Matamko ya CWT kuhusu Mfumo wa PEPMIS yanatuchanganya, Serikali iweke wazi kuhusu upandishaji wa madaraja ya Walimu

Matamko ya CWT kuhusu Mfumo wa PEPMIS yanatuchanganya, Serikali iweke wazi kuhusu upandishaji wa madaraja ya Walimu

jksang

New Member
Joined
Jul 29, 2025
Posts
2
Reaction score
0
Napenda kuwasilisha waraka huu nikiwa miongoni mwa Walimu wengi nchini ambao wameathirika kwa taarifa zinazotolewa na Chama chetu kuhusu utaratibu wa kupandishwa madaraja kwa kutumia Mfumo wa Public Employee Performance Management Information System (PEPMIS).

Hivi karibuni, CHAMA CHA WALIMU TANZANIA - CWT kupitia Viongozi wake kimekuwa kikitoa matamko kwa Walimu kuwa mfumo wa PEPMIS hautatumika tena kama kigezo cha kupandishwa madaraja.

Hata hivyo, baada ya kufuatilia kwa Maafisa Utumishi katika halmashauri zetu, imebainika hakuna waraka rasmi kutoka Serikalini (TAMISEMI au UTUMISHI) unaoonyesha mabadiliko hayo.

Maafisa hao wameendelea kusisitiza kuwa PEPMIS bado ni sehemu ya vigezo muhimu vinavyotumika kupima sifa za Mwalimu kupandishwa daraja.

Hali hii imeleta mkanganyiko mkubwa kwa Walimu wengi ambao sasa hawajui mwelekeo sahihi wa Kisheria au kiutumishi. Matokeo yake ni:

1. Walimu kutopata tathmini kupitia PEPMIS kwa imani kuwa si lazima tena – hivyo kukosa sifa za kupandishwa madaraja.

2. Kutokea kwa sintofahamu kati ya walimu, viongozi wa shule, na maafisa utumishi.

3. Kupungua kwa ari ya kazi kwa walimu wanaohisi kupotezewa fursa zao kwa taarifa zisizo rasmi.

Kwa msingi huo:

-------------------------​

MAOMBI YETU KWA CWT:
1.
Kutoa tamko la marekebisho au ufafanuzi rasmi juu ya matumizi ya PEPMIS – ikiwa limepokelewa agizo la Serikali, lifafanuliwe na kuambatanishwa na waraka husika.

2. Kushirikiana kwa karibu na TAMISEMI/UTUMISHI ili kuhakikisha taarifa zinazotolewa kwa Wanachama wake ni sahihi na zenye uthibitisho.

3. Kuhakikisha walimu hawapotezi haki zao kwa kusababishiwa mkanganyiko na taarifa zisizo rasmi.

-------------

Tunathibitisha kuwa bado tunaiheshimu CWT kama chombo muhimu cha kutetea maslahi ya Walimu, lakini tunasisitiza kuwa taarifa zozote zinazohusu ajira, vigezo vya utumishi, na miongozo ya Serikali zinapaswa kutolewa kwa umakini mkubwa na kwa uthibitisho wa maandishi ya kiserikali.

Tunatarajia majibu na mwelekeo mpya kutoka kwa uongozi wa CWT.

---

Wako katika kutetea haki ya Mwalimu,


Pia soma ~ Prof. Shemdoe: Uzembe wa Ma-Afisa Rasilimali Watu katika Mfumo wa PEPMIS umezuia Watumishi kutopanda daraja
 
Mfumo wenyewe una changamoto nyingi sana. Karibia mwezi sasa mpango kazi wa mwaka haujapitishwa na wakuu wa idara au vitengo kwa kisingizio kuwa hawawaoni watu walio chini ya idara/vitengo vyao.
 
Hivi suala la walimu walioko masomoni limekaaje ktk suala la kupanda madaraja?
 
Back
Top Bottom