Matamshi ya mbunge Simai wa Zanzibar yazua taharuki ndani ya Chama cha Mapinduzi, yaibua ishu zake

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
435
Reaction score
733
Anaitwa Simai Mohammed Said. Awali alikuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa Jimbo la Tunguu (CCM). Baadaye Rais Samia akamteua kuwa Mbunge (wa kuteuliwa) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika zile nafasi 10 za Rais.

Hivi karibuni mbunge Simai amezua mjadala uliyosababisha taharuki ndani ya chama chake cha CCM kufuatia kutoa matamshi bungeni yenye sura ya U-Zanzibar dhidi ya U-Tanganyika huku wengi wakitafsiri ni vita vya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2030.

CHOKOCHOKO ZA SIMAI ZILIANZIA HAPA?
Awali, mbunge huyo alisimama bungeni na kudai kuwa, wapo makada wa Chama cha Mapinduzi wanalenga urais wa mwaka 2030 na hivyo kumkosea heshima Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Mbunge huyo akichangia Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara, Mei 22, 2026 alisema yeyote anayehisi atapata u-rais mwaka 2030 kwa kutomheshimu Mwenyekiti, hatafanikiwa.

Wengi waliyoisikia hotuba yake hiyo walisema alimlenga Mbunge wa Gairo kupitia chama hicho, mheshimiwa Ahmed Shabiby aliyesema atagombea u-rais 2030 ili kupambana na rushwa na ufisadi ndani ya nchi hii.
Hata hivyo, maneno ya mheshimiwa Shabiby kugombea urais 2030 yalichukuliwa kama utani kwani wakati akiongea, mbunge mmoja wa nyuma yake alisema maneno yaliyomfanya mbunge huyo amwambie 'atakuwa makamu wa rais' na wabunge walicheka.

Mbunge Simai alisema Watanzania wasimame na Samia hata mwaka 2030 bila kujua kuwa, mwaka huo utakuwa kikomo cha rais aliyopo madarakani kwa sasa kugombea tena!

Mitandaoni akatrendi yeye, watu wakitoa maoni mbalimbali. Wengi wakimponda kwamba, matamshi yake yanaonesha wazi anasimamia Uzanzibar zaidi kuliko Utanzania na muungano.

ALIANZISHA TENA, AZUA MJADALA MKUBWA MITANDAONI
Kabla figisu hiyo haijapoa, Juni 2, 2026 Simai tena. Akiwa bungeni kuchangia Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, ametoa matamshi makali zaidi ya yale ya awali hali iliyozua taharuki mitandaoni hadi ndani ya chama chake ambayo hadi sasa hakujapoa.

Mjadala mkubwa kuhusu matamshi yake ni matumizi ya lugha katika siasa, ishara za kidini na wajibu wa viongozi wa umma katika uchaguzi na matumizi ya maneno wanayoyatumia wakiwa hadharani.
Akichangia bungeni siku hiyo, Simai alisema waziwazi kuwa, licha ya jitihada za Rais Samia kuleta maendeleo ya nchi, lakini kuna kiongozi mmoja wa juu serikalini ni Yuda (kwa maana ni msaliti kama Yuda Eskalioti wa kwenye Agano Jipya aliyemsaliti Yesu).

Ingawa hakumtaja kwa jina kiongozi huyo, lakini wajuzi wa kuunganisha matuko mbalimbali, walisema alimlenga Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Emmanuel Nchimbi kutokana na simulizi ya kihistoria aliyoiweka wazi.

Katika madai yake, Simai alisema kuwa kiongozi huyo amewasaliti baadhi ya watu aliyokuwa nao kisiasa, amewaumiza wanasiasa, watendaji wa serikali na wafanyabiashara na sasa anajaribu kujijenga upya kisiasa kwa kutafuta huruma za wananchi kupitia shughuli mbalimbali za kijamii na kidini.

Aidha, alidai kuwa kiongozi huyo anajaribu kujenga taswira kwamba yeye alikuwa karibu sana na Hayati John Magufuli, licha ya changamoto za kisiasa alizowahi kukumbana nazo katika kipindi cha utawala wake.
Mbali na matarajio yake ya kuungwa mkono na wengi wakati 'akihubiri' bungeni, badala yake aliambulia makofi machache huku watu mitandaoni wakianza kumnanga na kuweka wazi baadhi ya michango yake bungeni.

Wengine wamemwaga skendo zake ambazo huenda zilikuwa zikijulikana na wachache, hususan kwa upande wa Zanzibar.

ALIJIUZULU UWAZIRI KISA UHABA WA POMBE MAHOTELINI ZANZIBAR
Novemba 2023, Sumai Mohamed Said alikuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar. Lakini Januari, 2024 ajiuzulu siku mbili baada ya kutangaza uhaba wa pombe kwenye mahoteli na migahawa ya Zanzibar.
Simai alitangaza kujiuzulu akisema ni kutokana na kile alichokiita 'mazingira ya kazi yasiyo rafiki.'
Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa mambo ya siasa visiwani humo walisema kwamba, kuna jambo lilijificha nyuma ya pazia la kujiuzulu kwake.

