutafsiri matukio.

Unaweza kututhibitishia shetani yupo?
 
Uafrica ni ushetan uzungu na uarabu ni u Mungu asante sana ewe mtumwa
 
Sahihi kabisa.
 

No, Shetani si kitu halisia, ni dhana kwenye mawazo yako katika kutafsiri matukio.

Unaweza kututhibitishia shetani yupo?
namaanisha sifa zake ni za uhalisia. lakini hakuna kiumbe ambacho ni shetan
 
Ndugu, nimecheka kidogo! Sio kwa kukudharau hapana! Bali umegusa mambo ambayo nilikwambia tayari nilishaya experience kwa zaidi ya miaka 30,
Hayo ya kumuona babu yako nilisha yafanya miaka mingi, Tena sio kumuona tu, tulikuwa tunakula nae na kushiriki mambo mengi pamoja nae! Na sio Babu tu hata ndugu wengine waliokufa zamani walitokea na kuongea nao na kula nao!
mimi tokea nianze kutambika, sijawahi kula na babu yangu aliekufaga au ndugu walio kufaga. labda ndio maana mlianza ku experience mabaya.
ibada ni utamaduni wa watu husika.
Tena ibada yenye matokeo! Iwe unajua au hujui, mambo ya mizimu kuwa kwenye damu hiyo sio kweli inategemea na ushirika wako na hiyo mizimu!
mizimu maana yake wazazi wako wakale walio kufa. ni damu yako, na wapo kwenye vinasaba vyako. ukatae ukubali, wewe ni cheme hai kabisa ya babu wa baba yako na babu wa babu yako.
Otherwise unaongelea scientific! Genetics au vinasaba ni kweli viko kwenye damu kwasababu wazee wetu ndio wametuzaa tumecoppy genetics zao! Lakini hapa tunazungumzia MIZIMU kama ROHO na sio scientifically!
mizimu nimekwambia maana yake wwazee wako, haijalishi ni wamekufa au wako hai. na hii ikiwa na maana mizizi yako, wewe na matawi.
Matambiko ni mambo ya kiroho (spiritual) na sio kisayansi (scientifically) hivyo roho haina genetics Bali mwili.
matambiko ni mambo ya kimwili, yanayo leta experiences za kiroho kwa mtu. hakuna mambo ya kiroho bila kuanzia kwenye mwili.
 
Ila wewe una vinasaba vya ukibwetele huko unako sali. Ujuaji mwingi sana. Pia
 
Ila wewe una vinasaba vya ukibwetele huko unako sali. Ujuaji mwingi sana. Pia
Ukiona mtu anatukana au kukashifu ni dalili ya kukosa kitu kichwani tunaita TABULA LASA yaani kopo tupu!

Ni vyema wewe unayejifanya unajua ungetoa elimu yako na ungejenga hoja tofauti na yangu kwakuweka facts!

Lakini huna ulichoweka zaidi ya kashfa, Sasa huoni wewe ndiye kibwetere mwenyewe?!
 
Lusifa? Lusifa ni nani na anafanya kazi ipi mkuu

Huyu Lusifa ni wa wapi.
Kabla ya kuwa Shetani, alikuwa Malaika wa sifa, akimwabudu Mungu.

Baada ya kuasi, akawa Shetani. Kwa sasa anafanya biashara ya kudanganya wanadamu.
 

Matambiko ni tendo la kimwili kweli lenye maana ya kiroho! Maana hao mizimu hawako kwenye mwili Bali ni roho zilizokufa zamani! Unapotafuta mahusiano na roho, kinachoshirikiana hapo ni roho yako na roho zao! Matambiko ni ibada ya kuabudu roho za mababu waliokufa zamani. Kwakutafuta ushirika nao!
 
sio kuabudu, bali ku apriciate uwezo wao walipo hai, na kuomba mungu akupe uwezo kama wao, na ulinzi wao uwe pamoja nawe.

kisasa tunaweza sema ni kitenda cha ku activate DNA.

sala, na maombi inafanya kazi ya ku activate DNA Yako. wala haiusu kubadilisha mawazo ya mungu au yesu juu yako. bali una activate DNA.

KWAHIO; tufauti ya tambiko la kikristu na matambiko ya kiafrika, ni authority figure. wakristu wanamuweka yesu, au mitume wengine walio fanya makuuu katika historia yao, na waafrika tunawaweka ndugu zetu walio fanya makuu katika maisha yao.
 
Kabla ya kuwa Shetani, alikuwa Malaika wa sifa, akimwabudu Mungu.

Baada ya kuasi, akawa Shetani. Kwa sasa anafanya biashara ya kudanganya wanadamu.
Shetani+malaika+Mungu

Are all fragile thing they maybe killed by a whiff of science and common sense.
 
Sio Afrikq tu Ulaya kote kulikuwa na ibada za kishetani anzia ugiriki, wahindi,wachina wakorea ,wajapani n.k kwahiyo usidhani Kama ibada za mizimu ya waafrika tu ndio sio sahihi hata kwa wazungu pia hivyo hivyo ndio maana Kuna wahubiri wengi wanatoka uku kwenda kupeleka injili ulaya ibada halali ni ya mungu mmoja tu aliyeumba mbingu na nchi na si mizimu Wala mababu Ni kweli mizimu ipo na miungu mingine ipo lakini anayestahili kuabudiwa Ni Mungu mmoja tu ....wakristo tumeambiwa Usiabudu miungu mingine waislam wamekatazwa Shirki nadhani inamaanisha kumshirikisha Mungu na miungu mingine wanaoelewa kuhusu uislam watanisahihisha....

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…