RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
Mhadhara - 47:
Inakera!!
Siku hizi hakuna raha ya kutumia smartphone, ukifungua APP yoyote kwenye simu (kabla hukuendelea na mambo mengine) unaletewa matangazo ya biashara, na matangazo mengi ni MKOPO ONLINE. Unalazimishwa (bila ridhaa yako) utazame tangazo kisha ndo uendelee na mambo mengine kwenye simu yako.
Hii kero ya kuwatumia watu matangazo ya biashara kwenye smartphone ambayo yanakula "MB" inaudhi kupita kiasi. Nitumie ukurasa huu kuwaomba wahusika (TCRA, n.k) ambao wanahusika kudhibiti/kufuatilia/kuwaelekeza watu kuhusu masuala ya mitandao watafute mbinu nyingine ya kuwatangazia watu biashara.
Ikiwezekana itafutwe njia mbadala ya kuwafikishia watu matangazo ya biashara kwenye smartphone zao. Kwa mfano; kuwe na namba kama vile passwords ambazo mtu ambaye atahitaji kusoma tangazo lolote atabofya namba husika.
Haiwezekani nimenunua simu kwa hela zangu, nimesajili laini kwa taarifa zangu, na nimejaza salio kwa pesa zangu halafu natumiwa tangazo la biashara (mfano video) ambalo linatumia "Internet bundle" yangu, tena nalazimika kulitazama tangazo mpaka mwisho, au badala ya kuendelea na mambo mengine kwenye simu yangu nalazimika kwanza kutafuta kipengele cha kusitisha tangazo hilo, hii inakera.

Right Marker
Dar es salaam