Soma Pia: Mbunge Simai: Kuna Yuda Msaliti ndani ya Serikali hili anatafuta huruma kanisani

TUHUMA ZAKE NZITO ZINAZOMZUNGUKA
Inadaiwa alijiuzulu uwaziri mwaka 2024 kwa kulazimishwa (shinikizo) baada ya kugindulika anafanya biashara ya kusafirisha mabinti nje ya nchi kwa lengo la kuwauza (human trafficing).
Aidha, inadaiwa alilazimika kujiuzulu baada ya kubainika anauza vileo zikiwemo bia huko Pemba (Zanzibar Visiwani).
Mwaka 2025, aligombea Uwakilishi kwenye Bunge la Zanzibar lakini wajumbe 'walimkata kichwa' kufuatia skendo za kuuza mabinti nje. Ndipo akateuliwa kuwa mbunge kupitia viti 10 vya rais.

MAKADA UV-CCM, WANAHARAKATI WAMSHUKIA, WATAKA AWAJIBISHWE
Tayari baadhi ya makada wa CCM kutokea Umoja wa Vijana (UVCCM), wakiwemo wanaharakati kama vile Ahmed Kombo, wameibukia mitandaoni wakitaka kamati ya maadili ya chama imchukilie hatua za kinidhamu mbunge huyo wakidai kwamba, kwa nafasi yake ni utovu wa nidhamu kumsema Makamu wa Rais popote pale.
Wengine wamekwenda mbali wakihoji ni kwa nini mbunge huyo alisimama bungeni kumsema kiongozi ambaye anakaimu nafasi ya urais wa nchi kipindi hiki ambacho rais yupo ziara nje ya nchi!
Wengine walizidi kwenda mbali zaidi wakituhumu kuwa, kama mbunge huyo hataitwa kwenye kamati ya maadili ya bunge, basi matamshi yake yana baraka kutoka katika kiti chenye sauti kubwa.

SPIKA ALIYEMRUHUSU ACHUKUE DAKIKA KUTOA MATAMSHI YAKE ALAUMIWA
Wengine walimshangaa kiongozi wa bunge wa siku hiyo (alikuwa naibu spika) kwamba, ni kwa nini alimwacha Simai amalize kusema madai yake na kuingia kwenye 'hansadi' ya bunge itakayotumika miaka na miaka.
Hata hivyo, Naibu Spika mheshimiwa Daniel Sillo siku hiyo, alimkatisha akimtaka aende kwenye hoja moja kwa moja licha ya kwamba, tayari ujumbe wa mbunge huyo ulishasikika na kujulikana duniani kote.

ASKOFU AWASAKAMA WABUNGE WALIYOPIGA MAKOFI
Wakati mambo yakiwa bado ya motomoto, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza ameliandama Bunge kwa kuruhusu mjadala uliomfananisha Makamu wa Rais na msaliti 'Yuda' kuingia kwenye kumbukumbu rasmi za Hansard.
Kupitia tahadhari nzito aliyoitoa Juni 4, 2026 (leo), Askofu Bagonza amesema dhihaka hiyo iliyotolewa na mbunge Mzanzibari dhidi ya kiongozi Mtanganyika ni ufa hatari katika Muungano, huku akishangaa wabunge waliopiga makofi na kuwataja kuwa, ni sawa na "ma-tumbili" wanaoshangilia pori linaloteketea kwa moto bila kujua wao watakosa pa kulala.

TETESI ZA KISHUGHULIKIWA

Kwa mujibu wa machapisho ya mitandaoni ambayo hayana msemaji maalum, leo Juni 4, 2026, asubuhi ya leo, mbunge huyo amepewa barua na Katibu wa Wabunge wa CCM akitakiwa kujieleza kimaandishi ni kwa nini alitoa matamshi yenye kuchonganisha viongozi!
Aidha, inadaiwa ametakiwa kumtaja kwa jina mtu aliyemwita Yuda huku akipewa saa ishirini na nne za utekelezaji.
Screenshot_20260604_164432_Google.jpg
 
Mwaka 2025, aligombea Uwakilishi kwenye Bunge la Zanzibar lakini wajumbe 'walimkata kichwa' kufuatia skendo za kuuza mabinti nje. Ndipo akateuliwa kuwa mbunge kupitia viti 10 vya rais.
Hii tuhuma mbona inaiichafua 'nchi'. Please ebu itenganishe 'nchi' na hii tuhuma tafadhali. Wahusika please fanyieni kazi hili jambo.
 
Aidha, inadaiwa ametakiwa kumtaja kwa jina mtu aliyemwita Yuda huku akipewa saa ishirini na nne za utekelezaji.View attachment 3601135
Screenshot_20260604-133242~2.png
 
Ni nukuu verse ya marehemu Albert mangwea _ wimbo maskini wenzangu..

""Wazanzibar WAMECHOKA kutanga na nyika"""
 
Back
Top Bottom