Matambiko sio Ushetani

Matambiko sio Ushetani

Ndio maana nakwambia wewe to naandika kitu usichokijua na Sina muda wa kuandika story ndefu hapa,

Haya mambo ya matambiko sisi wenzako tumeishi nayo na tumeyafanya kwa zaidi ya miaka 30, sio mambo ya kusema "rudi kwa wazee wako!" Au "tambika kwa kitoroma au kiarabu!" Sisi tumepractise hayo mambo kwa miaka na miaka na tunayajua nje ndani, na hao wazee unao wasema ndio walikuwa makasisi wakuu wakuongoza ibada hizo mbovu!

Tukaona madhara yake makubwa na mabaya yakutusha sana! Tena yakutisha mno! Usichukulie poa! Tukakimbia mbio! Sasa wewe either umeyasoma au kuyasikia mahali ukaamua kuyapa support kwakuwa huyajui kiuhalisia na kiundani wake! Wenzako wako huko wanataka kujitoa wanashindwa! Huko ni kifungo kibaya sana! Ni utumwa mbaya mno! Usisikie!
Tunahitaji uzi mkuu andaa uzi washika day wajifunze...watu wabushi sana

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Yeah yote ni matambiko..Shida inakuja kwenye kafara za binadamu na masharti ya ajabu ajabu... ndio maana baadhi ya wazee wetu walihamia kwenye dini za ibrahimu.. lakini kila mtu atambike anavyoona ina faida kwake.
 
Shetani ni utendaji mwovu, hata binam akiwa mwovu sana tunaweza kumwita shetani,

Sasa pengine mtoa mada hajui hathari hasi za matambiko, madhara ya kutambikia miungu au mizimu!

Mimi ninae andika hapa najua tena nayajua haswa! Nimeyafanya kiuhalisia (practicing) sio dhana tu ya kuandika au kusikia! Na baada ya kuona madhara yake tukakimbia huko!

Matambiko ni ibada ya shetani totally! Kuabudu mizimu (miungu) kwa kutoa mnyama kama kafara etc Mbuzi, kondoo, kuku au ng'ombe! Vyakula , mimea au vinywaji ni kuabudu shetani! Na wanaofanya hivyo either kwakujua or kutokujua ni mawakala wa shetani! Either wanajua or hawajui! Amkeni!
Ww mlokole
 
Sio Afrikq tu Ulaya kote kulikuwa na ibada za kishetani anzia ugiriki, wahindi,wachina wakorea ,wajapani n.k kwahiyo usidhani Kama ibada za mizimu ya waafrika tu ndio sio sahihi hata kwa wazungu pia hivyo hivyo ndio maana Kuna wahubiri wengi wanatoka uku kwenda kupeleka injili ulaya ibada halali ni ya mungu mmoja tu aliyeumba mbingu na nchi na si mizimu Wala mababu Ni kweli mizimu ipo na miungu mingine ipo lakini anayestahili kuabudiwa Ni Mungu mmoja tu ....wakristo tumeambiwa Usiabudu miungu mingine waislam wamekatazwa Shirki nadhani inamaanisha kumshirikisha Mungu na miungu mingine wanaoelewa kuhusu uislam watanisahihisha....

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Maelezo yako ni kulingana na mtazamo wako tu.

Unaposema...
ibada halali ni ya mungu mmoja tu aliyeumba mbingu na nchi
Huu uhalali unatokea wapi na umejuaje kuwa ibada ya halali ni ya Mungu mmoja pekee.

Umeupima wapi uhalali huo na nani aliyekuhalalishia.

Wanaotambika siyo ibada halali? Kama siyo halali nani anawanyima huo uhalali.
Ni kweli mizimu ipo na miungu mingine ipo lakini anayestahili kuabudiwa Ni Mungu mmoja tu .
Hii ni kulingana na imani yako tu, hata wao wanaoabudu miungu mingi nao uhalali wao wanaupata kulingana na mafundisho yao. Kwahyo uhalali wao unatokana na point ya marejeleo ya mafundisho yao.

Mkikutana hzo pande mbili (mnaoabudu Mungu mmoja na waabuduo miungu mingi) hamuwezi elewana maana kila mmoja atapuuza cha mwenzake.

Unajua kuwa Mungu wako nae amekuwa categorized kwenye kundi la miungu ukienda kwenye jamii nyingine isiyomuamini?

Imani za wengine naomba mzitambue kwa heshima.
 
Back
Top Bottom