Spectophotometer
JF-Expert Member
- May 23, 2019
- 378
- 507
MATAMKO, JE, YANAJENGA AU KUZIDISHA UFA? JE, YANAPONYA AU YANAZIDI KUTONESHA?
NAJARIBU KUTAFAKARI.-TAFAKURI YA SHEIKH SHAMS ELMI.
1. Utangulizi
Katika mazingira ambayo Taifa letu linapitia changamoto ya kijamii na kisiasa inayohitaji busara, uzalendo na utulivu, ni muhimu sana kila Taasisi zikiwemo za kidini, kiraia na kijamii kuzingatia uzito wa kauli katika MATAMKO wanayoyatoa na hitajio la wakati huu wenye hasasia (sensitivity) za kisiasa na kihisia
Hotuba ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la 13 imeweka bayana juu ya:
a. Kuunda Tume maalumu ya uchunguzi ndani ya siku 100
b. Kuachiliwa vijana waliofunguliwa mashtaka mazito baada ya kufuata mkumbo wakati wa vurugu
c. Kutoa Dira ya Maendeleo ya miaka 5 yenye ajenda za mageuzi mkubwa ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.
d. Kuanza mchakato wa marekebisho ya Katiba, ambayo ni madai ya muda mrefu ya Watanzania
e. Kunyoosha tena mkono wa maridhiano.
Katika mazingira kama haya, na hotuba ya matumaini kama hii, ni busara, hekima na uzalendo Asasi zote muhimu kuunga mkono mchakato wa kitaifa unaolenga kupata muarubaini wa kudumu wa matatizo yote yanayo lalamikiwa.
2. Je, matamko yanajenga au KUZIDISHA UFA?
Katika siku za karibuni, yamejitokeza matamko kutoka kwa baadhi ya taasisi na viongozi wa kidini yenye kuashiria:
■ Kutoridhishwa kwao na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na mamlaka.
● Kukosa Imani na tume ya uchunguzi wa ndani na kutaka iwepo tume ya kimataifa.
● Kukariri kauli zenye taswira ya kukashifu hadhi ya Taifa bila ushahidi.
■ Kutafsiri matukio kwa misingi ya hisia kuliko ushahidi
Kuhukumu kabla ya uchunguzi ni kinyume na misingi ya Haki.
Kanuni za kiutawala, kitaaluma na kidini zinatambua kuwa:
( Hukumu yoyote bila uchunguzi wa kina ni chanzo cha dhulma na mgawanyiko.)
Ikiwa Serikali imeonyesha utayari wa kufanya uchunguzi huru na kuchukua hatua, kwa nini taasisi zingine zitoe hitimisho na maelekezo ?
Kauli inayokaririwa na baadhi ya viongozi wa dini na wanaharakati kwamba “Taifa limepoteza heshima” bila vielelezo ni hatari, Heshima ya nchi yetu imejengwa kwa miongo mingi na kwa gharama kubwa sana, ndio nchi iliyosimamia uhuru wa nchi za kusini mwa Afrika, kutoa hukumu nyepesi kwa Taifa lenye heshima nzito kama Tanzania sidhani kama ni tafakuri iliyotokana na ibada ya kiroho.
Hotuba ya Mh. Rais wakati akilifungua Bunge la 13 ilihudhuriwa na kusikilizwa na wawakilishi wa mataifa mengi bila kuwa na taaswira ya kubezwa.
Kauli zinazoashiria Taifa kupoteza heshima bila ushahidi ni hatari kwa sababu:
Zinachafua taswira ya taifa kimataifa
Zinawatisha wawekezaji na watalii
Zinawakatisha tamaa wananchi
Zinaweza kutumiwa kama silaha ya kisiasa na waharibifu maadui wa nchi yetu.
Kutanguliza Hisia kabla ya ushahidi:
Kutoa matamko yanayotoa hukumu bila kusubiri tume maalumu kuchunguza chanzo halisi, waasisi, wapangaji, walionufaika na mgogoro huo, ni sawa na🙁 Kutibu dalili bila kugusa ugonjwa.)
3. Mifumo ya Kimataifa ya Kuvuruga Nchi (Destabilization Patterns)
Ni muhimu kwa wasomi wazalendo, wanasiasa wazalendo na Taasisi za kiraia za kizalendo kuwa makini na mifumo ya kimataifa yenye malengo ya kupenyeza ajenda zao za kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa kuchochea vurugu katika nchi ambazo hazikubali sera zao.
Kwa kuzingatia tafiti za kimataifa (International Crisis Group, Brookings, AU Peace & Security Reports, CEJIL, Latin American Studies Association), ipo mifano ya nchi ambazo zilikumbwa na machafuko makubwa kupitia:
● Taasisi za ndani kutoa matamko makali ya kisiasa
● Mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu kuingilia mambo ya ndani ya nchi hizo kwa msingi isiyozingatia historia, tamaduni, muundo wa kisiasa wa ndani ya nchi hizo.
4. Makanisa au Taasisi za dini kushiriki katika misukumo ya kisiasa badala ya upatanishi
a. Afrika
DR Congo (2015–2018)
Mchanganyiko wa matamko makali na mitazamo hasi ya baadhi ya taasisi za dini ndani ya nchi zilikaribisha shinikizo la NGOs za kimataifa ambazo zilifadhili maandamano yaliyopelekea vifo na vurugu kubwa.
Sudan (2019–2023)
Mashirika ya kimataifa na mitandao ya kijamii iliyokuwa inaendeshwa na wanaharakati waliopo nje ya Sudan yaliendesha kampeni kali kwa Gen Z wa Sudan zilizoingiza nchi kwenye maandamano yasio na mwisho na Hatimae jeshi kuchukua nchi katika mapinduzi ya kijeshi na hatimaye nchi imeingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, Leo hii wasudani ni wakimbizi na wengine tunao hapa Tanzania katika vyuo vyetu vikuu.
Kenya (2007 na 2017)
Nchi jirani na ndugu ambayo raia zake Wana undugu wa nasaba na wa tanzania, tumekuwa na utani wa jadi na mizaha mitandaoni, lakini hivi karibuni utani huo wa jadi umegeuka ghafla kwa baadhi yao hususan wanao jiitaa wanaharakati kwa kushiriki dhidi ya utulivu wa Tanzania, wanaharakati Hao wamejisahaulisha kabisa Mivutano mikubwa ya uchaguzi iliyotokea katika nchi yao na kuzi huusisha sana NGOs za kimataifa na baadhi ya taasisi za dini na kusababisha maafa na mpasuko wa kijamii ambao hadi Leo bado athari zake zinawatesa.
Hitimisho na Wito wa Kitaifa
Katika kipindi ambapo Taifa limeamua kuchukua hatua za kisheria na za maridhiano kupitia:
Tume ya uchunguzi
Mkono wa maridhiano
Marekebisho ya Katiba
Kuachiwa kwa vijana waliofuata mkumbo
Dira ya miaka 5 yenye mageuzi mkubwa ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Ni busara na uzalendo kwa taasisi zetu za dini na kiraia kuzingatia:
Lugha ya kuponya, si kutonesha
Matamshi yanayojenga, si kuhukumu
Mchakato wa kitaifa, si ajenda binafsi
Ushahidi, si hisia
Wakati serikali imeanza mchakato wa uchunguzi rasmi, kutoa “hukumu” kabla ya uchunguzi ni sawa na kuharibu mbegu kabla haijamea.
Mungu Ibariki Tanzania.